Kifo cha Rais Nkurunziza kimepunguza kujiamini kwangu

Kifo cha Rais Nkurunziza kimepunguza kujiamini kwangu

Serikali inasema hivyo ila inafanyaje? Umewahi kumuona kiongozi mkubwa kavaa barakoa, si ulisikia sp alivyoambiwa kwa kuvaa barakoa
Vitendo vya viongozi vinaashiria kuwa corona imekwisha na hivyo tahadhari kama za barakoa na kunawa nsi muhimu sana - they dont walk the talk!
Ukivaa barakoa unapingana na anachotaka kuonesha jiwe hivyo utafukuzwa uwaziri wako ndio maana viongozi hawavai Bara lakini Zanzibar wanavaa hata rais mwenyewe. Siasa mbovu za jiwe za kulazimisha mtazipata freshi baada ya uchaguzi, sasa anawabembeleza tuu.
 
Nahisi Kuna mbinu chafu Wakenya
na mabeberu 🐐 🐐 wanajfanyiaa Burundi na soon mbinu hiyo itaingizwa nchini.
Nchini wakenya wamepigwa bao. Corona IPO na inaendelea kuwepo. Tusichekane.
 
Kurunziza kafa kwa ugonjwa wa moyo,Mama yake kafa kwa kisukari,Dada yake anaugua Kansa.Mke alipata Covid na hajafa.Unasemaje hapo?
Ninalo basi ba ndugu mie nashangaa kwa kweli watu wanavyopenda kuisingizia korona
 
Tuseme nini sisi madaktari?
Ripoti ya daktari ndio kila kitu kama wamefariki kwa Corona kwanini wafiche? Mbona mkewe katangazwa kua ana Corona?

Nkuruzinza kafariki kwa mshtuko wa moyo,
Period.
Sasa kwani mimi nimebisha niwashangae nyie mtu akipatwa hata na mafua au alikuwa na ugonjwa wa siku nyingi ikitokea gafla kafariki anaanza kunyooshewa vidole tushukuru Mungu huku Africa mkono wa Bwana ulitenda mema na tusichoke kuomba na kushukuru mauti ilikuwepo toka enzi ya Adamu na Hawa naitaendelsa kuwapo hofu yetu ni kutangulia lakini mwisho wa siku kufa ni faida kuishi ni Kristo
 
Yaani huu ugonjwa unakuwa watu unakuacha mdomo wazi manake huamini kweli fumbo ni kubwa kuliko tunavyoamini
Alihudhuria mpira jumamosi akiwa mzima,,jumapili pia akaonekana mzima kabla hajaugua ghafla na kupelekwa hospital,,jumatatu,,jumanne kafariki,,
Kosa lililofanyika baada ya wife kuugua alitakiwa apime asap kwahiyo kama kulikua na shida ingeonekana kabla tatizo halijawa kubwa,hivi ndivyo waliweza kumwokoa pm wa UK,wangechelewa kidogo nae alikuwa anapotea
 
Kama nilikuwa nikiamini kuwa CORONA hainiwezi maana ninaye Mungu baba, sasa nimeanza kufikiria tofauti. Kumbe lolote linaweza kutokea kwa yeyote. Rais Nkurunziza sijui kafa kwa ugonjwa gani hasa ila naamini Corona haiwezi kupuuzwa kwenye hili. Tuwe makini bado
Nadhani kuna kitu anataka kufunguka lakini umeshindwa na umeamua kupitia kwenye mgongo wa marehemu Nkurunziza.
Funguka kijana.
 
Mch. Gamanywa aliwaponda waumini wake kanisani waliovaa barakoa ,aliwaambia unakuja na barakoa kanisani Mungu ananuka ?

Lakini wao sasa hivi wakiombea waumini hawawagusi tena
REKEBISHWA sio Mtumishi Muadilifu Gamanywa...
Yule alikuwa TAPELI Anayejinasibu NABII MWINGIRA wa EPHATA.
 
Kurunziza kafa kwa ugonjwa wa moyo,Mama yake kafa kwa kisukari,Dada yake anaugua Kansa.Mke alipata Covid na hajafa.Unasemaje hapo?
Hii ajabu. Wote wapatwe magonjwa
yasioambukiza kwa wakati mmoja. Inawezekana ila kwa kuwa mkewe tayari alikuwa na korona,Wenye uwezo wa kuchanganya akili zao na za kuambiwa wanaweza kutuambia nani mkweli. Hasa wanaojua hesabu zilee za probability.
 
Nadhani kuna kitu anataka kufunguka lakini umeshindwa na umeamua kupitia kwenye mgongo wa marehemu Nkurunziza.
Funguka kijana.
Funguka mdau Kama Kuna unachofaham zaidi ya hiki nilichokisema
 
Inategemea mwili wako unareact vipi na hao virus,,kwa wengine virus wanapoingia kwenye cell za damu,ACE2Receptor kunakuwa na inflimation,,ambayo kwa wengine immunity yao inafanya kazi in excess na kutranslate kama cell zinabust,inafanya cytokine ifanya overeaction ya kugandisha damu kunako mishipa ya damu,kitu kinachopelekea cardiac arrest au stroke ama heart attack
Kitaalum ndo tunapata amfifiro
 
Tuseme nini sisi madaktari?
Ripoti ya daktari ndio kila kitu kama wamefariki kwa Corona kwanini wafiche? Mbona mkewe katangazwa kua ana Corona?

Nkuruzinza kafariki kwa mshtuko wa moyo,
Period.
Ni kweli na unaamini kuwa Kuna watu wasiojulikana Tz?
 
Back
Top Bottom