Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania


The dataz ni kwamba pamoja na sehemu zote ambazo marehemu aliacha documents zinazowahusu, kuna ambazo ziko mikononi mwa wajumbe wa Congress ya USA, sasa the dataz ni kwamba wao wanasubiri itakapofikia Tanzania kupewa zile hela za Bush na ule mkopo maalum wa mamillioni ya dola ambao uliahidiwa kwa Mkulo majuzi, ndio mtakiona cha moto, wale wote mliohusika in one way or another,

Siwatishiii nyau, ila ninaamini mnazo akili za kutosha kujua the seriousness ya hizi dataz, maana hamuwezi kufanya uhuni wenu mpaka US, kama mlifikiri kuwa mna akili sana kama za kumwagia waandishi tindikali sasa subirini the fallout

Baharia, baharia, mwanangu acha kutupeleka. LOL! Congress washakamata ishu...nini?

E bwana wazalendo wataogopa, acha hizo baharia! Ha ha haaaaaaaaaa!

Yani sina mbavu.
 
Imani yangu imeongezeka maradufu...mpaka sasa bado:

1. Naamini Balali hajafa.

2. Naamini alikuwa raia wa USA.

3. Naamini siku moja tutakuja kujua ukweli...

Kama unaamini Balali hajafa, je unaamini kuwa Nyani Ngabu kafa?
 
Baharia, baharia, mwanangu acha kutupeleka. LOL! Congress washakamata ishu...nini? E bwana wazalendo wataogopa, acha hizo baharia! Ha ha haaaaaaaaaa! Yani sina mbavu.

Documents zipo kila kona mkuu, na tunajua jinsi zinavyotafutwa toka last week mkuu na wanaozitafuta, mimi ninazo mbavu mkuu ndio maana ninamwaga vitu mkuu kwa sababu ninajua kuwa wabunge wetu wengi tu wamekuwa wakiitwa Congress, all the times ni last two weeks tu wa mwisho alikuwa huko!

Sasa kwa wale viongozi wetu waliofikiri akifa basi wamepona, ninawaonea huruma sana bro! Hakuna anyekupelekea kokote ila ni wewe tu ndiye unayejipeleka kutokuwa na mbavu!

Ni Mtanzania asiyekuwa na akili tu ndiye anyeweza kuamini kuwa kuondolewa kwa Lowassa, hakuhusiani na ziara ya Bush, sasa unafikiri kabla ya hela zake kuja itakuwaje? Atakuja mtu wake kwanza mkuu!

Huu ujumbe kuna unaowahusu mkuu, leo sidhani kama kutalalika huko! Na very soon tutazipata na kuziweka hapa hyizo documents si unajua hapa JF kulivy0o na vichwa nina hakika kuna watu wanazo tayarii hapa, subiri kidogo tu mkuu zinakuja hizoooooooo!
 
1
. Need I say the least that logic is the base of reasoning and unless you're illogic you'll never use incredible sources to testify Ballali's death? Sources Sources Sources; you came here testifying Ballali died in DC, does your sources more credible than JKs' who said Ballali died in Boston when sending condolences to Ballali's family? Do you want me to give benefit of doubts!

Mkuu some of us tunsimama kuhesabuwa ila huwa hatukai nyuma nyuma yua wengine kusubiri wasme tu halafu tutafute sababu, hapana na hata siku moja sitashika hiyo nafasi yako ya kukaa pembeni kama fisi kusubiri mifupa, je wewe unasema alifia wapi, mimi nimesema DC, Jk amesema Boston, je wewe unasema wapi? Unafikiri ninahitaji your anything kuweka my opinion? kila unapofungua mdomo ni more nonesense as if kuna anye-care!

2.
the way, since I register (Aug. 2007) I've never change my membership nor register another name, only JS.

Samahani mkuu sijawahi kukuona mahali popote pale ukisema anything, mpaka pale tu nikisema mimi na wala sijali ila tatizo ni kwamba unaishusha hadhi ya JF majina yamekuwa mengi mno, punguza mkuu sio siri!

