Kifo cha mwanangu kipenzi kimetokana na uzembe

MWANANGU AMEFARIKI AKIWA NA MIAKA 2.5 TAYARI ALIKUWA MKUBWA NAMTUMA NAMFUNDISHA ALIKUWA NA AKILI NA MTOTO MZURI SANA MSIBA UPO CHAMA KARIBUNI TUMPUMZISHE UHAI WAKE UMEDHULUMIWA MUNGU NASHITAKI KWAKO MIMI MASKINI NISIE NA SAUTI
pole sana mkuu, Pole mno. Mungu aipokee roho ya mwanetu Amina.
 
Pole sana kwa kumpoteza mtoto. Japo Imani za dini zinasema kifo ni mapenzi ya Mungu lakini ni uhakika kabisa kuwa vipo vifo vinavyotokea kabla ya wakati

Pamoja na hayo kila linalotokea hapa dunia linakuja kwa ajili ya kutufundisha na kuweka Mazingira bora zaidi ya wakati ujao

Kwa kifo cha mwanao ni vema ukataja jina la hospital husika na ikiwezekana wahudumu waliokupokea na kukaa bila kukupa huduma kwasababu ya mtandao Jambo ambalo ki uhalisia na kiutendaji haitakiwi kuwa hivyo

Kuendelea kuficha identify za wazembe ni sehemu ya kuendelea kuficha maovu na kulea uovu.

R.I.P our child
 
Binafsi naona kuna kitu hakijakaa sawa.... Naona kama unataka kutupiga kamba hivi?

1. Hutuambii mtoto alikuwa anaumwa nini..

2. Hutuambii kaanza kuumwa lini na imekuaje mpaka umauti ukamfika.


Kingine katika vitu ambavyo hospitali huwa wako makini navyo ni watoto na wajawazito.... Ni ngumu sana mtoto kukaa masaa 7 bila kuhudumiwa kama kweli alikuwa amezidiwa..

Hebu leta vithibitisho vya wewe kuhudhuria hospitali, tutumie hata picha ya risiti ya consultation tuu..
 
Hio nilikata mapema sana ili siku lilitokea la kuhitaji uharaka wa huduma basi dogo apatiwe huduma chap hata kama sipo
Hamasisha na marafiki, maana watu tuna uzembe tukiamini hatutazidiwa.

Mi nahamasisha marafiki zangu wakate ili wasijeanza nisumbua na michango ambayo yaepukika
 
Mbona mi sijawahi kutana na hiyo kadhia kwa TotoAfya Kadi?

Kwa watu wazima najua kuna tatizo kutokana na grade ulipo
 
Pole sana mkuu, Sasa hata hospital unashindwa kuitaja hapa mkuu?.
 
Pole sana jamani mwenyezi Mungu akutie nguvu ni hospital gani hiyo Jaman
 
Aisee pole sana, kwani si wangemtibu mtandao ukirudi wanaingiza taarifa za kadi tu

mkuu, we hujui tu ....pengine ni kwa sababu unatumia cash,

watu wa wanaotumia bima huwa wanadharauliwa sana

unaweza ukaenda hsp na netwk ipo lkn ukaambiwa hamna...utakaa hapo mpk mwenyewe uondoke
ni basi tu hatuna pa kusemea
 
Pole sana mkuu.Aliyemleta kwenye mgongo wa Ardhi ndiye aliyemuondoa. Hizi juhudi zetu za kufanikiwa na kutofanikiwa ni juhudi zetu tu ambazo hatuwezi kukataa tamaa kuzipigania. Shukuru kwa hilo, songa mbele.
 
Kama miezi sita iliyopita kuna binamu yangu nilimpeleka hospital age 6 years around saa nane usiku dogo alizidiwa ilikua private hospital eti kufika getini mlinzi anatuzuia kuingia kisa hatuna Barakoa nusura nimpasue jiwe la kichwa. Mpaka kuna watu waliokua na busara zao wakaja kuingilia tukaingia ndani. Mtu anaona mtoto kazidiwa tena ni usiku badala ya kuokoa mtoto yeye anakomaa kufuata protocols.

Pole sana Mkuu
 
Pole sana ndugu, vilio vyetu ni kama vya samaki baharini, unapoteza mpendwa wako kwa uzembe tu wa wauguzi na huna pa kudai haki yako. Pole sana best, Mungu awatie nguvu mvuke salama.
 
Pole Sana! Matokeo ya madaktari wa .com, hawafanyi lolote bila ya kuwepo mtandao. Ungekutana na wa miaka 47, wanaoonekana ni washamba, Kwa kumuangalia, kumshika hapa na pale, mwanao angeokolewa.
Apumzike Kwa Amani!
 
Mkuu pole sana kwa kumpoteza mtoto wako. Siwezi kukuhoji sana ila kwa ninavyofahamu.
1. Zipo dawa za dharura ambazo hutumika kwa wagonjwa then baada ya kutatua dharura mhusika hurudisha hizo dawa ili zitumike kwa wengine wenye dharura.
2. Kama unabima ambayo unauhakika ni active hosptal nyingi hasa za serikali huwa makini sana katika kuwahudumia wateja wa bima za afya( pesa za bima ni sehemu ya mapato na malipo kwa watoa huduma)
3. Uhai wa mtu ni priority ya kwanza kwa kituo cha kutoa huduma za afya hivyo sababu ya mtandao na kumsaidia mtoto haina mashiko.
Nimetaja hayo nikitaka kukueleza kuwa kuna namna zaidi ya mtandao ambayo imepelekea ukapoteza mtoto wako.
Anyway pole sana mkuu ila ingefaa ukaitaja hiyo hospital.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…