Kifo cha Mwalimu Nyerere 14/10/1999, ulikuwa wapi?

Kifo cha Mwalimu Nyerere 14/10/1999, ulikuwa wapi?

Mkuu sitakaa nisahau mi nilikuwa ndo niko darasa la saba ila kipindi anatangazwa kafariki tulikuwa migombani tunachuma kahawa na redio tulikuwa nayo tumening'iniza kwenye mkahawa!!tena umenikumbusha dedio ilikuwa aina ya national ile ya batery 4 kubwa[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Radio Dedio [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nilikuwa chumba cha sita, lakini nilikuwa na akili zangu, kwani SHULE yetu ipo karibu na makaazi so niliskia wimbo wa taifa unapigwa redioni mchana kwenye saa sita na ushee hv, nikawaambia marafiki zangu"mbona wimbo unapigwa sahv" mmoja wa marafiki zangu akasema kitu sio bure ndio tukaenda kusikiliza.
 
Siku hiyo tulikuwa tunamzika dada yangu ninayemfuatia hapo nimemaliza darasa la saba,. Ni siku ambayo sitaisahau maishani mwangu
 
Kumbe huku % kubwa ni watoto ?,ushauri wangu ni huu,suala la umri lizingatiwe ili uweze kuwa member wa jf,pls wahusika walifanyie Kali
Dah! Unachosema ni kweli ndugu. Ndiyo maana mara nyingine nimekuwa nikistaajabu mada nyingi msinazokuwa zikichangiwa sana ni zile zinazohusu mambo ya kijinga kama vile ngono, nk. Wakati ule zile za muhimu zinazohusu mambo ya kijamii zikipuuzwa!

Kumbe asilimia 99% ni watoto walio balehe juzi![emoji53]
 
Umeonaeee, sie wakati huyo jamaa anakufa tuwatu wazima kabisa na k tunakula. Nashangaa wengi wanasema lapili mara darasa la tatu, si bora hao walokuwa form 4. Ndo maana tunapojadili maswala ya msingi huku tunakuwa na shida sana kumbe watoto wamejaaa aghhhhhrrrri.

Natania tu bwana watotot msiogope, nyie ndo mnafanya JF isiwe boared, I like you kids.
We like u too bro..
 
Mnaoshangaa watoto,hamjui hii ndo generation mpya imacoverup wakati wale wazamani wakipukututika na kuachia nafasi,
haa sio watoto tena wameshakua wakubwa,waliokuwa la pili,la kwanza sasa wana miaka 24-25,hawa ni watu wazima tu,hata wewe wa miaka 35 ama 40 sasa unaweza kuoa bila tabu.


Mimi kipindi hicho niko dodoma nafuatilia pensheni ya kustaafu,kwakweli tulilia sana
Shikamoo babu
 
Nilikuwa mwaka wa nne mwanzoni enzi hizo panaitwa FoE... Electrical Engineering..

Redio zote no kupiga ndombolo mwezi mzima. Ni nyimbo za maombolezo tu...

ILA HUMU KUNA WATOTO WENGI... ndo maana wengine tunavumiliaga matusi na kashfa nyingi humu
haaaaaa!!shikamoo sasa!!
 
Watu wanasema walikua primary schools wanatokea wengine wanasema kumbe jamii forum imevamiwa na watoto sasa mimi sijui utaniitaje maana sikuwa nimezaliwa [emoji23]
Ata avatar yako ina dhirihisha iloh dogo[emoji102]
 
asante mleta mada maana leo imenifanya nijue kwa nini mda mwingine watu wanajibu viroja kumbe wengi ni chini ya miaka 30
 
Nilikuwa darasa la kwanza Kamunyonge s/m..ile nafika shule mida ya saa 7 siku hyo alhamisi namkuta mwl matete paredi na bendera tayari ikiwa robo tatu ya mlingoti
Yego jaji. Waongelamo maboksi?
 
Nipo zangu kazini na kama miaka miwili hivi baada ya internship
 
Gatete. Mwaka huo mie nilikuwa njagu field force hapo kamunyonge. Mwl Matete namkumbuka. Unamkumbuka yule mzee Mtagalala hapo juu ya shule?
 
Back
Top Bottom