3.
problem is you think all members will accept what you say and whenever one disagree you jump to a conclusion that is the one disagree previous. My brother/sister, no one is after your credibility and no one even know who you are! We are all trying to contribute despite of whether will converge to same point on not. If we do not converge then someone has to admit instead of calling other opinions NONSENSE!

Unajua unapoharibu ni pale tu unapolilia personal badala ya hoja, na ndipo mwenyewe unaponiambia kuwa wewe ni nani, wasionijua huwa hawana muda wa maneno kama yako mkuu, huwa wana hoja, halafu hii ya kukubali ninayosema mbona utaishia kupoata ugonjwa wa moyo mkuu, maana toka uanze umegundua kuwa sijaacha kuandika kama ulivyotegmea, sasa sijui utafanyaje mkuu, ila nikuhakikishie kuwa mimi ni mtu mzima nionapokuja hapa nitafuta elimu kwa wenye nayo sasa ni clear kuwa wewe huna hiyo elimu zaidi tu personal attacks ambazo nazo pia unajichanganya tu, punguzamajina mkuu unaiharibu forum hii!
 
Quote:
Originally Posted by Yebo Yebo
Imani yangu imeongezeka maradufu...mpaka sasa bado:

1. Naamini Balali hajafa.

2. Naamini alikuwa raia wa USA.

3. Naamini siku moja tutakuja kujua ukweli...


Mkuu Yebo Yebo,

Heshima mbele mkuu, siku zote huwa ninakauminia, hii ndio tunaita kusimama uhesabiwe, badala ya kufuata upepo wa wengine na kujaribu bila mafanikio kuwa-fault wengine, wakati wewe huna msimamo,

wa kwako mkuu ni mfano wa kuigwa, Salute!

Sasa hivi tunajaribu kuwashinikiza waandishi wetu wampate Butiku ili atemne cheche, nafikiri siku hiyo mvua ya mawe itaanguka!
 
Mimi pia kutokana na kauli tofauti zilizotolewa kuhusiana na kifo cha Ballali namini huyu jamaa hajafa. umeambia Anna Muganda, mke wa Ballali ndiye aliyewajulisha Ikulu na BoT kuhusiana na kifo cha Ballali. Je, ilikuwaje kukawa na kauli zenye tofauti kubwa kati ya Ikulu na familia ya Ballali? Na ni sababu zipi zilizoifanya Ikulu na BoT kunyamaza tangu walipotaarifiwa kifo hicho hadi kulipoandikwa katika gazeti la Tanzania Daima. Na hao walioalikwa toka ofisi ya ubalozi akiwemo balozi mwenyewe mbona hawataki kuongea chochote kuhusiana na kuhudhuria mazishi hayo? Na ni kwanini Watanzania hatujaambiwa ni ugonjwa gani uliomuua Ballali? Tumeambiwa kwamba ni kazi ya Mungu, lakini hatukuambiwa ni kipi hasa kilichokuwa kinamsumbua Ballali hadi kifo chake.

Ikulu: Ballali kafia hospitali Boston
Familia: Ballali kafia nyumbani washington

Bado kuna utata mkubwa kuhusu kifo cha Ballali wengi wa Watanzania tutaendelea kuamini kwamba kuna mchezo umechezwa na wachezaji wa mchezo huo hawakuwa makini katika kupanga habari ya kifo cha Ballali, sasa wanaumbuka na hakuna aliyejitokeza toka Ikulu, BoT au familia kuinyoosha habari hii ili wengi tuiamini.
 
Naomba nimpongeze JMUSHI kwa msimamo wake. Zilipotoka tu hizi fununu za kufa kwa Ballali, JMUSHI alisisitiza tena na tena :"Habeas corpus" show me the body!

Kama wangeruhusiwa Watanzania waliotaka kwenda kuomboleza kufanya hivyo, na wakapita wakiutazama na kuuaga mwili wa marehemu kama ilivyo desturi, hakungekuweko na maneno.
 
