Deejay nasmile
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 5,794
- 5,352
KIFO NI KIBAYA SANA..NI BORA UFE WEWE KULIKO ATANGULIE YULE ULIMPENDA NA KUMZOEA.
Habari wakuu,poleni na majukumu
Najua kila mtu ameshawahi kusikia neno KIFO..ndio ni neno fupi lenye herufi chache tu,Herufi nne yaani K I F O.
Nadhani tukiongelea katika maneno ambayo yanaogopwa na hayapendwi na kiumbe yeyote,neno KIFO linaweza kuwa namba moja.
KIFO hakipendwi, KIFO kinaogopwa,KIFO kinachefua.Haijailishi ni KIFO cha kitu gani,KIFO cha kiumbe hai mfano Binadamu/mnyama au KIFO cha Kitu kingine mfano Biashara,kazi,uhusiano n.k
Hili neno lipo miaka na miaka, nadhani tangu kuumbwa kwa ulimwengu tumekuwa tunalisikia Au kuona kifo cha watu,mimea,wanyama na hata kifo cha biashara,kazi..Japo leo mada kuu ya leo ni kuhusu KIFO cha binadamu.
KIFO NI NINI??
Kifo ni fumbo kubwa sana ambapo hakuna mtu hata mmoja aliye hai anajua fumbo hili,ni fumbo ambalo Mungu amewafumbia wanadamu,viumbe hai,na utajua fumbo hili pindi utakapo kufa.
Japokuwa kuna baadhi ya watu kutokana na imani/akili au mawazo yao wamejaribu kusema maana tofauti tofauti kuhusu KIFO.Wengine wanasema ni KIFO ni Usingizi,ndoto N.k
Lakini maana iliyo kuu au maalumu ni kwamba KIFO ni hali ya kufarakana au kutengana kwa vitu au hali zinazofanya UHAI kuwepo.Ndio Ni tendo la KUKOSA au kutokuwa na UHAI.
Kwanini Kuna KIFO?
Hili swali nalo lina majibu mengi sana kutokana na imani au elimu zetu za duniani.
Kutokana na imani yangu naamini tunakufa ili Kurudi kule kwa MUUMBA WETU.Ndio huwezi kumuona muumba wako kama hujafa,lakini tu kama utatimiza kazi ile uliyotumwa na muumba wako ipasavyo .
KIFO hakina muda maalum ni wakati wowote kifo kinaweza kukumba,haijalishi u mzima au mgonjwa au umejificha mahali gani.
TURUDI KWENYE MADA
Mwaka huu 2021 kwa upande wangu ndio mwaka ambao nimejua uzito,maumivu na ubaya wa KIFO. Nilimpoteza Mtu muhimu. Mtu niliyezoea kumuona kwa miaka yote 30s niliyonayo.Mtu ambaye sikuwahi wala kuweza kuishi naye mbali kwa muda wa miezi mitatu bila kuonana nae.. Hata wakati nikiwa chuo kila mwisho wa semister lazima tu nitaenda kuhakikisha naonana nae,naongea nae,nacheka nae..kisha ndio naendelea na ratiba zingine.
Mtu ambaye hata nikifanya ukorofi,ujinga wowote alikuwa achoki kunitetea. Mtu ambaye nikiwa na huzuni analiwaza na kunipa ushauri HAKIKA nilijiona nina bahati mimi. Sikuwaza kumpoteza Mtu huyu.
Sio kwamba sikuwahi kusikia KIFO,au kuwahi kufiwa kabla.. HAPANA!!..Nilifiwa na Baba yangu mzazi,Bibi na Babu zangu,Mashangazi,Walimu,Marafiki N.k lakini sikuumia sana..
Najua utajiuliza KWANINI?
Je, nilikua siwapendi? HAPANA!
Nilikuwa nawapenda sana,lakini shida kubwa hapa ni ...
UPENDO NA MAZOEA
Wakati baba anafariki nilikuwa na miaka 4..kwa hiyo hapo utaona kuwa kwanza sikuwa na kitu HISIA na kujua nini kimetokea kutokana na umri wangu..Pia sikumzoea sana kutokana na kuishi nae muda mchache (4yrs)
Nilifiwa na marafiki,jamaa na ndugu wengine wengi. Hao wote niliumia lakini naweza kusema sio sana...au niseme maumivu/majonzi yaliwahi kuisha/kusahaulika mapema.
KWANINI?
Ni kwa sababu niliwapenda ila SIKUWAZOEA!!
Mwalimu ilikuwa ni mpaka nimuone shuleni/darasani tu,
Shangazi au Rafiki ni mpaka tukutane kwenye miadi,kikao,michezo au kwa shughuli flani.
Hivyo tukiachana hapo kila mtu anawaza yake anaendelea na mambo yake. Je? Hujawahi kuona unapata taarifa tu kuwa rafiki yako yule siku hizi Mbunge! Alafu ukawa hujui aliingia lini kwenye siasa,chama gani wala jimbo gani..??
Au shangazi yako amefariki !!! ukawa hujui ameumwa lini,au alipatwa na nini.
NDIO MAANA NAONA NI BORA NINGETANGULIA MIMI (MUNGU ANISAMEHE KAMA NAKOSOA KAZI YAKE)KULIKO YULE NILIYEMPENDA NA KUMZOEA!!!
