Wakuu,
Kweli naona tuko kama wale watu waliochorewa mlango ukutani halafu wakawa wanang'ang'a nia kutoka nje kupitia kwenye mchoro huo badala ya mlango wa kweli. Kati ya malumbano yaliyoendelea, Mchungaji Kishoka aliuliza kama tutapata usuluhishi wa EPA ikiwa mama Ballali ataongea na Mkuu JMushi1 akasema tutapata kujua undani wa suala hili.
Kwa kweli nilipenda swali la Mchungaji kwani naona kwamba tumemsimamia rohoni mama wa watu ambaye kwa sasa angependa amalizie msiba wake na kuendelea maisha. Hivi kama mama Ballali akiamua kusema (kama inavyosemekana aliamua kutojihusisha na serikali baada ya kumfanya mumewe adui wa umma) "I will not dignify any of your nonsense by answering any question or taking any part on this", tutafaidika vipi? Wahenga walisema, unaweza kumleta punda mtoni kwa lazima lakini huwezi kumlazimisha anywe maji (sikusudii kumfananisha mama Ballali na punda bali ni kuelezea pointi yangu).
Mkuu Mushi nae alimjibu mchungaji jawabu zuri sana (na kwa hili nakubaliana naye) kuwa tunataka tujue undani wa EPA. Nafikiri hii ndio fundamental desire of every JF member...kujua ilikuwaje. Lakini kwa bahati mbaya naona tumeingia kiza na kumshupalia Ballali as if yeye ndio mtuhumiwa. Kama ni shahidi nyota wa serikali, kwanini wengine hatujawashupalia, kina Mramba, Mgonja, Rostam, Chenge na wengineo wengi?
Inasikitisha kuona kuwa tunatoka nje ya mstari na kuanza kufuatilia jinsi Ballali alivyofunga ndoa na mkewe au wake wa zamani...how is this relevant? Najua kuna watu watataka kusema kuwa Ballali na mkewe walishirikiana, lakini kabla ya kusema hivi, waelewe kwamba, Ballali hakuwahi kushtakiwa wala kutajwa kama mtuhumiwa hivyo mambo ya familia yake yalikuwa ni ya kwake na sio ya taifa.
Ningependa kupendekeza kuwa huyu mama mwacheni apumzike, keshateseka sana kuuguza na hahitaji maneno kuchangamsha siku yake. Kwa wale ambao wanaamini kuwa Ballali amefariki, vema, endelea na imani yako kwa amani. Vivyo hivyo kwa wale ambao hawaamini kuwa Ballali amefariki, vema, endelea na imani yako kwa amani. Kwa wengine kama mimi, well, tuiweke serikali kitimoto ili tujue ni nani walihusika na hatima yao ni ipi? Na kwanini wengine waliondolewa nyadhifa zao serikalini wakati wengine bado wanaendelea kupeta. Je tutegemee fedha nyingine zaidi zichotwe wakati tunakaribia uchaguzi ujao? Nafikiri haya ndio maswali tunapaswa kudeal nayo.