Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

After consipary theories are solved by Mama Muganda Ballali then what? Do we get solution on EPA, Meremeta and Tangold?

Issue hapa sasa ni mtu aliyekuwa karibu vya kutosha na mtuhumiwa wa kwanza!

Mtu ambaye na yeye pia ni mtuhumiwa!Sasa kama wana connection ya ki Bonnie and Clyde watatenganishwa vipi?

Si ni yeye huyo Anna Muganda Ballali amekataa kutoa ushirikiano kwa watanzania kwa vigezo vya siri ya familia?

Yani kwamba watanzania hawahusiki na upotevu wa zaidi ya dolla billion 3 za kimarekani ambazo yeye na mumewe huyo aliyetutangazia kuwa ni marehemu walihusika kwa namna moja ama nyingine kuzifuja pesa za masikini!?

Mwanamama aliyekuwa na uhusiano na pia aliyeoana na Ballali kabla ya scandal kujulikana aachwe nje ya mjadala kwa vigezo vipi hivyo?

Halafu kuwa naye kipindi chote hadi kifo kilipotangazwa asitajwe kwenye huu mjadala?
Narudia tena...Kama mama hatotoa ushirikiano basi acha iwe mbaya!

Meku,

Naona hapa wewe ndio umekuwa mpelelezi, mwendesha mashtaka na jaji kwa pamoja. Nikumbushe ni lini Ballali alishtakiwa au kutajwa kuwa ni mtuhumiwa?
 
Wakuu,

Kweli naona tuko kama wale watu waliochorewa mlango ukutani halafu wakawa wanang'ang'a nia kutoka nje kupitia kwenye mchoro huo badala ya mlango wa kweli. Kati ya malumbano yaliyoendelea, Mchungaji Kishoka aliuliza kama tutapata usuluhishi wa EPA ikiwa mama Ballali ataongea na Mkuu JMushi1 akasema tutapata kujua undani wa suala hili.

Kwa kweli nilipenda swali la Mchungaji kwani naona kwamba tumemsimamia rohoni mama wa watu ambaye kwa sasa angependa amalizie msiba wake na kuendelea maisha. Hivi kama mama Ballali akiamua kusema (kama inavyosemekana aliamua kutojihusisha na serikali baada ya kumfanya mumewe adui wa umma) "I will not dignify any of your nonsense by answering any question or taking any part on this", tutafaidika vipi? Wahenga walisema, unaweza kumleta punda mtoni kwa lazima lakini huwezi kumlazimisha anywe maji (sikusudii kumfananisha mama Ballali na punda bali ni kuelezea pointi yangu).

Mkuu Mushi nae alimjibu mchungaji jawabu zuri sana (na kwa hili nakubaliana naye) kuwa tunataka tujue undani wa EPA. Nafikiri hii ndio fundamental desire of every JF member...kujua ilikuwaje. Lakini kwa bahati mbaya naona tumeingia kiza na kumshupalia Ballali as if yeye ndio mtuhumiwa. Kama ni shahidi nyota wa serikali, kwanini wengine hatujawashupalia, kina Mramba, Mgonja, Rostam, Chenge na wengineo wengi?

Inasikitisha kuona kuwa tunatoka nje ya mstari na kuanza kufuatilia jinsi Ballali alivyofunga ndoa na mkewe au wake wa zamani...how is this relevant? Najua kuna watu watataka kusema kuwa Ballali na mkewe walishirikiana, lakini kabla ya kusema hivi, waelewe kwamba, Ballali hakuwahi kushtakiwa wala kutajwa kama mtuhumiwa hivyo mambo ya familia yake yalikuwa ni ya kwake na sio ya taifa.

Ningependa kupendekeza kuwa huyu mama mwacheni apumzike, keshateseka sana kuuguza na hahitaji maneno kuchangamsha siku yake. Kwa wale ambao wanaamini kuwa Ballali amefariki, vema, endelea na imani yako kwa amani. Vivyo hivyo kwa wale ambao hawaamini kuwa Ballali amefariki, vema, endelea na imani yako kwa amani. Kwa wengine kama mimi, well, tuiweke serikali kitimoto ili tujue ni nani walihusika na hatima yao ni ipi? Na kwanini wengine waliondolewa nyadhifa zao serikalini wakati wengine bado wanaendelea kupeta. Je tutegemee fedha nyingine zaidi zichotwe wakati tunakaribia uchaguzi ujao? Nafikiri haya ndio maswali tunapaswa kudeal nayo.