Nilikuwa na maana hospital alikokuwa amelazwa, kisha tukaambiwa karudi nyumbani hali yake iliendelea vizuri na baadaye atarudi TZ kutoa ushahidi.. yote haya hamkuyawekea mashaka isipokuwa leo mliposikia amekufa!..
Yaani mnadai kujua zaidi kuhusu maiti kuliko alipokuwa hai as if kutabalisha kitu.. sasa kama hii sio NDIVYO TULIVYO nini hasa!

Mkandara,

Bado hujanijibu swali langu rahisi sana, umesema unajua alikokuwa amelazwa Dr. Ballali kabla ya kupata nafuu, je alilazwa hospitali ipi?

Ukijibu hilo ni mwanzo mzuri.
 
Mushi hii ni quote ya Mkulu MMJ, ni kipi usichoelewa hapa mkuu? Ujumbe wangu kwa viongozi wa Tanzania mnaohusika na hiki kifo na kufikiri kuwa sasa mmepona, labda tuwamegee tu kuhusu dataz kidogo, kutoka kwa dataz nzito tulizonazo,

The dataz ni kwamba pamoja na sehemu zote ambazo marehemu aliacha documents zinazowahusu, kuna ambazo ziko mikononi mwa wajumbe wa Congress ya USA, sasa the dataz ni kwamba wao wanasubiri itakapofikia Tanzania kupewa zile hela za Bush na ule mkopo maalum wa mamillioni ya dola ambao uliahidiwa kwa Mkulo majuzi, ndio mtakiona cha moto, wale wote mliohusika in one way or another,

Siwatishiii nyau, ila ninaamini mnazo akili za kutosha kujua the seriousness ya hizi dataz, maana hamuwezi kufanya uhuni wenu mpaka US, kama mlifikiri kuwa mna akili sana kama za kumwagia waandishi tindikali sasa subirini the fallout,

ndugu yangu Muuungwana sikia hiyo mwanangu kutoka kwangu FMES!

Mkuu FMES,

Hizi habari tumeanbiwa toka mwaka jana mwezi wa tisa, kwamba eti Ballali ana documents kibao na anasubiri tu apone ili azimwage. Jasusi anatuambia hapa kwamba Ballali alipata nafuu,
lakini bado hakuwaumbua mafisadi wenzake, kwanini?

Amefariki tarehe 16, wiki mbili zimepita, hizo documents ziko wapi? nafikiri ni yale yale ya kuvuta muda wakiamini Watanzania watasahau, bahati mbaya hatutasahau.

Naamini Ballali anajua mengi kuhusu wizi wa pesa zetu na ndio maana kwa kushirikiana na serikali wameamua kufake kifo chake ili kujiokoa yeye mwenyewe na kuwaokoa hao mafisadi mpaka juu kwa JK mwenyewe. Hiyo ndio motive ya hili suala zima. Hakutaka kwenda Keko, na hao wenzake kuumbuliwa maana miezi sita tuliyoambiwa tusubiri kuhusu Ballali na wezi wa EPA inakaribia.

Wanafikiri huku nje ni kama kule Bagamoyo ambako mtu anaweza kujifia na kuzikwa bila ya records zake kuachwa popote. Ndio maana ikaja hiyo ya kwamba kafia nyumbani. Walichosahau ni kwamba sasa kuna Watanzania wengi wametapakaa dunia nzima na wanajua taratibu za kila nchi husika.

Unataka watu na akili zetu tuamini Ballali kafa wakati kitu pekee kisicho na utata ni jeneza lililokuwa limelala kanisani? Kuna siri gani kwenye kueleza mgonjwa kafia hospitali gani?

Haiwezekani kwa binadamu wa kawaida, eti kakako afariki, umfiche kifo mamako, eti unasubiri Ikulu watangaze, tena Ikulu hao hao unaofikiri wamemwua? Instinct ya mwanadamu kwenye kifo haiko hivyo.

Taratibu watu wengi wanaanza kuamini kwamba Ballali hajafa.
 
Balali kafa hajafa kafa hajafa kafa hajafa.......then what???
 
Mkuu Yebo Yebo,
Unaamini kuwa Balali hajafa, kwa nini katika point yako namba mbili unatumia past tense (balali ALIKUWA raia wa Marekani). Ina maana sasa si raia wa Marekani, kimetpkea nini hadi uraia wake umekoma?
 
