Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Basi tuseme Balali amepotezwa na hii ndiyo iwe slogan hapa JF

nakuunga mkono ndugu kuwa kwa hapa kwetu iwe ni kuwa balali kapotezwa na sio kafa...
cku zote toka day 1 ya hii movie ya balali kufa nimekuwa naipinga na sijui ka wengi walikua wakipenda swala hilo,na bado mpaka kesho napinga tuu huu usaniii there r somethingz vinatatiza mnoooo in de whole kufa,matanga,kuzikwa etc n etc
 
Taratibu naanza kukubali kuwa MAFISADI wameisha tuingilia mpaka majumbani mwetu, kama kweli watu wazima wamekaa wakafikia kupanga mtu mzima afe. Hiyo mimi inanichanganya sana.

Lakini ukiangalia tukio zima la kutangaza kifo cha Balali utagundua hakukua na kifo hila tu ni mipango.

Katika utanzania wetu hivi ni nani anayeweza kufiwa na mtu wa karibu akaomba ruhusa kutangaza msiba?

Hivi inakuwaje wakati wa msiba mama mtu analindwa na hakuna anayeruhusiwa kuingia?

Hivi inakuaje tunaambiwa huko iringa hata wakuna cha msiba wala nini?

Hivi inakuwaje tunatafuta wiki nzima hata ka-picha ka kutuonyesha msiba hakuna kabisa na watu walikuwa marekani ambapo technojia si haba?

Hivi hata ndugu zake balali, jamaa zake walikuwa wamemchoka kiasi kwamba hawaewezi kumzika au kupata kumbukumbu?

Nafikiri inabidi nifikirie kuwa UFISADI uliofanyika BoT si wakawaida, inawezekana walilamba kila kitu au na makampuni walionayo baadhi ya watu inawezekana ni yetu wote.

Jamani tangu lini watu wakubwa wakadanganywa kama watoto?
 
Freeman Mbowe una undugu na Nyerere jamani, mbona wanaranda wajihi wao, najua watu wengi wanarandana hapa duniani, just curious to know about Freeman and JK nyerere
 
si alifukuzwa ajira yake ya udalali pale BOT, au nalo lilikuwa changa la macho. Maana siku hizi hakuna kuingia ndani au kukaa nje unaweza umbuka hivi hiiivi, ilobaki ni kukaa mguu mmoja ndani mwingine nje.


Walivyotuambia ni kwamba uteuzi wake wa kuwa Gavana ulitenguliwa- hii ni tofauti kabisa na kufukuzwa kazi serikalini. Ni jambo la kawaida kwa maafisa wa serikali kunyang'anywa vyeo na kupangiwa kazi zingine.
 
Walivyotuambia ni kwamba uteuzi wake wa kuwa Gavana ulitenguliwa- hii ni tofauti kabisa na kufukuzwa kazi serikalini. Ni jambo la kawaida kwa maafisa wa serikali kunyang'anywa vyeo na kupangiwa kazi zingine.

so how come they announced that they didnt know his whereabouts? something smelling like a rotten fish... mhhhhhhh......
 
Kwenye thread moja niliuliza.... msimamo wa Anna Muganada kwenye hili swala zima uko wapi(Tangu tuhuma zimeanza mpaka kufukuzwa kazi kwa Ballali?

Needless to say, Anna Muganda na Ballali lao moja. Ballali aliamua kukaa kimya "hospitali," na Anna Muganda nae mpango wake ni kuendeleza uzi ule ule.
 
Mwafrica Wa Kike Juzi Hapa Nilisema Anna Muganda Sasa Hivi Ataolewa Tena Na David Balali,ukasema Ndoa Itafanyika Acapulco Ndiyo Hayo,ukisikia Don Apson Mwangonda Ndiyo Kazi Zake Hizo Yeye Alkuwa Thinking Tank Wakati Wa Marehemu Mkapa Sorry Mweshimiwa.
 
Daudi Ballali hakuwa mtumishi wa serikali (kwa maana ya muajiriwa). Alikuwa ni mtumishi wa IMF/WB?. Kitu ambacho ni cha kuangalia sana ni kuwa kabla ya kuwa Gavana alikuwa Mshauri wa Rais wa Mambo ya Uchumi (mshauri wa Mkapa). Na ndipo kutoka huko akapewa Ugavana on secondment.

Sasa washauri wa Rais sidhani kama ni watumishi wa umma bali wanalipwa toka Ikulu na wanatumika at the "pleasure of the President".
 