Maoni yangu ni kuwa kama tusipokuwa makini sasa watanzania watahisi vibaya jinsi ambavyo wanatishwa ama kutukanwa wanapouliza maswali muhimu kuhusiana na wizi wa mali zao!

HAKUNA CHA PERSONAL ISUE ZA KIFAMILIA PALE INAPOKUJA KWENYE HAKI YA MTANZANIA KUHUSIANA NA KASHFA HII!

Nani asiyejua hata serikali yenyewe imegwaya kuwashughulikia mafisadi?
Halafu kama kuna wale wasioamini kuwa ni lazima kuna wale tutakaojitolea muhanga...Then wamekosea!
 
Meku,

Naona hapa wewe ndio umekuwa mpelelezi, mwendesha mashtaka na jaji kwa pamoja. Nikumbushe ni lini Ballali alishtakiwa au kutajwa kuwa ni mtuhumiwa?

Kutokana na taarifa zote...Mkapa,Ballali na mama Anna Muganda wametajwa kuhusika na kashfa...Serikali imekataa kuwashughulikia kwasababu zao wanazozijua...Mtu aliyekuwa amebakia ambaye alikuwa na nafasi ya kuwapa ukweli watanzania ni Anna Muganda Ballali!
Sasa nyie mnaokataa asitajwe ndio wale ambao mli misscaliculate the serioussness and the resolve of the true patriots!
Kama kweli wanataka tuachane nao watoe habari ambazo Taifa zima linazililia!
 
Kutoshitakiwa kwa Ballali na baadae kufa ki utata si ndio mtego na ufisadi juu ya ufisadi?
Tutauliza maswali kwa niaba ya watanzania hata iweje!
Tunajua kuna vikwazo...Lakini hilo halitanizuia kuuliza yale wananchi wanayouliza kila siku mitaani!
Narudia tena ni lazima muelewe kuwa kutotajwa na serikali kwa Ballali kama mtuhumiwa ndio moja wapo ya sababu za mjadala huu kwamba kuna uwezekano wa foul play!
Uchunguzi wa foul play kwa wale ambao hawaelewi namna FBI wanavyofanya uchunguzi...Basi pia hawataelewa kuwa hakuna cha personal issues kwenye chunguzi kama hizo!
HAPA MAREKANI MTU AKIFA SUSPECT WA KWANZA NI EITHER MKE AMA MUME!

Kwa taarifa yako personal issues zinawezekana ndizo zilizobeba siri yote!
 
Kutokana na taarifa zote...Mkapa,Ballali na mama Anna Muganda wametajwa kuhusika na kashfa...Serikali imekataa kuwashughulikia kwasababu zao wanazozijua...Mtu aliyekuwa amebakia ambaye alikuwa na nafasi ya kuwapa ukweli watanzania ni Anna Muganda Ballali!
Sasa nyie mnaokataa asitajwe ndio wale ambao mli misscaliculate the serioussness and the resolve of the true patriots!
Kama kweli wanataka tuachane nao watoe habari ambazo Taifa zima linazililia!

Mkuu,

Kulingana na maelezo yako hapo juu, inaelekea kuna watu watatu. Let's say wote walishiriki, mbona vidole vinanyooshwa kwa mtu mmoja (au wawili) tu? Katika wote hao uliowataja, ni nani hasa aliyekuwa na nguvu (final say and influence). Mkapa anaachiwa bila kusakamwa huku akitutusi na kusema kuwa anaishi kwa pensheni tu, je hii ni haki?