Nyani.. what you did today is unforgivable...

Na pia wote walioshiriki!

Kama watu wanaingia kichwa kichwa kujadili kitu cha kidaku daku "Nyani Kafa..." kama vile ni kitu muhimu, basi watu nao ni irresponsible pamoja na Nyani wao.

Nadhani Nyani alichagua kichwa cha thread kibaya, kuhusisha taarifa za kifo kimzaha mzaha kwenye front page la JF, lakini ujumbe wake umefika vizuri: kwamba chochote utakacho anzisha hapa JF watu watashiriki tu, haijalishi ni cha kipuuzi vipi.

Mjadala wa kifo cha Ballali, ambao Nyani alisema hauna maana - na ndio ujumbe wa "Nyani Kafa...," - una vipimo vya kitaifa, na nadhani sio vibaya wanao taka kuuendeleza waundeleze, na Nyani anaweza kuchagua kuacha kushiriki kama na wengine tunavyoweza kuchagua kuendelea kushiriki.

Lakini watu wakijiingiza kwenye mjadala wa "Nyani Kafa..." wakati unaona aliye uanzisha ni 'marehemu' Nyani mwenyewe, basi wa kulaumiwa ni wao pamoja na Nyani wao!
 
Wenye akili tambueni mambo haya,

Mkiona viongozi wetu wameanza kujisariti wao wenyewe, huku wakisingiziana wao kwa wao mjue Dola hiyo iko mashakani,

Mkiona mkuu wa nchi ametulia kimya!!!!! Mjue inchi iko karibu kutakasika.

Mkiona vibaraka wengi wanaotetea mafisadi wamesimama patakatifu pa patakatifu, mjue mlungula wamepokea na kama si hivyo basi wanaigopa Dola.

Uoga, Hofu ni chanzo cha umaskini.

Tabiri sasa tunakwenda wapi. mbele kiza tololo...............................,

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika..........
 
1.
Naamini Ballali anajua mengi kuhusu wizi wa pesa zetu na ndio maana kwa kushirikiana na serikali wameamua kufake kifo chake ili kujiokoa yeye mwenyewe na kuwaokoa hao mafisadi mpaka juu kwa JK mwenyewe. Hiyo ndio motive ya hili suala zima. Hakutaka kwenda Keko, na hao wenzake kuumbuliwa maana miezi sita tuliyoambiwa tusubiri kuhusu Ballali na wezi wa EPA inakaribia.

Mkuu Heshima mbele,

Again respect kwa msimamo mzito sana ndio hasa maana ya JF yaani demokrasia juu, wabunge wengi ukiongea nao kwa pembeni, wanasema kuwa kuondoka kwa Balali kwenda huko US hakukubadilisha anything kwa sababu wao wanajua kuwa kila kitu kipo bongo as far as ushahidi kuhusiana na EPA, na wanajua sana kila aliyehusika, wanasema kuwa next bajeti ndio wataanza na EPA kwa hiyo mimi sidhani kama kama serikali imehusika na "kumuuuua" basi imetatua anything na kuna ambayo siwezi kuyaweka hapa oin this nimekutumia kwenye PM nafikrii wakati wake kuwa hapa bado. Lakini ninaamini kwa dhati sana kuwa kuna some serious co-ordinated efforts kujaribu kuzipata hizo documents on the European na US side!

2.
Unataka watu na akili zetu tuamini Ballali kafa

Mkuu hii point nilifikiri kuwa tuliushakubaliana kutokubaliana, wewe unaamini hajafa, mimi ninaamini 100% kuwa amekufa.

