Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Itakuwa vipi kamati ya EPA itakapoleta taarifa ambayo kila jambo anatakiwa athibitishe Ballali kama vile nani alimwndikia vimemo vya akasaini.
Au walete taarifa kuwa yale ni makampuni ya Ballali na Ditto na kwa sababu wameshakufa no Mo MONEY

Hoja yako nzuri kweli. Lakini sidhani kama Balali ndio alikuwa kila kitu ndani ya BOT. I mean, haiwezekani kwamba yeye ndio alikuwa mhasibu, karani etc. Kwahiyo katika kuidhinisha malipo haya ya EPA, kuna watu wengi wenye information. Mimi nimekiri kwamba Balali huenda ndio alikuwa shahidi mkuu, lakini naamini kabisa wako mashahidi wengine kwenye hili.
 
Kijiwe kitafungwa kwa kuandika kwamba aliyemuua Ballali ni Rostam Aziz?

Gazeti linaweza kufungiwa lakini sio JF. Ukifungia JF leo, zitakuja zingine 20.

Mimi siamini hii habari ya sumu kwamba ni kweli. Wewe utalishwa sumu, ukimbilie USA, ukae miezi tisa, hakuna hata daktari mmoja ambaye anaweza kusimama na kusema wazi kwamba umelishwa sumu?

Hata KGB walipotaka kumuua yule jamaa wa Ukraine bado ilijulikana, hata Polonium 210 ya UK bado ilijulikana, sasa hii sumu ya gavana wetu ni sumu gani hiyo?

Hili suala la sumu mimi nililipinga toka mwanzoni na sasa ndio natapata sababu kubwa za kulipinga. Sumu ilikuwa ni sababu ya Ballali kutoroka TZ na kupotelea kimoja USA wakati wanaandaa mipango mingine.

Kuna kampeni kubwa ya kuwadanganya Watanzania juu ya hili jambo la Ballali.
 
Kijiwe kitafungwa kwa kuandika kwamba aliyemuua Ballali ni Rostam Aziz?

Gazeti linaweza kufungiwa lakini sio JF. Ukifungia JF leo, zitakuja zingine 20.

Mimi siamini hii habari ya sumu kwamba ni kweli. Wewe utalishwa sumu, ukimbilie USA, ukae miezi sita, hakuna hata daktari mmoja ambaye anaweza kusimama na kusema wazi kwamba umelishwa sumu?

Hata KGB walipotaka kumuua yule jamaa wa Ukraine bado ilijulikana, hata Polonium 210 ya UK bado ilijulikana, sasa hii sumu ya gavana wetu ni sumu gani hiyo?

Hili suala la sumu mimi nililipinga toka mwanzoni na sasa ndio natapata sababu kubwa za kulipinga. Sumu ilikuwa ni sababu ya Ballali kutoroka TZ na kupotelea kimoja USA wakati wanaandaa mipango mingine.

Kuna kampeni kubwa ya kuwadanganya Watanzania juu ya hili jambo la Ballali.

Kikubwa zaidi ni pale wanaJF wanaposhadadia kuhusu kunyweshwa sumu huku. Ukicheki huku ndani kuna threads kibao kuhusu kunyweshwa sumu kwa Balali. Tukiomba ushahidi tunaitwa critics!
 
Inaeleweka Mburushi kafanya kweli lakini alitumia aina gani ya sumu??????
 
Kijiwe kitafungwa kwa kuandika kwamba aliyemuua Ballali ni Rostam Aziz?

Gazeti linaweza kufungiwa lakini sio JF. Ukifungia JF leo, zitakuja zingine 20.

Mimi siamini hii habari ya sumu kwamba ni kweli. Wewe utalishwa sumu, ukimbilie USA, ukae miezi tisa, hakuna hata daktari mmoja ambaye anaweza kusimama na kusema wazi kwamba umelishwa sumu?

Hata KGB walipotaka kumuua yule jamaa wa Ukraine bado ilijulikana, hata Polonium 210 ya UK bado ilijulikana, sasa hii sumu ya gavana wetu ni sumu gani hiyo?