Jasusi aliomba tutajiwe anwani za nyumba za kina Ballali zilizopo huko Italy, Switzerland na kwengineko, mbona hatujapata jibu? Lakini tunajua nyumba za Mkapa zilipo whether ni Masaki au Lushoto (bila kutaja ya Ocean Road ambayo ni ya zamani na next to it ilipo Bank M), sasa mbona tunamwachia huyu bwana akipeta tu? Kwani si tunajua mshahara wa Rais na marupurupu yake (hata ukichukulia wakati akiwa waziri)? Kweli kwa mshahara huo, mtu anaweza kuwa na mali zote hizo na kamgodi kadogo pale Kiwira?

Hapa naona ni tunatwanga maji au kujaribu kuzima moshi wakati tunaacha chanzo cha moto kikijiimarisha.
 
Kutoshitakiwa kwa Ballali na baadae kufa ki utata si ndio mtego na ufisadi juu ya ufisadi?
Tutauliza maswali kwa niaba ya watanzania hata iweje!
Tunajua kuna vikwazo...Lakini hilo halitanizuia kuuliza yale wananchi wanayouliza kila siku mitaani!
Narudia tena ni lazima muelewe kuwa kutotajwa na serikali kwa Ballali kama mtuhumiwa ndio moja wapo ya sababu za mjadala huu kwamba kuna uwezekano wa foul play!Uchunguzi wa foul play kwa wale ambao hawaelewi namna FBI wanavyofanya uchunguzi...Basi pia hawataelewa kuwa hakuna cha personal issues kwenye chunguzi kama hizo!
HAPA MAREKANI MTU AKIFA SUSPECT WA KWANZA NI EITHER MKE AMA MUME!

Kwa taarifa yako personal issues zinawezekana ndizo zilizobeba siri yote!

Meku,

Hapa ndipo nakubaliana nawe kuwa tunataka tujue ni nani hakutaka Ballali atoe ushahidi na kwa sababu gani.

Kwa upande mwingine, niwie radhi, sikujua wewe ni mtaalam wa FBI na namna wanavyofanya uchunguzi. Hata hivyo, pamoja na ulimbukeni wangu huo najua kuwa nchini Marekani, suspect anakuwa ni spouse pale kifo kinapokuwa ruled as a homicide. Illness, nope. With illness I believe the suspect is, well, whatever the diagnosis of an illness and FBI will not be involved. Even if it is a homicide, in most cases local detectives will deal with it.
 
Kwa taarifa yako personal issues zinawezekana ndizo zilizobeba siri yote!

Meku,

In court of law the language such as "zinawezekana" is known as speculation. With all due respect, I do not believe you'd want to be person speculates but rather provide facts, correct?
 
Mushi,
You are a piece of shit. We are supposed to be talking about issues and not personalities Di8vorce ya mtu na ndoa ya mtu inahusiana vipi na nini?
You are a piece of shit. FMES samahani mkuu, nilisema sitarudi tena lakini siwezi kuvumilia upumbavu kama huu!

Mheshimiwa Jasusi,

Nafikiri hapa JF tumejadili mara nyingi tu juu ya ndoa za viongozi wetu, naweza kukutafutia baadhi ya threads ambazo hata wewe umechangia.

Pambana na Jmushi1 kwa hoja na sio matusi, kama kitchen inaanza kuwa too hot, you better get out of it.

Kwenye hili naamini Ballali na Muganda wote ni wahusika, hivyo kwa wanaotaka wana kila right ya kuchimba mpaka chini juu ya mambo yao. Jmushi1 hajatoka nje ya hawa wawili na binafsi naona ni ruhusa tu. Tumemjadili Mkapa na mama Mkapa ndio iwe Ballali na mama Ballali?
 
Wakuu,

Kweli naona tuko kama wale watu waliochorewa mlango ukutani halafu wakawa wanang'ang'a nia kutoka nje kupitia kwenye mchoro huo badala ya mlango wa kweli. Kati ya malumbano yaliyoendelea, Mchungaji Kishoka aliuliza kama tutapata usuluhishi wa EPA ikiwa mama Ballali ataongea na Mkuu JMushi1 akasema tutapata kujua undani wa suala hili.