3.
wakati kitu pekee kisicho na utata ni jeneza lililokuwa limelala kanisani? Kuna siri gani kwenye kueleza mgonjwa kafia hospitali gani?[/
B]

Balozi Sefue aliuona mwili ndani ya jeneza, wazungu toka World Bank na IMF waliuona ule mwili ndani ya jeneza, watoto wa marehemu waliuona mwili kwenye jeneza, kama hii nayo ni point ya muhimu if you will,

sasa kama wale ambao hawakuwepo wanajua kuwa ule mwili haukuwa wa Balali, kwa kweli hapo sina argument against maana inaonekana kuna watu ambao hawakuwepo huko wanaojua mengi sana ambayo wengine hatujui,

lakini Balozi Sefue ninamuaminia sana tena sana, sio mtu wa wasi wasi wala mbabaishaji kama wengine, sasa for him kumdanganya bosi wake Membe na rais wa Jamhuri, au kwamba wote wana njama moja, kwamba Kikwete naye anahusika na a deal ya 'kumuua" Balali, lakini akamuacha Lowassa ajiuzulu ambaye najua anajua mengi kuliko Balali, nafikiri ni kitendawili kikubwa sana ndugu yangu Mtanzania unakijua.

Otherwise una strong arguments, keep it up mkuu tule education hapa!
 
1.

Mkuu Heshima mbele,

Again respect kwa msimamo mzito sana ndio hasa maana ya JF yaani demokrasia juu, wabunge wengi ukiongea nao kwa pembeni, wanasema kuwa kuondoka kwa Balali kwenda huko US hakukubadilisha anything kwa sababu wao wanajua kuwa kila kitu kipo bongo as far as ushahidi kuhusiana na EPA, na wanajua sana kila aliyehusika, wanasema kuwa next bajeti ndio wataanza na EPA kwa hiyo mimi sidhani kama kama serikali imehusika na "kumuuuua" basi imetatua anything na kuna ambayo siwezi kuyaweka hapa oin this nimekutumia kwenye PM nafikrii wakati wake kuwa hapa bado. Lakini ninaamini kwa dhati sana kuwa kuna some serious co-ordinated efforts kujaribu kuzipata hizo documents on the European na US side!

2.

Mkuu hii point nilifikiri kuwa tuliushakubaliana kutokubaliana, wewe unaamini hajafa, mimi ninaamini 100% kuwa amekufa.

3. B]

Balozi Sefue aliuona mwili ndani ya jeneza, wazungu toka World Bank na IMF waliuona ule mwili ndani ya jeneza, watoto wa marehemu waliuona mwili kwenye jeneza, kama hii nayo ni point ya muhimu if you will,

sasa kama wale ambao hawakuwepo wanajua kuwa ule mwili haukuwa wa Balali, kwa kweli hapo sina argument against maana inaonekana kuna watu ambao hawakuwepo huko wanaojua mengi sana ambayo wengine hatujui,

lakini Balozi Sefue ninamuaminia sana tena sana, sio mtu wa wasi wasi wala mbabaishaji kama wengine, sasa for him kumdanganya bosi wake Membe na rais wa Jamhuri, au kwamba wote wana njama moja, kwamba Kikwete naye anahusika na a deal ya 'kumuua" Balali, lakini akamuacha Lowassa ajiuzulu ambaye najua anajua mengi kuliko Balali, nafikiri ni kitendawili kikubwa sana ndugu yangu Mtanzania unakijua.

Otherwise una strong arguments, keep it up mkuu tule education hapa!

FMES,

Unasema balozi Sefue aliuona mwili, kweli una uhakika na hiyo statement? Kuna watu walihudhuria hayo mazishi na wanasema hakuna aliyeuona mwili hapo. Hata statements mbalimbali zilizotolewa zilisema hakutakuwa na kuuona/kuuaga mwili zaidi ya kuliaaga jeneza ambalo lilikuwa limefunikwa.

Tuhakikishie hapa kama kweli Sefue aliona jeneza lililofunguliwa lenye mwili wa Ballali. Hivyo hivyo hata hao wakuu wa IMF hawakuuona mwili wa Ballali.

Angalia source yako ya data, wasije wakawa wanakupotosha ili utoe taarifa ambazo sio sahihi hapa JF, hiyo itakuwa mbaya sana. Hata Jasusi hakuna hata sehemu moja aliposema watu waliona mwili wa marehemu kule kanisani. Sisi hapa tunataka ukweli wa hili jambo na sio kwamba tuko hapa kubisha tu. Kuonwa kwa mwili pale kanisani ingelikuwa njia moja wapo ya kuelekea kwenye ukweli. Hivyo ni muhimu mno statement kubwa kama hiyo iwe ina usahihi vinginevyo iondoe.

