obrien daniels
Member
- May 4, 2022
- 44
- 61
Hili ndilo najua leo, kuwa ulimpoteza umpendaye! Pole sana.Dah!! Pole sana. Hakuna maumivu makali kwa binadamu kama haya ya kumpoteza mtu umpendaye.
Hata mimi nilimpoteza mke wangu miaka kadhaa iliyopita, kwa uzembe wa hawa jamaa. Natambua maumivu unayopitia. Mwenye Mungu akujalie wepesi katika kipindi hiki unachopitia.
Ofcourse nilikosa kabisa ujasiri wa kutoa taarifa. Alikuwa ni wife material! Uzembe wa kibinadamu ukatokea, akaondoka kirahisi rahisi tu!Hili ndilo najua leo, kuwa ulimpoteza umpendaye! Pole sana.
Mkuu inabidi tu ukubaliane na mitazamo ya wengineIna maana huyo fisi wenu alizuia kifo?
Mkuu pole sana sanaMwanangu aliumwa usiku ghafla tukalazimika kwenda hospitali ya karibu wakasema tumpeleke hospital ya ++++, kufika pale saa 8 usiku wanasema network hakuna hadi irudi wamekuja kumhudumia asubuhi saa 4 mtoto kashalegea anatapika damu nyeusi. Tumemlaza kitandani wakaniagiza mavitu mengi kumbe mtoto amekata roho kwa uzembe wa madaktari.
Naumia sana, mwanangu kachomwa chomwa kateseka kafariki kwenye maumivu makali sana kwa uzembe. Nisamehe mwanangu na ulale salama kama ningekuwa na pesa usingefariki maana masikini nimeganda na wewe masaa 7 hospitali bila msaada.
Kwanini wasingemhudumia mtoto jamani naumia sana mimi jamani
Hiyo itakuwa ni hospitali ya serikali, mara nyingi wanafanya kazi kwa mazoea. Net work ndio hutumika kuunganisha shughuli kwenye hospitali nyingi kubwa, lakini ukikwama hospitali au Dr mwelewa hurudi kwenye analogy ili kuokoa kwanza uhai.Pole sana, ila kwa Tanzania yetu ya leo usipoitaja hiyo hospitali huu uzi utakuwa hauna maana,hii sio kuwachongea wenye hospitali bali itasaidia kuepusha wengine wasije kuwa wahanga wa kilichokutokea...
Acha fix wewe. Nani aandike mtoto fulani atakufa kwa uzembe?Pole kifo kilishaandikwa, Allah akujaze subra, inna lilahi waina ilaihi rajiun.
Kifo hakiandikwi, huo ni utetezi wa watoa huduma wazembe. Kama kimeadikwa hospitali zinajengwa kwa ajili gani? Madaktari wa kawaida miaka sita wako darasani kwa gharama kubwa kwa kusudi gani? Kufa kupo, juhudi za kuokoa vifo ambavyo vinazuilika ndio furaha ya daktari.Pole kifo kilishaandikwa, Allah akujaze subra, inna lilahi waina ilaihi rajiun.
Kwelii we Extrovert,Wewe ni sehemu ya huo uzembe pia. Baba wa mtoto yupo wapi? Hospitali ni moja tu hapo ulipo?
RIP chalii mdogo.
Japo kinadharia hospitali usiku hazifungwi, huduma usiku ni mbovu. Kitengo cha maabara mhudumu usiku mpaka afuatwe nyumbani ikibidi. X- ray ndio kabisa mpaka kesho. Hospitali ngazi ya mkoa utamkuta daktari mmoja usiku, na anaweza kuwa ni intern.Japo ni mipango ya Mungu lakini asilimia kubwa sana za vifo vinavyotokea mahospitali yetu ni sababu ya uzembe na dharau.
Asilimia kubwa ya hospitali hasa za serikali hazina huduma za maana usiku. Ukienda hospitali usiku unakutana na manesi wenye visirani na kama kuna dokta basi kalala fofofo hana hata habari.
Maabara unaambiwa hakuna mtu, mpaka ukija kupata huduma ya maana basi kumekucha na ikiwa ni maradhi ambayo yalihitaji kipimo cha haraka ili kutibiwa yanakuwa yashakumaliza.
Yote kwa yote, Mungu akupe subira katika machungu unayoyapitia. Ikiwa ni faraja yeyote kwako, basi elewa kuwa yupo mahala pazuri zaidi. Pole.
Na wengi hufanya hospitali kuwa guest bubu. Unakuta dokta na nesi wamekumbatiana sehemu huko kupelekea kuwa na visirani pale wanapohudumia wakihisi wamekatishwa starehe zao.Japo kinadharia hospitali usiku hazifungwi, huduma usiku ni mbovu. Kitengo cha maabara mhudumu usiku mpaka afuatwe nyumbani ikibidi. X- ray ndio kabisa mpaka kesho. Hospitali ngazi ya mkoa utamkuta daktari mmoja usiku, na anaweza kuwa ni intern.
Watafanyaje hivyo na mazoea yamewajaa? Mazoea huzaa tabia.Inaelekea ulitumia bima ya afya na kadi inaonesha muda wake haujaisha, kwanini wasiruhusiwe kutia huduma kwanza na mambo ya mtandao yakafuata baadae?
Wewe ni sehemu ya huo uzembe pia. Baba wa mtoto yupo wapi? Hospitali ni moja tu hapo ulipo?
RIP chalii mdogo.
Pole sanaJapo ni mipango ya Mungu lakini asilimia kubwa sana za vifo vinavyotokea mahospitali yetu ni sababu ya uzembe na dharau.
Asilimia kubwa ya hospitali hasa za serikali hazina huduma za maana usiku. Ukienda hospitali usiku unakutana na manesi wenye visirani na kama kuna dokta basi kalala fofofo hana hata habari.
Maabara unaambiwa hakuna mtu, mpaka ukija kupata huduma ya maana basi kumekucha na ikiwa ni maradhi ambayo yalihitaji kipimo cha haraka ili kutibiwa yanakuwa yashakumaliza.
Yote kwa yote, Mungu akupe subira katika machungu unayoyapitia. Ikiwa ni faraja yeyote kwako, basi elewa kuwa kijana wako yupo mahala pazuri zaidi. Pole.
Pole sana,Mungu akupe wepesi ktk hili inauma sana.Kuna siku mdogo wangu aliganyiwa operation badae akaanza vimba usoni akameambia nesi amwite Dr,alijibiwa vibaya sana bahati nzuri alinitaarifu nilipofika sikutaka mengi nilienda moja kwa moja kwa mganga mfawidhi na kumeeleza uozo na kumwambia afatilie na mhusika aliitwa akanikita ofsini kwao,na hakapata huduma.Kumbe wakati mwingine ni kuonesha kuwa una Haki ya huduma na siyo ofa au kuwabembelezaMwanangu aliumwa usiku ghafla tukalazimika kwenda hospitali ya karibu wakasema tumpeleke hospital ya ++++, kufika pale saa 8 usiku wanasema network hakuna hadi irudi wamekuja kumhudumia asubuhi saa 4 mtoto kashalegea anatapika damu nyeusi. Tumemlaza kitandani wakaniagiza mavitu mengi kumbe mtoto amekata roho kwa uzembe wa madaktari.
Naumia sana, mwanangu kachomwa chomwa kateseka kafariki kwenye maumivu makali sana kwa uzembe. Nisamehe mwanangu na ulale salama kama ningekuwa na pesa usingefariki maana masikini nimeganda na wewe masaa 7 hospitali bila msaada.
Kwanini wasingemhudumia mtoto jamani naumia sana mimi jamani