Kwa kweli nilipenda swali la Mchungaji kwani naona kwamba tumemsimamia rohoni mama wa watu ambaye kwa sasa angependa amalizie msiba wake na kuendelea maisha. Hivi kama mama Ballali akiamua kusema (kama inavyosemekana aliamua kutojihusisha na serikali baada ya kumfanya mumewe adui wa umma) "I will not dignify any of your nonsense by answering any question or taking any part on this", tutafaidika vipi? Wahenga walisema, unaweza kumleta punda mtoni kwa lazima lakini huwezi kumlazimisha anywe maji (sikusudii kumfananisha mama Ballali na punda bali ni kuelezea pointi yangu).

Mkuu Mushi nae alimjibu mchungaji jawabu zuri sana (na kwa hili nakubaliana naye) kuwa tunataka tujue undani wa EPA. Nafikiri hii ndio fundamental desire of every JF member...kujua ilikuwaje. Lakini kwa bahati mbaya naona tumeingia kiza na kumshupalia Ballali as if yeye ndio mtuhumiwa. Kama ni shahidi nyota wa serikali, kwanini wengine hatujawashupalia, kina Mramba, Mgonja, Rostam, Chenge na wengineo wengi?

Inasikitisha kuona kuwa tunatoka nje ya mstari na kuanza kufuatilia jinsi Ballali alivyofunga ndoa na mkewe au wake wa zamani...how is this relevant? Najua kuna watu watataka kusema kuwa Ballali na mkewe walishirikiana, lakini kabla ya kusema hivi, waelewe kwamba, Ballali hakuwahi kushtakiwa wala kutajwa kama mtuhumiwa hivyo mambo ya familia yake yalikuwa ni ya kwake na sio ya taifa.

Ningependa kupendekeza kuwa huyu mama mwacheni apumzike, keshateseka sana kuuguza na hahitaji maneno kuchangamsha siku yake. Kwa wale ambao wanaamini kuwa Ballali amefariki, vema, endelea na imani yako kwa amani. Vivyo hivyo kwa wale ambao hawaamini kuwa Ballali amefariki, vema, endelea na imani yako kwa amani. Kwa wengine kama mimi, well, tuiweke serikali kitimoto ili tujue ni nani walihusika na hatima yao ni ipi? Na kwanini wengine waliondolewa nyadhifa zao serikalini wakati wengine bado wanaendelea kupeta. Je tutegemee fedha nyingine zaidi zichotwe wakati tunakaribia uchaguzi ujao? Nafikiri haya ndio maswali tunapaswa kudeal nayo.

Mkuu,

Argument yako ina make sense kama tu unaamini Ballali kafa, wengine tunaamini hajafa, hivyo hakuna masiba wala majonzi ambayo Anna Muganda anatakiwa ayamalize salama.
 
Mheshimiwa Jasusi,

Nafikiri hapa JF tumejadili mara nyingi tu juu ya ndoa za viongozi wetu, naweza kukutafutia baadhi ya threads ambazo hata wewe umechangia.

Pambana na Jmushi1 kwa hoja na sio matusi, kama kitchen inaanza kuwa too hot, you better get out of it.

Kwenye hili naamini Ballali na Muganda wote ni wahusika, hivyo kwa wanaotaka wana kila right ya kuchimba mpaka chini juu ya mambo yao. Jmushi1 hajatoka nje ya hawa wawili na binafsi naona ni ruhusa tu. Tumemjadili Mkapa na mama Mkapa ndio iwe Ballali na mama Ballali?

Hapana, Mtanzania.
Hapa sikubali. Mkapa na mkewe walituomba kura they are fair game.
Ballali na mkewe hawakuwa viongozi wetu. They never campaigned for any position of public leadership. Let's be fair. Otherwise nitaomba Moderator aingilie kati na kama mimi ndiye mwenye makosa nipigwe palanja.
 
Anko vipi tena....this is out of your character....
Nyani,
I know it is out of my character lakini hata siku 40 hazijapita kuna wapumbavu wanasema hatujafiwa. Ungefanya nini ungekuwa katika viatu vyangu?
 