Hili suala la sumu mimi nililipinga toka mwanzoni na sasa ndio natapata sababu kubwa za kulipinga. Sumu ilikuwa ni sababu ya Ballali kutoroka TZ na kupotelea kimoja USA wakati wanaandaa mipango mingine.

Kuna kampeni kubwa ya kuwadanganya Watanzania juu ya hili jambo la Ballali.

Mkuu Mtanzania
Mtu kulishwa sumu kwa kiwango cha Balali ama mimi na wewe ni daktari anaweza kujua na ndugu zake ama zako wa karibu na wakiamua kusema watasema na wakiamua kuendelea kuuguza ni uamuzi wao .Hili liwe wazi maana mwisho kila kitu kitakuja nje .

NO JF haiwezi kufungwa na yeyote acheni hisia za kuwapa kichwa kwamba wanaweza maana hii nis sauti ya Umma na kufunga hiki ni kufungua kingine na kingine .Kwanza wanafungia wapi ? Hii haiko Brela .
 
****Hata KGB walipotaka kumuua yule jamaa wa Ukraine bado ilijulikana, hata Polonium 210 ya UK bado ilijulikana, sasa hii sumu ya gavana wetu ni sumu gani hiyo?**
SUMU ILIOMUUA """KOLIMBA""DODOMA NA ""MTOTO WA MALECELA"" NDIO ILIOMUUA BALALI ...ILA YA KOLIMBA ILIONGEZWA NGUVU ZAIDI
MTANZANIA NATUMAINI UKIFWATILIA UKO UNAWEZA KUTULETEA CONTENTS ZA HIYO SUMU....NA KUWEZA KUJADILIWA....LABDA OMBI LANGU KWA WALE WANACHAMA WA CCM MTAKAOITWA DODOMA HALI MKIJUA ZALI LAWEZA KUWATOKEA NAOMBENI MSIKARIBIE MAUTI MNAYOIONA ""CCM SASA NI WAUAJI HALISI"""" NA WALA SI CHAMA TENA ...LAITI NYERERE ANGAJUA AMEACHA MAFISADI PEKEE ANGEWEZA KUSIKITIKA LAKINI KUMBE AMEACHA CCM YA WAUAJI WATUPU TENA KWA SUMU JAMANI NINGEPENDA KUJUA VYAMA VYENYE MREGO W MAUAJI KAMA CCM ..DUNIAN KOTE TUWENAVYO MAKINI
 
MKUU MTANZANIA

NATUMAINI WEYE ULIE KARIBU NAO UKO WAWEZA KUTUELIMISHA NINI CHA KUFANYA AMA WAZAZI WETU WENGINE CCM ..JE WAKIITWA WAJIBUJE KWA UONGOZI..AU WAKIMBILIE CCBRT KULAZWA NA KUTAFUTA VYETI KISA KUHIOJIWA ..KAZI IPO NYIE WATU HAWA WAUAJI HAMWUWAONI AU MPAKA WAJE KUGINGA NYUMBA KWA NYUMBA NA MAPANGA NDIPO MTAKAPOIOGOPA CCM..HAYA KAZI KWAO
 
****Hata KGB walipotaka kumuua yule jamaa wa Ukraine bado ilijulikana, hata Polonium 210 ya UK bado ilijulikana, sasa hii sumu ya gavana wetu ni sumu gani hiyo?**
SUMU ILIOMUUA """KOLIMBA""DODOMA NA ""MTOTO WA MALECELA"" NDIO ILIOMUUA BALALI ...ILA YA KOLIMBA ILIONGEZWA NGUVU ZAIDI
MTANZANIA NATUMAINI UKIFWATILIA UKO UNAWEZA KUTULETEA CONTENTS ZA HIYO SUMU....NA KUWEZA KUJADILIWA....LABDA OMBI LANGU KWA WALE WANACHAMA WA CCM MTAKAOITWA DODOMA HALI MKIJUA ZALI LAWEZA KUWATOKEA NAOMBENI MSIKARIBIE MAUTI MNAYOIONA ""CCM SASA NI WAUAJI HALISI"""" NA WALA SI CHAMA TENA ...LAITI NYERERE ANGAJUA AMEACHA MAFISADI PEKEE ANGEWEZA KUSIKITIKA LAKINI KUMBE AMEACHA CCM YA WAUAJI WATUPU TENA KWA SUMU JAMANI NINGEPENDA KUJUA VYAMA VYENYE MREGO W MAUAJI KAMA CCM ..DUNIAN KOTE TUWENAVYO MAKINI
Total crap. Story za vijiwe vya kahawa. Mkiombwa ushahidi mnakuwa wakali. I'm not buying that.
 