Daudi Ballali hakuwa mtumishi wa serikali (kwa maana ya muajiriwa). Alikuwa ni mtumishi wa IMF/WB?. Kitu ambacho ni cha kuangalia sana ni kuwa kabla ya kuwa Gavana alikuwa Mshauri wa Rais wa Mambo ya Uchumi (mshauri wa Mkapa). Na ndipo kutoka huko akapewa Ugavana on secondment.

Sasa washauri wa Rais sidhani kama ni watumishi wa umma bali wanalipwa toka Ikulu na wanatumika at the "pleasure of the President".

Sasa Mkuu
Ukiwa secondment, kama balali alivyokuwa ukiachishwa kazi huko unarudi moja kwa moja ulikotokea. Mbona inaonekana bado Balali aliendelea kuwa chini ya BoT, pamoja na kuachishwa kazi huko?

Nafikiri hapa pia ndio maana kukawa na mkanganyo nani atangaze kifo chake.
 
Anayeamini kuwa BALALI kafa anyooshe mkono juu...........!
 
BoT yajivua lawama ukomo ajira ya Ballali (Majira)

Na Reuben Kagaruki

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imejisafisha na kusema kuwa haijui ni lini aliyekuwa Gavana wa BoT, Dkt. Daud Ballali, aliandikiwa barua ya kufutwa kazi na kuipokea kwa sababu haihusiki na jambo hilo.

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Ikulu kusema kuwa wenye taarifa za lini Dkt. Ballali aliandikiwa barua ya kufutwa kazi na aliipokea lini ni BoT.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndullu, alisema nafasi ya ugavana ni ya kuteuliwa na Rais, hivyo na uamuzi wa kufutwa kazi unatoka huko huko kwake.

"Hii ni nafasi ya kuteuliwa, unajua vyeo vya kuteuliwa unaitwa tu na kuambiwa," alisema Profesa Ndullu na kusisitiza kuwa katika nafasi ya Ugavana Ikulu ndio mwajiri na sio BoT.

Kauli hiyo ya Profesa Ndullu inaonekana kuwachanganya wananchi hasa kutokana na kauli iliyotolewa na Ikulu juzi kuwa BoT ndio wanaojua Dkt. Ballali aliandikiwa lini barua ya kufutwa kazi na aliipokea lini.

Juzi akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari Dar es Salaam lililomtaka aeleze ni lini Dkt. Ballali aliandikiwa barua ya kufutwa kazi na aliipokea lini, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Bw. Salva Rweyemamu,alisema wenye jibu hilo ni BoT, lakini katika hali ya kushangaza Benki hiyo nayo imeruka kiunzi hicho ikisema hilo ni suala la Ikulu.

Utata huo unazidi kuibuka huku wananchi wakisema kuwa Dkt. Ballali hajawahi kufukuzwa kazi na kifo chake kimetokea akiwa bado mtumishi wa serikali hivyo iliwajibika kusimamia mazishi yake.

Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Bw. Augustino Mrema, alikaririwa na gazeti hili hili akisema Dkt. Ballali hajawahi kufukuzwa kazi. Alisema kama aliwahi kufukuzwa kazi basi ioneshe kitabu alichosaini kudhibitisha kupokea barua ya kufukuzwa kazi na Rais ili Watanzania wajiridhishe.

Kama hiyo haitoshi, baada ya kutangaza kumfuta kazi gavana huyo wa zamani, serikali haikujishughulisha kumtafuta na mara zote imekuwa ikisema kwamba haina haja ya kujua hospitali aliyolazwa kwa kuwa ilikuwa bado haijamhitaji.

Profesa Ndullu alipoulizwa leo kama Dkt. Ballali aliweza kukabidhi ofisi wakati anaondoka kwenda kutibiwa, alisema wakati anaenda kutibiwa kuna watu waliokuwa chini yake walioachiwa majukumu.

"Taasisi nyeti kama hii inaendeshwa kwa kumbukumbu, kuna Bodi ya Uendeshaji na kiongozi mmoja peke yake hawezi kuwa mwendeshaji," alisisitiza Profesa Ndullu.

Profesa Ndullu alisema alipoteuliwa kushika nafasi hiyo Septemba mwaka jana na kuanzia kipindi hicho alikuwa na mawasiliano naye mara kwa mara na alikuwa akimpa maelekezo hata pale afya yake ilipozidi kudorora.