Jasusi,
Siyo obligatory kujibu kila kinachoandikwa hapa, vinginevyo unaweza kujikuta unaumia zaidi. Nafikiri kwa kuwa inaelekea wewe ni member wa family ya wafiwa, ungetusaidia kuhakikisha ule wosia alioacha marehemu unakuwa public, if at all what was reported by raia mwema has any truth.
 
Nyani,
I know it is out of my character lakini hata siku 40 hazijapita kuna wapumbavu wanasema hatujafiwa. Ungefanya nini ungekuwa katika viatu vyangu?

Hey...ndio maana wikendi hii iliyopita hata Nyani Ngabu alikufa lakini kuna ambao hawaamini...
 
Kitila, FMES, Mwanakijiji, naona mna endorse matusi ya Jasusi kwa JMushi.

Mpaka Nyani Ngabu anakuwa moral authority kwenye usuluhishi wa matundiko yenye matusi?
Nyani, no offense here. Nashangazwa tu na double-standard za makomredi wangu hapa.

Anna Muganda alituhumiwa kwa ufisadi na kesi yake ilitetewa ndani ya Bunge na Nazir Karamagi, mtuhumuiwa mwingine wa ufisadi. Sasa kama uadilifu wa Anna Muganda umejadiliwa ndani ya Bunge la Tanzania, tutawezaje kushabikia Jmushi anvyotukanwa kwa kuleta discussion ya Anna Muganda hapa?

Mi sikubaliani na kila anachosema Jmushi, na kuna wakati nakerwa na jinsi anavyouliza maswali ambayo wakati mwingine ni kama marudio rudio.

Lakini tukianza ku endorse matusi ya Jasusi hapa, hiki kitakuwa kijiwe kweli hapa. Kama ndo mnaruhusu matusi semeni. Msione tunavumilia tukitukanwa, tutafukuzwa wote hapa, Oohooo!

Wee vipi bana..? Utatoaje kauli kama hiyo halafu unasema no offense? Hivi unadhani mimi nitaichukuliaje? Tatizo la baadhi yenu mmejiweka katika level fulani ambayo inawafanya mjione mko bora zaidi (morally, intellectually, etc.) zaidi ya wengine wakati si hivyo hata kidogo. Nyani Ngabu is just my alter ego. It's not the real me. Should you be fortunate enough to meet me in person one day, you'll be shocked in disbelief. Please, keep my name out of your mouth and don't use me as an example for anything, okay?
 
Ukiona hivyo ujue tumechoka; inafika mahala unasema acha liende tu. Sasa kama kuna watu hadi leo wanaamini kwamba Balali hakushiriki kutuibia, kwa nini tusiwape sarcastic thanks hata wakitoa matusi, si ndivyo walivyo? au?

Afrika ngumu ndugu yangu. Wewe hujasikia mke wake Mugabe anawambia wapinzani huko Zimbabwe kuwa mume wake hatoki ikulu ng'o na wapinzani walie tu kwa sababu hawatakuja kuiona ikulu na hakuna mtu wa kumtoa Mugabe madarakani hadi siku zake hapa duniani ziishe. Kwa hali hii utaacha kudata?
 
Wee vipi bana..? Utatoaje kauli kama hiyo halafu unasema no offense? Hivi unadhani mimi nitaichukuliaje? Tatizo la baadhi yenu mmejiweka katika level fulani ambayo inawafanya mjione mko bora zaidi (morally, intellectually, etc.) zaidi ya wengine wakati si hivyo hata kidogo. Nyani Ngabu is just my alter ego. It's not the real me. Should you be fortunate enough to meet me in person one day, you'll be shocked in disbelief. Please, keep my name out of your mouth and don't use me as an example for anything, okay?

Nimesema no offense kwa sababu umeonyesha leadership ulivyo muhoji Jasusi kwa matusi yake, lakini na wewe una rekodi ya matusi hapa kwenye hili jamvi na umejaa mizaha kama thread yako ya "Nyani Kafa..." ambayo imepeteshwa na Wakuu.

Ndo maana nikasema hata Nyani Ngabu ana rise to a higher plane kusuluhisha matusi, huku wale ambao kawaida huwa wanakemea mizaha na matusi kwenye jamvi hapa leo wanatoa vi thanks kwenye matusi ya Jasusi.