Ansbert Ngurumo

NILIWAHI kudokeza mambo mawili kwenye safu hii kuhusu aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), hayati Daudi Ballali.

Kwanza nilihoji kama ugonjwa wake ulitokana na kulishwa sumu. Sikujibiwa. Pili, nilisema kwamba taarifa za watu wanaojua mambo yanayoendelea serikalini zilieleza kuwa Ballali asingerejea Tanzania.

Yote mawili yamekuwa. Ballali hakurejea. Sasa taarifa mpya zinasema kwamba kabla hajafa alimtaja mtu aliyemlisha sumu iliyosababisha ‘ugonjwa’ wake, hadi akakimbizwa nje ya nchi kutibiwa.

Watu wake wa karibu wamemnukuu hayati Ballali akimtaja mtu aliyemlisha sumu. Yawezekana hii ni kauli mojawapo ambayo wanafamilia walitaka kuiweka hadharani katika mkutano na wanahabari. Tuwape muda.

Kwa sababu zinazoeleweka, hatutamtaja ‘muuaji’ huyo hapa kwa sasa. Lakini kadiri siku zinavyokwenda, iwapo na sisi hatutalishwa sumu, kama hatajitaja, tutamtaja siku moja, katika kuweka vema historia ya mapambano dhidi ya ufisadi.

Siku mambo yote yatakapokuwa yamewekwa vizuri, Watanzania watakaokuwa hai wakati huo watapata fursa ya kutambua jinsi ufisadi ulivyowahi kuwa sehemu nyeti ya utawala wa nchi hii.

Kitu kimoja hakitawashangaza. Nacho ni sura na majina yanayozungumzwa na kuhusishwa na ufisadi katika serikali za awamu ya tatu na ya nne.

Hata katika hili la sasa, mtu yule yule aliyetajwa na hayati Ballali, kwamba ‘ndiye alinilisha sumu,’ ni kigogo yule yule ambaye amekuwa anahusishwa katika mazingira na matukio mengi ya ufisadi wa kupindukia.

Yumo katika orodha ya mafisadi 11 walioanikwa hadharani na Dk. Willibrod Slaa, Septemba 15, 2007 katika mkutano wa hadhara wa Temeke Mwembe Yanga, Dar es Salaam.

Yumo miongoni mwa waasisi wa kaulimbiu ya ‘Maisha bora kwa kila Mtanzania.’ Ni mmoja wa watu ambao kwa sasa wanaangaliwa kwa macho ya chuki, kwa kuwasababishia Watanzania maisha duni.

Ni mmoja wa vinara waliofadhili na kutangaza kwa nguvu zote dhana ya ‘Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya’ ambayo imekuwa ikifupishwa kwa kuitwa ANGUKA; na kuwa kiini cha anguko la Tanzania.

Ni muasisi wa dhana iliyoangusha uchumi wa nchi na kudunisha maisha ya Watanzania, huku akiasisi dhana nyingine ya kimya kimya ya ‘Maisha bora kwa kila fisadi.’ Mtu huyu huyu aliyetajwa na hayati Ballali kwamba ndiye alimlisha sumu, yumo miongoni mwa vigogo wanaotuhumiwa kulihujumu taifa kwa kuunda mitego ya uchotaji wa pesa za wananchi kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu (EPA).

Ndiye anayetajwa kuwa mmoja wa vigogo walionufaika na pesa za Richmond; mtu ambaye inasemekana alikula njama kuchomoa mafaili ya Richmond katika kumbukumbu za msajili wa makampuni ili ‘kuiingiza mjini’ Kamati ya Bunge iliyokuwa inachunguza tuhuma dhidi ya kampuni hiyo.

