Kifo cha mwanangu kipenzi kimetokana na uzembe

Hospitali za Umma shida sana,nimewahi kupewa dawa mseto bila kupima malaria.
Kuna kipindi nilipeleka wagonjwa wawili Hospitali ya Palestina Sinza,mmoja alikuwa na malaria na mwingine alijeruhiwa na panga.Tukaanza na majeruhi kwanza,tukawapa fom ya polisi(PF3) wakatuambia tusubiri na hapo ni saa 7 usiku.Baadae akaja mmoja akatuambia hamna uzi kwa ajili ya kushona kidonda hivyo hadi madukani.Nikawauliza huu mda ndio inaingia saa 8 ni duka gani lipo wazi,wakajibu usiwe na wasiwasi uzi tunauza humuhumu hospitali.Jamaa akanambia toa sh.elfu 7 tununue uzi pamoja na dawa na gharama za kushona kidonda.
Ilibidi nitoe tu,baada ya hapo nikaanza kuhangaika na mgonjwa wa malaria ila yeye alikuwa na bima.Hadi kufika saa 9 wakamaliza kumshona mgonjwa.
 
Pole sana ila wewe ndo mzembe kwanini muda wote huo umeupoteza pale ungemtoa pale na kumpeleka hospitali nyingine lazima uwe na maaamuzi magumu siku nyingine
 
Pole Sana ndugu,Mungu akutie faraja,mtoto Yuko mbinguni,jikaze tuuu.
Mungu atakupa watoto wengine ,Pole sana
 
Pole sana Mkuu.
 
Ungetoa kitu kidogo Internet ingerudi chapchap!! Pole sana, Mungu ailaze pema roho yake. Watu wanapenda pesa kuliko uhai wa mtu. Haya ndio mambo aliyoyayapiga nyundo JPM.
makampuni ya BIMA wajitathmini upya....

Note this [emoji3578]
 
We waheshimu watu wote usichague wa kumuheshimu. Tatizo linalotukabili wengi ni kutaka kuonekana wema kwa kila mtu hili huzaa unafiki.

Nchi yetu imekwama kwa tabia ya namna hio hio ambayo imestawi katika jamii za watu wengi.
"Nisamehe mwanangu na ulale salama kama ningekuwa na pesa usingefariki maana masikini nimeganda na wewe masaa 7 hospitali bila msaada".


Ona sababu yake hii, we umeifikiriaje.
Mi nimemuelewa saana kwakweli
 
Mhhh! Umeshajiongeza tayal!
Jpm kaacha mfumo wa bima ukiwa hivyo,
Mfumo unatakiwa kubadilika ,ili emergencies ziwe zinatolewa hata kabla ya system ya malipo haijakuwa checked,
Mtu anasubiri system hadi mtoto anafariki kweli ? Wakati huduma ya bima ni pre paid
 
Pole sana mkuu
 
Pole sana mkuu mungu akutie nguvu hao wahudumu wana roho za kishetani pesa na uhai wa mtu hatari sana
 
Pole sana kwa kumpoteza mtoto! Apumzike kwa amani
 
Too bad
 
Nimeumia sana. Pole sana ndugu yangu, Mungu amrehemu mwanetu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…