MAMA! MAMA YANGU
Umeniachia pigo kubwa sana katika maisha yangu, sidhani kama nitakuja kuamini kuwa sitakuona tena..MAMA nilikupenda,ninakupenda na nitakupenda daima...SIO TU NILIKUPENDA LAKINI PIA NILIKUZOEA SANA.
Kuna muda natamani hata nisikanyage hapa nyumbani pale tu ninapokumbuka kuwa HAUPO tena humu ndani...NILIZOEA nikitoka huko mtaani nakuja nakusimulia story zote zinazoendelea huko mtaani,nikifanya jambo baya unaniita kwa upole,unanikalisha na kunifundisha namna nzuri ya kuishi.
Juzi timu yetu pendwa imepatwa na matokeo mabaya najua Tungeliwazana wenyewe.Lakini nasikitika hata hukupata nafasi ya kutazama timu yako pendwa japo uliipania sana Ile mechi..Na sio hayo tu kuna mambo mengi tulipanga but hayajakamilika bado na UMENIACHA mpendwa wangu.najua hata nikikamilisha peke yangu sitakuwa na fuaraha sana kama vile na wewe ungeona kile tulichopanga kimekamilika..sitakuwa na thamani nacho kama wewe HAUPO..
MAMA ni mtu ambaye kwangu mimi alikuwa ni kila kitu..Ilifika mahali nilisahau kabisa kama kuna KIFO..Na hata mara chache nilipokuwa nikikumbuka kuhusu KIFO nilijua ni mimi nitakufa,yule atakufa,wale watakufa ila sio yeye MAMA.sikawahi kujua watu wanapitia uchungu wa namna hii..Nilidhani wanajiliza tu kujifanyisha,niliwaona ni wajinga sio majasiri,lakini HATIMAYE pamoja na ujasiri wangu hatimaye NIMELIA MIMI, NIMELIA MBELE ZA WATU...MBELE YA WATOTO WADOGO.....Mtu NILIYEMPENDA NA KUMZOEA HAYUPO TENA..SITAMUONA TENA DAH!!!
HEBU FIKILIA YULE UNAYEMPENDA NA ULIYEMZOEA
1:ANAKUFA!
Yaan hana pumzi,haongei unamuuliza hakujibu,unatamani umpe kile chakula akipendacho lakini hawezi kula.Unaiona namba yake ya simu kwenye simu yako unatamani kumpigia lakini unakumbuka kuwa HATAPOKEA,Hatajibu sms...unawaza vipi niifute? HAPANA!! HAPANA!! Huko aliko ananiona nafuta namba yake...anasikitika kuwa namtenga ..SIWEZI kuifuta namba yake na sitaisahau Daima..
2:Mnamuweka kwenye JENEZA.
Marafiki zako,ndugu zako wanaenda kuchagua jeneza,huku wakisema HILI ZURI!! dah kuna JENEZA zuri??? unatamani uwatukane,unaona kama wanafanya ukatili..lakini BASI SASA!! Ndio utaratibu huo.
3:MNAMFUKIA chini ya ardhi..
Unawaza Vipi
Labda pengine Alilala tu na ameamka na kuzinduka kisha anatuita tumfukue lakini hatusikii na tunaondoka tu,
Mnamuacha peke ake makaburini,anakata tamaa..anajiuliza mpaka wewe kipenzi chake unamtenga?? humsikii??
Usiku vile unavotisha lakini unamuacha kule peke ake??...Lakini wewe umelala ndani,umejifunika shuka! umewasha taa! na umefunga milango..INAUMA SANA !!!
Ni MTIHANI MGUMU SANA KUMPOTEZA MTU ULIYEMZOEA...KUNA MUDA NAJIULIZA KWANINI NISINGEANZA MIMI AKABAKI YEYE...PUMZIKA MAMA YANGU
HITIMISHO:
NAJUA KILA MTU ANA MTU WAKE ANAYEMPENDA NA ALIYEMZOEA AMBAYE HAKUPENDA/HATAPENDA AFIKWE NA UMAUTI.LAKINI AMINI KIFO KIPO JAPO HATUKIPENDI,MIMI NIMEAMINI JAMANI KIFO KIPO.
MIMI KIFO CHA MAMA NI KIFO KINACHONIPA MTIHANI MKUBWA SANA WA KUSAHAU..SIDHANI KAMA NITAFAULU,WAPO WANAOMPENDA NA WALIOMZOEA
BABA YAO
MAMA YAO
DADA YAO
KAKA YAO
MKE WAKO
MUME WAKO
MTOTO/WATOTO WAKO
N.K
JE UTAFAULU MTIHANI WA UCHUNGU UTAKAOPITIA SIKU WAKITUTOKA?? SIKU KIKIWAKUMBA????
TUZIDI KUWAOMBEA KWA MWENYEZI MUNGU KILA SIKU.SARA NI MUHIMU..
INAUMA SANA KUFIWA NA UNAYEMPENDA NA ULIYEMZOEA.
LAKINI PIA TUKUMBUKE KUWA SIO KILA KIFO NI KIBAYA KUTOKANA NA TULIVYOJIANDA SISI WENYEWE KWA MUUMBA WETU.
Tunapitia kipindi kigumu sana..
Ewe Mola, nisamehe dhambi zangu, dhambi za baba yangu, mama yangu, mke/mume wangu na wanangu na jamaa zangu na marafiki.
Ewe Mwenyezi Mungu , usiuchukue uhai wangu ila pale nitakapo kuwa tayari kukutana nawe.AMEENI
By nasmiletz
july 2021
nasmiletz@gmail.com

Upvote
23