Ni kigogo huyo huyo ambaye kwa wakati fulani alidhaniwa kuwa na hisa katika urais wa Jakaya Kikwete, hata ikawalazimu wanahabari kumhoji rais moja kwa moja kuhusu suala hilo.

Ni mtu huyo huyo ambaye miezi michache iliyopita, kabla ya masuala ya ufisadi kupamba moto, alikuwa akidhaniwa kuwa mfadhili na mkombozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM); na ambaye baadhi ya watu wanaojua jinsi awamu hii inavyofanya kazi, waliwahi kudokeza kwamba ‘ndiye rais’ wa Tanzania asiyeishi Ikulu, anayeendesha nchi atakavyo kupitia kwa rais aliyechaguliwa, anayeishi Ikulu.

Lakini kikubwa kinachomgusa na kumfadhaisha kigogo huyu ni taarifa kwamba ndiye ameshiriki kwa kiasi kikubwa kuchota mabilioni ya EPA kutoka BoT na kuyazungusha kwenye miradi yake, huku akiingiza mengine kwenye kazi za CCM, zikiwamo harakati za kampeni za uchaguzi mkuu.

Kutokana na ukaribu wake na walio madarakani, serikali imeshindwa hata kuchukua hatua madhubuti dhidi ya walioiba pesa za EPA; ikasema haiwajui, lakini ikakiri kwamba wanarudisha pesa taratibu! Serikali hii hii ikashindwa kuiweka hadharani ripoti kamili ya uchunguzi wa wizi wa EPA kama ilivyoandaliwa na wataalamu wa Ernst & Young.

Serikali ikamficha mtu wake kwa jinsi ile ile ilivyokuwa inaficha ugonjwa wa Ballali, nchi aliko na hospitali alikolazwa, huku baadhi ya maofisa wa serikali wakisemekana kumtembelea mgonjwa wao kushuhudia kama bado yuko hai.

Usiri wa serikali katika suala la Ballali umeiaibisha yenyewe, na umeondoa kabisa imani ya wananchi kwa serikali hii. Umeonyesha unyonge na udhaifu mkubwa wa watawala wa sasa, na kudhihirisha wasiwasi ambao tumekuwa nao siku zote, kwamba nchi hii sasa inaendeshwa na mafisadi.

Lakini huu umekuwa usiri uliokithiri, kiasi cha serikali kudiriki kuficha hata kifo chake, hadi gazeti hili lilipoibua taarifa hizo, na kulazimisha serikali kukiri.

Nawaonea huruma watumishi wa serikali hii wasio mafisadi, lakini wanaofunzwa kutunza siri za mafisadi.

Tabia hii ya serikali ndiyo imewafanya wananchi wengine kudhani kwamba hata Ballali mwenyewe hajafa; kwamba ni njama za mafisadi kumficha kabisa ili kuua ushahidi katika suala la EPA.

Lakini hata wale wanaoamini kwamba amefariki dunia, wanajenga hoja hiyo hiyo; kwamba wamemuua ili kuficha siri yao.

Kwa kifo cha Ballali lipo jambo ambalo hatutalijua kamwe kuhusu wizi wa EPA. Maana kabla hajafa, Ballali mwenyewe alisema hakula hela za EPA, bali anawajua waliozichota, na kwamba asingekufa peke yake.

Sasa wamemtanguliza wakidhani atakufa peke yake. Lakini sisi wengine tunasema kwamba hao hao waliomtanguliza, watamfuata.

Hatuwezi kujua mapenzi ya Mungu, na si vema kumsingizia Mungu. Lakini akili timamu inatueleza kuwa kama tungekuwa na serikali makini, kifo cha Ballali kingeahirishwa.

Huyu ndiye alipaswa kulindwa na serikali ili aweze kutoa ushahidi ambao ungeiwezesha serikali kuchukua hatua za kujisafisha, na kudhibiti ufisadi mwingine.

Lakini kwa kuwa si serikali makini, na kwa kuwa haina nia ya kujisafisha; na kwa kuwa inawajua na kuwalinda waliohusika na wizi wa EPA; na kwa kuwa wanaohusishwa na kifo cha Ballali ni wale wale walioshiriki kuiumba serikali hii; Watanzania hawatakuwa na makosa wakiibeza na hata kuituhumu kwa kumuua Ballali.