Kuhusu umuhimu wa Ballali, mkuu nafikiri unajua maana ya kumfunga paka kengere, kama wahusika wa EPA ni JK, Mkapa, Apson, unafikiri hao wabunge watasema nini? Ushahidi wa Ballali ungelikuwa kumfunga paka kengere, makelele ya hiyo kengere yangewaamsha hata panya walio lala. Sasa amekwenda basi mkazo utawekwa kwenye hilo deal lililochnguzwa tu na kuficha kuhusika kwa viongozi wa juu wa CCM.

Kuwepo kwa Ballali na ushahidi wake ingelikuwa muhimu mno, si umeona tu mama Meghji kamtupia mzigo wote Ballali, sasa Ballali amekufa, je tutajua kuhusika hasa kwa mama Meghji?

Hilo la documents mimi silipi nguvu na hata kama zipo basi zitakuwa za kulipa kisasi zaidi kuliko ukweli. Zitakuwa documents ambazo ziko edited na zinazojaribu kumwondoa yeye kwenye madhambi na kutupia wengine. Documents ambazo mhusika hawezi kuulizwa hapa mbona pako hivi? Documents ambazo aliogopa kuzitoa kwa miezi tisa, sasa kapotea ndio eti anawaachia wengine wazitoe?
 
Iam just speechless! I can see our government has a long way to fight its own citizens.
 
FMES: Umeongea mambo mengi sana, nitajaribu ku-address machache kati ya hayo.

i) Mkuu, hii issue ni nzito sana. Wewe umewahi kuona wapi watanzania wanabisha kifo kilichotokea? Watanzania huwa wanaweza wakatofautiana sababu za kifo na mahala pa mtu kuzikwa, lakini sio mtu kufa. Sasa ukiona watu hapa JF tumetofautiana kwa kiasi hiki, ujue kuna kitu hapa.

ii)Huwezi kukataa kwamba wewe ni miongoni mwa watu waliosababisha confusion na shaka kuhusu kufa kwa Balali. Mimi binafsi hii ilikuwa ni mara ya kwanza kuona umeleta dataz mbili tofauti ndani ya kipindi kifupi kabisa: moja ikikanusha habari za Invisible kuhusu kufa kwa Balali na ingine ikihibitisha kwamba Balali kafa! Hatujamzoea FMES wa namna hii. FMES tunayemjua hapa JF ni yule ambaye huzifanyia kazi dataz zake kwanza kabla ya kuzimiwaga na akishakuzimwaga huwa zinabaki hivyo na huthibitika hivyo. Sasa mkuu ulitaka kweli watu tusi-question incosistency ya posts zako mbili?

iii) Kuna kamsemo kanasema hivi kwa kiingereza: if you are a watcher you should be prepared to be watched! Sasa wakuu nyie mnaotusaidia kuchunguza habari nzito kama hizi, muwe tayari pia kuchunguzwa. Msitarajie kwamba mtaleta habari hapa sisi tuzipokee kama zilivyo, no, tutachunguza authenticity na intentio yake. So far, kwenye hii issue habari zenu mlizotuletea zinaleta maswali mengi zaidi kuliko majibu. Sasa tukisema hivi msituelewa vibaya, there is nothing personal here. Isitoshe, nafikiri mimi unanielewa vizuri tangu bcs. Huwa ukishusha issue nikaikubali huwa naikubali na kukusifia sana tu na wewe umeshakiri hivyo hapa sio mara moja wala mara mbili. Sasa kwa nini ufikiri kwamba nimekushambulia au kukuharibia jina pale ninapo-question habari mbili tofauti ulizotuletea katika kipindi kifupi kabisa?