My Take:
What on earth is this, King Majuto drama? Yaani muda wote serikali inasema haijui aliko kumbe Ndullu alikuwa na mawasiliano naye ya "mara kwa mara"?
 
Hivi si kuna kipindi waziri wa fedha alikaririwa akisema Balali hayuko Marekani tena? Tena siku hizi za karibuni? Mbona Gavana alikuwa anawasiliana naye mpaka afya ilipokuwa inaanza kudorora?
 
jamani mnatutisha! kuna gazeti moja la udaku nadhani ni risasi au sani sina uhakika niliiona mtaani leo, mbele kabisa kuna picha inayoonyesha jeneza lenye mwili wa bilali ukiwa altareni kwenye kanisa kuu la st stephen the matyrs, washington dc. tena wakasema mazishi yeke yalitumia masaa sita, mpaka watu wakachoka kufuatilia ibada.

sasa mwafrika wa kike tueleze kama nalo hili ni bonge la move.

siwezi kukataa kwa hili la mwafrika mwanamke, kwa kuwa mafisadi wa tz wanaishi mwezini, wakati sisi tunaishi hapa ardhini. mtu kuwa na 50bilioni kwenye akaunti yake, anaweza kutengeneza move moja nzuri kuliko zile za hollywood.

mh, mbesaaa


Mazishi yalikuwa ya faragha na picha za mgando na Video hazikuruhusiwa na hata picha via phone's hawa wa gazeti wao waliipata wapi ?
 
Lunyungu: Kulikuwa na wapiga picha wawili ndani mle... na wote walikuwa ni ndugu wa Ballali.. mmoja ni binti ya kike. Mmoja wao alipiga picha za ndani na makaburini na huyo mwingine alipiga picha za nje tu...
 
Kweli Sinema inaendelea kunoga, unafiwa na ndugu yako, unapata nguvu za kuwa mpinga picha?
 
Hapana,
Wapiga picha hawakuwa ndugu wa Balali. Mmoja ni small time thug anaitwa Loo Mhagama na mwenzake. Hawa walijibanza upande mwingine wa barabara wakati
gari ya mazishi ilipokuwa inaondoka.
 
Hapana,
Wapiga picha hawakuwa ndugu wa Balali. Mmoja ni small time thug anaitwa Loo Mhagama na mwenzake. Hawa walijibanza upande mwingine wa barabara wakati
gari ya mazishi ilipokuwa inaondoka.

Mkuu unaweza kujibu duku duku zinazojitokeza hapa? Inaonekana unajua kidogo. Inakuwaje msiba unakuwa siri kubwa?
 
Mkuu unaweza kujibu duku duku zinazojitokeza hapa? Inaonekana unajua kidogo. Inakuwaje msiba unakuwa siri kubwa?

Kakindomaster,
Mkuu siwezi kutoa majibu yatakayotosheleza. Uache mjadala uchukue mkondo wake wenyewe. Lakini swali mnalopaswa kujiuliza ni faida gani ambayo familia ingepata kwa kupitia zoezi zima la kudanganya kifo? Kwetu sisi msiba haukuwa siri. Tumemwuuguza mgonjwa kwa miezi tisa. Ups and downs zote za matumaini na kukata tamaa tumezipitia. Simu za ajabu ajabu tumepigiwa. Sasa mlitaka tuandike kwenye Washington Post kuwa ndugu yetu kafa?
 
Sasa mnamtisha Muungwana maana nakumbuka alikurupuka akamfukuza mtu kazi mara akajutia ushauri ,sasa hili la kifo ni nani aliempa habari na jamaa kutangaza kwa huzuni ,huu naona utakuwa mwisho wa machozi ya mamba.
Yaani hapa si ajabu serikali ikasema ilikuwa haijui alipo na walipopewa habari walizipokea kama zilivyo na kuutangazia umma, sijui niamini kama duniani hakuna siri ,ila hii kama ni siri haikutimia miaka 20,wanasema siri hujulikana baada ya miaka 20 ,Muungwana wambie jama sasa warudishe feza zetu ,la si hivyo wataishia jela yaani wakamatwe usiku kama wahaini wa Pemba.
Wapemba wameilaani CCM sasa kila kitu chao kinatoka nnje na kila wanavyojaribu kuficha ndivyo inavyozidi hatari kwa hawa mafisadi,Kikwete bwaga manyanga.
 
Back
Top Bottom