Ndiyo maana, ingawa kwenye misiba hatutarajii watu wamkejeli marehemu, Watanzania wameshindwa kuzuia hisia zao. Kwa kujitahidi sana, wamezielekeza zaidi kwa serikali badala ya marehemu.

Mojawapo ya kauli zilizozagaa mitaani sasa ni kwamba ‘kafa Ballali, bado wengine kumi.’ Hawa wanaosema hivi wanarejea orodha ya ‘mafisadi’ iliyotajwa na Dk. Slaa, ambayo huko nyuma niliwahi kuiita ‘JK Eleven.’ Lakini kikubwa ni kwamba huyo anayesemekana kumlisha sumu Ballali ni mmojawapo wa hao kumi waliobaki.

Hili linakomaza dhana nyingine kwamba watu hawa sasa wameamua kumalizana wakigombea maisha bora walioyowanyima wananchi.

Tunachojua tulio wengi ni kwamba Ballali si wa kwanza. Na hawezi kuwa wa mwisho. Lakini mwisho wao wote ni mmoja.

Yawezekana bado kumi au zaidi ya kumi. Lakini ukweli ni kwamba Ballali ametangulia, ushahidi wa EPA umekufa, na imani ya watu kwa serikali imekufa!

+447853850425
ansbertn@yahoo.com
www.ngurumo.blogspot.com

source: http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/5/25/makala2.php

Kama RA vile

Hata wewe bado hujamtaja
 
Mimi nasema hivi watu wengine wanastahili hayo wanayoyapata. Balali hakuona umuhimu wa maisha yake ukilinganisha na siri ya kuwaficha hawa majambazi. Kama angelijua thamani ya maisha yake angetutajia majina na mtiriko mzima wa wizi pale BOT. Lakini kwa kuwa aliona ni bora a-sacrifice maisha yake ili kuendelea kuwatunzia siri majambazi wengine.Ndo haya yamemtokea. Sorry!! Ila ndo ukweli

Hivi kama Balali mwenyewe alishindwa kuweka hii ishu wazi tunategemea nini jipya kwa hao mnaosema wameachiwa siri yote. Kama ni ndugu ,Mke au Wakili watakachofanya ni kufaidika tu na hizo nyaraka kwa kuzifanyia blackmail.
 
Labda walimtishia familia yake so he has to sacrifice his life kwa ajili ya wale anaowapenda. Na alijua yeye lazima wamuue tu anyway
 
****Hata KGB walipotaka kumuua yule jamaa wa Ukraine bado ilijulikana, hata Polonium 210 ya UK bado ilijulikana, sasa hii sumu ya gavana wetu ni sumu gani hiyo?**
SUMU ILIOMUUA """KOLIMBA""DODOMA NA ""MTOTO WA MALECELA"" NDIO ILIOMUUA BALALI ...ILA YA KOLIMBA ILIONGEZWA NGUVU ZAIDI
MTANZANIA NATUMAINI UKIFWATILIA UKO UNAWEZA KUTULETEA CONTENTS ZA HIYO SUMU....NA KUWEZA KUJADILIWA....LABDA OMBI LANGU KWA WALE WANACHAMA WA CCM MTAKAOITWA DODOMA HALI MKIJUA ZALI LAWEZA KUWATOKEA NAOMBENI MSIKARIBIE MAUTI MNAYOIONA ""CCM SASA NI WAUAJI HALISI"""" NA WALA SI CHAMA TENA ...LAITI NYERERE ANGAJUA AMEACHA MAFISADI PEKEE ANGEWEZA KUSIKITIKA LAKINI KUMBE AMEACHA CCM YA WAUAJI WATUPU TENA KWA SUMU JAMANI NINGEPENDA KUJUA VYAMA VYENYE MREGO W MAUAJI KAMA CCM ..DUNIAN KOTE TUWENAVYO MAKINI

Mwanahalisi,

Watu hamfanyi mazoezi, mkikumbwa na ugonjwa wa moyo, mnasema mmepewa sumu?