iv) Binafsi sijasema kwamba nimethibitisha kwamba Balali kafa. Siwezi kusema hivi kwa sababu mimi kwa kweli sina access yeyote kuhusu habari za Balali zaidi ya kusoma kwenye magazeti na hapa JF. Ninachosema ni kwamba matukio ya kuugua na kufa kwa Balali yanaleta shaka na wale wanaotilia shaka kuhusu kifo cha Balali wamenishawishi zaidi kuliko wale wanaosema amekufa. Katika umri wangu huu, nimeshashuhudia ugonjwa na vifo vingi kabisa. Sijawahi kuona hospitali anayougulia mtu iwe siri. Kikubwa zaidi sijawahi kuona msiba mkubwa kama wa Balali usiwe na shughuli ya kuhani nyumbani kwa marehemu-mjini na kijijini. Tumeambiwa nyumbani kwa Balali mjini DSM na huko kijijini kwake Iringa hapakuwa na msiba wowote. Sasa wewe umewahi kuona wapi haya katika msiba wa kitanzania? Kubwa kuliko yote, sijawahi kuona waombolezaji wa kifo cha mkristo wakaenda kanisani wasiage mwili kama ilivyotokea kwa Balali. Sasa ni wazi kwamba matukio haya hayatoshi kuthibitisha kwamba Balali hajafa lakini bila shaka yanajenga uhalali wa kutosha wa kuhoji ukweli kuhusu kifo cha Balali. Bahati mbaya ndugu yetu Jasusi, ambaye inaonekana yupo karibu sana na familia ya Balali, inaonekana hana majibu ya ya maswali haya, na kwa sababu hizi sisi wengine tuna-question credibility ya habari zake. Kama hawezi hata kutuambia hospitali aliyokuwa anaugulia ndugu yake (hatuulizi ugonjwa) na kisha anasema alibadili jina kwa sababu ambazo hazishikiki kwa nini tuamini yale anayoyasema?

v) Umegusia kwa mbali kuhoji kwangu kuhusu credibility ya serikali yetu kuhusu kuugua na kufa kwa Balali (assuming this is true anyway) na kujenga taswira kwamba nimefanya hivi tu kwa sababu ya upinzani wangu kwa serikali. Well, of course ni kweli kwamba mimi ni miongoni mwa watu ambao hawaimini hii serikali ya CCM chini ya JK. Lakini kwa hili ni zaidi ya upinzani. Hapa tunaongelea jambo baya kabisa kwa serikali ambalo linaharibu heshima ya wananchi kwa serikali yeyote hili katika nchi yetu sio tu hii ya JK bali yeyote ijayo huko mbele. Kwanza tuliambiwa kwamba huyo anayeitwa mkurugenzi wa usalama wa Taifa (kwangu mimi ni usalama wa CCM) alienda huko US na akashangazwa kumkuta Balali yupo hai na akamtaka akipona asirudi TZ!!!!! Sasa wewe utasema huyu ni mtu anayelinda usalama wa Taifa? Hapo kweli unataka watu waimini hii serikali? Ok, twende mbele zaidi, umeshudia contradictory statements za Salva Rweyemamu na Benno Ndulu kuhusu kuugua na kufa kwa Balali-hawa wote wapo katika serikali moja na wameteuliwa na mtu mmoja. Bado utasema hapo bado tuna serikali kwa maana halisi ya serikali tunayoijua au ni mkusanyiko wa watu wanaolipwa mshahara na walipa kodi? Think again. There is something seriously wrong and fishy about this government na nyie ambao mpo nao karibu mngejitahidi kuwasaidia badala ya kujaribu kuhalalisha uchuro wanaoufanya.

Again, it is right and fine for us,you and me, to differ on these issues, but there is absolutely nothing personal here. Hii ya mtu kutofautiana na wewe na kuanza kusema anakuchafulia jina haitusaidii katika adhima yetu ya kujenga tabia ya kujadili na kutofautiana bila kugombana. Inawezekana kabisa tukatofautiana bila kufukiri mtu amekuchafulia jina au kukuchukia. More importantly, we can be loyal to each other without obstructing our independent thinking.
 
1.
Again, it is right and fine for us,you and me, to differ on these issues, but there is absolutely nothing personal here. Hii ya mtu kutofautiana na wewe na kuanza kusema anakuchafulia jina haitusaidii katika adhima yetu ya kujenga tabia ya kujadili na kutofautiana bila kugombana. Inawezekana kabisa tukatofautiana bila kufukiri mtu amekuchafulia jina au kukuchukia. More importantly, we can be loyal to each other without obstructing our independent thinking.

