Hii habari inanichanganya. Nakiri kwamba sikuwahi kusikia kabisa habari za mazishi ya pili ya
Ndugu Edward Moringe Sokoine hapo mwaka jana (sijui ni tarehe zip za mwezi upi?). N'nachokumbuka tu ni kwamba Moringe tulimzika katikati ya zizi la ng'ombe kijijini kwao Monduli na zizi likaendelea kutumika kusetiri ng'ombe kama ilivyo desturi yetu. Nakumbuka mengi yalisemwa baada ya kifo cha Moringe; ya kishirikina na ya kimafya kinyume kabisa na
"post mortem report" ya madaktari. Leo ninapopata habari kama hii najiuliza maswali yafuatayo:
- tangu Sokoine afariki tarehe 12 Aprili 1984 hao watoto wake walikuwa wapi?
- Post mortem investigation hufainyika ili kubaini sababu za kifo cha marehemu si kwa malengo ya maelezo na kumbu kumbu tu bali pia ili kuchukua hatua kama kuna ushaidi wa kutosha kwamba kifo kimesababishwa na uzembe au makusudi ya mtu yeyote. uchunguzi huu ukifanyika sasa na ikagundulika kuna mazingira ya kuwa kifo kilisababishwa na makusudi au uzembe wa yeyote itasaida nini iwapo wasabishaji walishakufa miaka mingi?
- Mazingira mazuri zaidi ya kufanya post mortem investigation ni wakatimwili bado mbichi kikemikali. Kwa hali ya kifo hiki cha takribani miaka 29 tangu kitokee na mazingira aliyozikwa (na kuzikwa tena baada ya tetemeko) huo uchunguzi utatumia sayansi ipi?
- Uchunguzi huu unachochewa na nini sasa hivi na una maslahi gani kwa taifa na familia (kwa hao watoto wa marehemu?)