Kolimba alikuwa kwenye pressure kubwa, ingelikuwa huku ULaya, kabla ya kwenda kwenye hicho kikao, angepimwa pressure kwanza na kuhakikisha yu salama kabisa. Lakini kwa TZ ndio kwanza mtu anaweka nyama choma kwanza.

Ye mtoto wa Malecela mimi siyajui vizuri kwahiyo wacha nisitoe comments zangu.

Sijui kwa US, lakini naamini hapa UK, kumlisha sumu mtu ni kosa, hata bila ya yeye kusema, hospitali wanaita polisi. Kama ni kweli alilishwa sumu, hospitali walikaa kimya basi mafisadi
wetu wametoa rushwa mpaka kwa madaktari wa USA, mpaka kwa polisi kwi kwi kwi!!! Haiwezekani.

Mimi swali langu ni lile lile, je alilazwa kwenye hospitali ipi? Huku nje kuna Freedom of Information na inatosha kuliandika vizuri swali, jibu utapewa tu.

Najua ndio maana familia yake hawataki kabisa kutaja hospitali, hawataki wafanye ujinga wa Kitinye.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema wazi kwamba serikali haihusiki na kifo cha Gavana wa zamani wa BoT, Daudi Ballali.... more to come
 
Ansbert Ngurumo

Watu wake wa karibu wamemnukuu hayati Ballali akimtaja mtu aliyemlisha sumu. Yawezekana hii ni kauli mojawapo ambayo wanafamilia walitaka kuiweka hadharani katika mkutano na wanahabari. Tuwape muda.

Kwa sababu zinazoeleweka, hatutamtaja ‘muuaji' huyo hapa kwa sasa. Lakini kadiri siku zinavyokwenda,

hapo ndio ninapo boreka na magazeti ya bongo, kichwa cha habari kinasema huyu, ukishanunua gazeti unabakia na vitendawili! hutamtaja kwa faida ya nani? hamna vyombo vya dola kumshitaki? tuseme hata madaktari wake hawakujua BALLALI amekuwa poisoned? acheni utani! na pesa za wananchi wanaonunua habari kumbe hamna kitu, sana sana speculations!

iwapo na sisi hatutalishwa sumu, kama hatajitaja, tutamtaja siku moja, katika kuweka vema historia ya mapambano dhidi ya ufisadi.

woga huo, woga nao!!!...inakufanya uwe a coward!

Mojawapo ya kauli zilizozagaa mitaani sasa ni kwamba ‘kafa Ballali, bado wengine kumi.' Hawa wanaosema hivi wanarejea orodha ya ‘mafisadi' iliyotajwa na Dk. Slaa, ambayo huko nyuma niliwahi kuiita ‘JK Eleven.' Lakini kikubwa ni kwamba huyo anayesemekana kumlisha sumu Ballali ni mmojawapo wa hao kumi waliobaki.

+447853850425
ansbertn@yahoo.com
www.ngurumo.blogspot.com

source: http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/5/25/makala2.php

hearsays, speculations & more hearsays!!!... jamani kuna facts na fictions,... kama BALLALI alilishwa sumu, au kuuliwa kwa namna yeyote ile kwa nchi kama Marekani hiyo ingekuwa detected, na vyombo vyao vya dola wangeingilia kati, ndio maana wenzetu hao wana issue death certificate baada ya Autopsy/post mortem, huzikwi tu holela holela.

nitaendelea kuamini Daudi Ballali amefariki kutokana na maradhi hayo ya Cancer ya kichwa, lakini kifo chake kitaendelea kubakia simulizi kwa watanzania kwani amefariki na "siri nzito" ya zile pesa.

aaaah, maudhi matupu, sijui leo nimeamka vibaya (?)
 
Mwanahalisi,

Watu hamfanyi mazoezi, mkikumbwa na ugonjwa wa moyo, mnasema mmepewa sumu?

Kolimba alikuwa kwenye pressure kubwa, ingelikuwa huku ULaya, kabla ya kwenda kwenye hicho kikao, angepimwa pressure kwanza na kuhakikisha yu salama kabisa. Lakini kwa TZ ndio kwanza mtu anaweka nyama choma kwanza.

Ye mtoto wa Malecela mimi siyajui vizuri kwahiyo wacha nisitoe comments zangu.