2.
Kama tukienda na conspiracy theory ya Mtanzania na MWK, kwamba Balali hajafa, ambayo na mimi sasa wameshanishawishi kabisa kukubaliana nao, ni wazi kwamba FMES alikuwa amesaulika katika ule mduara wa waliokuwa wanapika uongo kuhusu kuugua na kifo cha Balali. Inaonekana baadaye akakumbukwa na kupewa directions kwamba aje hapa abadili msimamo wake wakitarajia kwamba, kwa uzito wake hapa JF, hoja zake zitakubalika.

3.
Lazima tukiri kwamba huu mchezo umechezwa vizuri na wahusika wanaijua vizuri sana nguvu ya JF sasa hivi, na ndio maana wakawatumia vinara kabiaa wa JF katika kusambaza na kuaminisha habari za kiini macho kuhusu Balali. Vinara hawa waliotumika, ama kwa kujua au bila wao kujua, ndio hao niliowatajia hapo juu: Invisible, MKJJ na FMES.

Mkuu nilitegemea utakuja na apology, kwa kuandika majungu mazito ambayo ukweli ni lazima ukubali kuwa huna hata one inch of ukweli on it, never before nilitegemea kuwa siku moja utafikiria kuniweka kwenye kama unavyouita mwenyewe "Mduara" wa serikali na some people katika kujaribu kuwadanganya wananchi,

Hebu angalia hizi quote zako wenyewe mkuu zinavyojichanganya, na kutofautiana kabisa na unachokiita kutofautiana kimawazo au kiitikadi, kwa sababu ulichorushha kwenye quote hizi mbili za mwisho ni serious criminal accusations mkuu sio kutofautiana kimawazo on Balali's death,

Sasa mkuu nilitegemea utakuwa mstaarabu na ku-apologise kwa kunisngizia maneno mazito ambayo huna ukweli kabisaa mkuu, ninasema hivi hizi accusations zako ni majungu na uongo, pia ni uzandiki na very irresponsible tena kwa mtu kama wewe, kuni-place kwenye kikundi fulani cha Conspiracy Thoeries za "kuua viongozi wa serikali ili kuficha uozo wake" unasema ni kutofautiana kimawazo? Ni kuwa na independent in thinking? Ni kuwa objective? Ni kutofikiri ndani ya box lako mkuu? Unasema this is not personal?

Unasema hii ni kutofautiana tu na sio kuchafuliana jina? Mkuu kwenye hili ni lazima ukubali kuwa kwanza huna ukweli na nitashukuru sana ukiweza kuuweka ukweli hapa wa maneno yako, ikibidi ushahidi kuwa umezipata wapi hizi habari, kwa sababu ninarudia tena kuwa haya ni majungu, uzandiki, na ni uongo ambao huna ukweli, kama unao nitashukuru ukiuweka hapa JF wananchi wote wauone,

Ni haki yangu kama mwana-JF, kukubali au kukataa anything kwa kusema wazi ni kwa nini ninakubali, na ni kwa nini ninakata, na wewe pia ninajua kuwa ni likewise, lakini Mkuu Kitila mimi kuja hapa na kuanza kusema kuwa Kitila unakataa au unakubali hiii hoja kwa sababu wewe ni member wa kikundi fulani cha Conspiracy cha serikali ndio maana una maoni kama haya, unasema hii ni independent thinking? Kitila unasema bila aibu na unajaribu kutetea hii hoja kweli?

Mkuu ninasubiri utoe facts za kunihusisha na mduara wa watu wanaoua viongozi wetu, kama huna kubali na useme kuwa huna facts ila uliyajenga majungu, uzandiki, na uongo against me bila ya kuwa na ukweli hata mmoja, sidhani kama hili ni gumu kulifanya kwa mtu kama wewe! Na Ninarudia tena kuwa ninaamini 100% Balali amefariki na amezikwa tayari.

Ahsante Mkuu!
 
Back
Top Bottom