Kifo cha Mwalimu Nyerere 14/10/1999, ulikuwa wapi?

Kifo cha Mwalimu Nyerere 14/10/1999, ulikuwa wapi?

Darasa la pili shule ya msingi Yombo Dovya,siku hii hua naikumbuka sana maana wali ulipakuliwa kwenye sinia nikaambiwa nitakula na marehemu bibi yangu,
Basi kila nikimuita aje kula anasema wee endelea .. endelea ,nikamaliza wali wote bibi akalala njaa kisa tuu kifo cha baba wa taifa maana tv ilikua moja tuu mtaani kwa jirani
 
Nilikuwa kwenye daladala maeneo ya Fire uelekeo Forodhani sekondari,ghafla mwimbo wa Taifa,Tukajua tu tayari Mwalimu Nyerere ametutoke!Majira ya Mchana hivi ilikuwa nilikuwa naingia zamu ya Mchana Shule,enzi hizo shule ile Ina zamu ya Asubuh na mchana,kwa Form 1 na Form 3,then form 2 na Form 4 wanaingia kwa wakati mmoja!
 
Nilikuwa darasa la 2 shule ya msingi chemchem, Iringa mjini. Nilimuuliza mama yangu huyo Nyerere atapokelewa wapi, akanambia kaenda moja kwa moja kwa Mungu maana hana dhambi, kuskia hivyo nikafarijika. Hahahahaaa utoto raha sana haya kama wapo waliosoma chemchem enzi hizo hebu tuwasiliane.
Mm pia nmesoma chem chem enzi za mwalimu mkuu sailes
 
Wengi humu wakati J.K wakwanza anafariki walikuwa bado wanapanga mavi ya mafungu mafungu[emoji90] [emoji90] [emoji90] [emoji90] [emoji90]
 
Nilikua nimemaliza darasa la7 mwaka huo tukazuiwa hadi kufanya sherehe yetu ya kuhitimu elimu ya msingi kisa maombolezo ya siku 30 aliotoa bwana ben
 
Nilikuwa std VI, unaambiwa saa sita na wimbo wa taifa kwenye rtd, kufika shule tukaambiwa turudi nyumbani Mwalimu Nyerere amefariki[emoji13] [emoji13] Mwanzo nilifikiri Nyerere ndio mwalimu mkuu[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
 
Nilikuwa darasa la kwanza Kamunyonge s/m..ile nafika shule mida ya saa 7 siku hyo alhamisi namkuta mwl matete paredi na bendera tayari ikiwa robo tatu ya mlingoti
Habari za FFU hapo?
 
Lazima niwe mkweli nilikuwa darasa la sita shule ya msingi Mbuyuni hapo njia ya kuelekea posta, tulirudishw home kisa nyerere kafa, nilipofika nyumbani nilimkuta mwenye nyumba analia mithili ya mtu aliyebakwa
Ha ha ha ha
 
Nilikuwa njiapanda ya area c dodoma ndipo mzee wa stuli akalitangazia taifa.NDG WANANCHI
 
Ulikuwa wapi?,mimi nilikuwa darasa la pili shule moja maarufu jijini Mwanza, mwalim akapiga kengele akasema tunarudi nyumbani sababu Nyerere kafariki,nilikuwa hata sijui Nyerere ni nani, mimi nilikuwa namjua Ben Mkapa pekee,kurudi nyumbani jioni yake tunakuta Komba tayari ameshafanya yake (Jamaa alikuwa fasta sana) japo Tv tulikuwa tunaangalia kwa jirani.
Nyerere pumzika kwa amani
Mm nilikuwa form 3
 
NILIKUA NAMFUATA MKE WANGU AMANA VIJANA CENTRE ALIKUWA KWENYE SEMINA NIKITOKEA KIBAGU ILI TUKAMUONE SHANGAZI MUHIMBILI ALIPOKUWA AMELAZWA
 
Back
Top Bottom