Kifo cha mwanangu kipenzi kimetokana na uzembe

Pole sana,Allah akuafanyie wepesi,uwe na subira najua maumivu unayoyapitia
 
ubarikiwe kuna kitu nimeongeza
 
Ni kweli kabisa..
Mimi kijana wangu aligongwa na bodaboda..nikampeleka hospital ya walaya ya ilemela mwanza sikupata msaada wowote..ilikuwa jioni saa 12 daktari akaniambia yupo peke yake..akaniambia nimlaze Kwenye liubao lichafu Sana..mtoto wangu alikaa kwenye kiubao Kama nusu bila huduma yoyote..
Nikapata wazo la kukimbia Bugando..
Kwakweli Bugando nilipata huduma ya kiwango Cha SGR..siwezi kuwasaau wafanyakazi wa Bugando..
Kwanza nilipofika getini na mtoto..wahudumu walimkimbilia mtoto na kuanza huduma..Tena kila hatua naambiwa Nini kinaendelea..
mtoto kawekwa kwenye CT SCAN ndani ya muda mfupi..
Nilichojifunza..ukiwa masikini utafia kwenye vihospitali uchwara vya serikali..Mimi BIMA ilinisaidia Sana..
Kwakweli Kama una pesa ya kutosha/BIMA..nenda hospital za private..
 
Wengi sana wanakufa kwa uzembe na huduma mbovu kwenye hizi hospitali zetu.

Pole sana mkuu.
 
Upo sahihi kabisa hawa watu wa NHIF hawafai kabisa na siendi tena kwa vituko vyao vinachosha. Nilimpeleka NHIF Dodoma mwanangu 4yrs na Bima Toto alisumbuliwa na tape worm, na wanadondoka kabisa kwenye kaptula, eti wanampima damu na majibu hamna kitu, nawaonesha ushahidi ninao kwenye tissue paper. Wakaniudhi warudie damu Sasa utoboaji wao kutafuta mshipa nikagoma, wakaniandikia dawa albendazone, kwenda mtaani kea maDr wa Disp wakanipa dawa ya tape worm amepona,
 
Ubarikiwe hakika Mungu ndiye muweza wa yote,
 
Asante barikiwa sana
 
Ilikuwa hivo walimuwekea dripu tu mda kashalegea kazidiwa
 
Dah, pole sana ndg. Nasikitika sana kwa kweli. Ila kuna watu wameweka emoji za kicheko kwenye huu uzi. Nadhani ni bahati nbaya
 
pole sana alianza kutapika damu nyeusi ! probability ya kusave ilikuwa ndogo mno, ila wangemtibia pengine angesave
 
ningekuwa na pesa usingefariki maana masikini nimeganda na wewe masaa 7 hospitali bila msaada.
Pole sana...

Ungekuwa na hela ungempeleka wapi ambako kuna ma pediatrician saa nane usiku ?
 
Pole sana. Lakini hapo uliposema UZEMBE WA MADAKTARI nadhani umepeleka lawama pasipo. Una uhakika mapokezi wanakaa madaktari? Kada zipo nyingi hospitali. Sawa ee?! Jaribu kuzifahamu sio kuwabebesha mizigo watu wasiohusika.
 
Asante kwa ushauri.

Though uko nje mshike mkono tu.

Was a bad death ever. Ila tumwamini tu Mungu.
 
Huyo mwanao unamlisha nini ndugu mpaka minyoo idondoke kwenye kaptura??au unamlisha viporo??
 
Kuna maana gani ya kuwa na bima halafu tena utembee na mapesa ?
Ni jukumu la bima kuhakikisha mteja anapata huduma bora na kwa wakati ,
Premium service haitakiwi iwe ya kuunga unga
 
Una bahati sana hujakatia watoto bima na hujapata majanga ,
Bima ya mtoto ni 50000 tu , na ina wigo mpana sana wa hospitali kuhudumiwa ,jamaa amepata bahati mbaya tu ya kupoteza mtoto ila servise za bima so mbaya kiiivo kwa sasa
Mwanangu mmoja alipata operation ya koo kuondoa nyama ambazo zilikuwa zinamfanya apumue kwa tabu sana hasa usiku, bili ilikuja laki sita plus, na nilitumia kadi ya bima
 
Pole sana mkuu lakini usiogope kuwaanika ili kuokoa maisha ya wengine.
Niliwahi kuwaanika hospitali moja hapa mjini kidogo wanyimwe tenda ya kuendelea kututibu na kampuni na yule daktari akawajibishwa. Isivyo kawaida baadhi ya wafanyakazi wenzangu walinifata na kunilaumu kwanini nimeharibu kazi za watu bila kujali kama ningekufa siku ile au mwingine angeweza kufanyiwa upuuzi kama ule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…