Sijui kwa US, lakini naamini hapa UK, kumlisha sumu mtu ni kosa, hata bila ya yeye kusema, hospitali wanaita polisi. Kama ni kweli alilishwa sumu, hospitali walikaa kimya basi mafisadi
wetu wametoa rushwa mpaka kwa madaktari wa USA, mpaka kwa polisi kwi kwi kwi!!! Haiwezekani.

Mimi swali langu ni lile lile, je alilazwa kwenye hospitali ipi? Huku nje kuna Freedom of Information na inatosha kuliandika vizuri swali, jibu utapewa tu.

Najua ndio maana familia yake hawataki kabisa kutaja hospitali, hawataki wafanye ujinga wa Kitinye.
Hata viongozi wetu wa Nchi wanatujua sisi wananchi wao wa Tanzania kuwa tuna sifa zipi ndiyo maana wanaweza kufanya wayafanyayo wakati wote watakapo;[tangu enzi za kifo cha Sokoine hadi Leo kifo cha Ballali]; sifa katika hizo tulizobalikiwa ni:
===== Kuongea sana na kusahau [ blah blah blah]
==== kubwa zaidi, ingawa tunawajua akina nani ni vinara wa mambo hayo basi sisi huishia kwenye wale weak points;
from the begining, Ballali was just a messenger on implementing his bosses orders; we know his bosses, why attacking ballali who was a mere messenger?
Kikwete and Mkapa are the ones to answer these questions we are throwing to Ballali!
 
No hatuwezi kumtaja kwa kuunganisha hisia za mtu kwani hitaharibu kijiwe chetu, kumbukeni wanatafuta sababu ya msingi kuakikisha hiki kijiwe kinafungwa huu ndo wakati wa kuwa makini zaidi ili tuendelee kumkoma nyani gradi, kama kuna ushaidi wa kutosha tafadhari mtaje kama unaushaidi wa mazingira then please do not do that.

Kwani bado wana uwezo wa kukifunga ,Fundi mitambo embu tuwekee maoni kuhusu hili la uwezo wa kukifunga jiwe hili ,ili kuondoa tisha tisha ambazo WaPemba wameishaziacha mbaali na sasa wanapita na kuimba "....Kura Maoni kikwete kampe mkeo...." Nimeona kideo ya mkutano wao huko Pemba wanasema nakuimba kama hawana akili uzuri.Ila nilipouliza nikaambiwa ndio makali ya siasa hayo lazima ukubali kukumbwa na kila jambo yakiwamo mauti.
Kwako fundi mitambo vipi hili jiwe la Jamii bado jamaa wanauwezo nalo ??

Nikiunganisha hiyo habari ya kitendawili basi Rostamu hatoki ncha zote zilizotajwa anaingia kichwa kichwa ,kama nimekosa basi inabidi sasa patolewe mji ili jamaa amtaje .
 
Mimi swali langu ni lile lile, je alilazwa kwenye hospitali ipi? Huku nje kuna Freedom of Information na inatosha kuliandika vizuri swali, jibu utapewa tu.

Mkuu Mtanzania,

Heshima mbele, hapa umesema neno moja zito sana kuhusiana na this whole thing kuhusu Balali na kifo chake, sina tatizo na msimamo wako on the ishu ya kufa kwake, lakini at the same token ninajaribu ku-reason out,

Kwamba Balali, hajafa, familia yake imeamua ku-play a stint na kuwaaarifu dunia nzima kuwa amekufa, watu wa karibu na familia hiyo, ndugu wa karibu wote wa Balali na Muganda, wamekwenda huko DC, mmiliki wa Tanzania Daima ambaye naye ni ndugu wa karibu amefahamishwa kuhusu hicho kifo, serikali imefahamishwa kuhusu hicho kifo, dada yangu amefahamishwa na kualikwa kwenye msiba, juzi yamefanyika mazishi,

Sasa kama ninakuelewa vizuri, ni kwamba huu wote ni uongo uliotungwa na familia hiyo ya Balali, lakini Balali yupo na ataendelea kuishi baada ya all this?

kweli unaamini kuwa this makes a sense?
 
Back
Top Bottom