Humu JF kumejaa double standards. Kuna watu wanatukana with impunity.

Na, mimi leo nitajiwekaje kwenye moral/intellectual level juu yako Nyani? Wewe si unajua mi ni "juha kama jiwe"? Sasa lini ulinipandisha cheo?
 
Hivi hii thread yenyewe sio mzaha? Balali ni binadamu kama sisi. Ana ndugu, familia, na watu wanaompenda. Hajapatikana na hatia yoyote ya hayo anayotuhumiwa. Habari zikaja kwamba amefariki. Wengine wakaja na habari (maoni yao) kuwa hawaamini kama amefariki. Hivi mnadhani ndugu wa Balali (regardless of whether he's dead or not) wakiingia humu na kusoma yote yanayosemwa kuhusu uhai wake watajisikiaje? Uhai wa mtu sio jambo la mzaha. Kusema Nyani Ngabu kafa si sawa na kusema Balali kafa au hajafa. Nyani Ngabu sio jina langu. Ni jina bandia tu. Yeyote yule anaweza akajiita Nyani Ngabu. Daudi Balali ni jina la mtu na sio jina bandia (kwa kadri nijuavyo). Jamani, tuwe sensitive kidogo kwa baadhi ya mambo.
 
Mushi,
You are a piece of shit. We are supposed to be talking about issues and not personalities Di8vorce ya mtu na ndoa ya mtu inahusiana vipi na nini?
You are a piece of shit. FMES samahani mkuu, nilisema sitarudi tena lakini siwezi kuvumilia upumbavu kama huu!

mzee Jasusi, pamoja na yote unayoyasema na hisia zako kuhusu suala hili kwenda ulikokwenda si sahihi hata kidogo. Hoja hujibiwa kwa hoja na kama unaona wanacholeta ni vioja basi unaachana nao. Kwa kutukana au kumuita Mushi majina hakufanyi hoja zako za utetezi kuwa na nguvu zaidi.

Ninaelewa frustrations na hisia za kuingiliwa privacy yako na ya familia. Hata hivyo, kama tulivyojifunza katika kumzungumza Mengi (ambaye si public servant) kama tumeweza kuwazungumza kina Manji na watu wengine utaona kuwa mtu aliyekuwa mtumishi wa umma (kama ilivyokuwa Ballali) anakuwa ni fair game linapokuja suala la kuzungumzia mambo yake.

Katika hili Bi. Anna Muganda ni fair game kwa kadiri huyu Mushi anaona na kwa watu ambao wanafuatilia. Hata hivyo, naamini kuna mambo ambayo yanamlinda mwenzi wa mtu kusimama kuwa shahidi dhidi ya mume/mke wake. Marekani kuna hiyo sheria ambayo mara nyingi inamzuia mke/mume kuwa shahidi katika kesi inayomhusu Mwenzi wake.

Unazo hoja nzito za utetezi lakini kuvuka mstari na kumtukana huyu bwana mdogo kwa vile hukubaliani naye si sahihi na itakuwa uungwana kama utamwomba radhi ili tuendelee. Matusi dhidi ya mtu binafsi lazima tuyakatae ni hoja tu zinazopendwa.
 
Umeamua haki!
 
Nyani,
I know it is out of my character lakini hata siku 40 hazijapita kuna wapumbavu wanasema hatujafiwa. Ungefanya nini ungekuwa katika viatu vyangu?

Ukiona mtu anaanza kutukana jua hoja imeanza kumshinda, Nyerere angesema hoja za manguvu hizo. Inasikitisha kwamba hao hao wanaoongoza kujadili ndugu za wengine, mambo yakiwakaribia wanaanza kutumia matusi.

Unaweza kuita watu wapumbavu utakavyo wala kwa mimi haiwezi hata kunikosesha usingizi na nitaendelea kujadili suala la Ballali na Anna Muganda bila kujali kelele za mtu yeyote.

Watu tumeshindwa kutishika na vifungo, ndio yawe matusi?
 
Back
Top Bottom