Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Yaani umeelezea kama vile mwanasheria kumbe bogas tu!Vitabu gani vya sheria umefundishwa kuwa ubora wa mwanasheria unasaidia kupata dhamana katika murder case??????????????????????????????????
Kwani wewe hujui kama pasco ni mwanasheria?kwa taarifa yako huyu jamaa ni mwanasheria wa kujitegemea!
Usiwe unakurupuka kwa kukashifu watu pasipo heshima,una 200mil za kumlipa kwa kukashifu?
 

nakubaliana nawe 100% watuambie ukweli
 

Huyu mtoto atakuwa mtata sana anagalia youtube kwenye link hapa chini , mwenyewe anafurahia miaka 18
[h=1]LULU akiongelea maisha yake baada ya MIAKA 18 ndani ya TAKE ONE [/h]LULU akiongelea maisha yake baada ya MIAKA 18 ndani ya TAKE ONE - YouTube
 

kaka ww hujui kama tumbo linatembea na kinyesi? choo lazima aende
 
kasomewa mashitaka leo kwa hisani ya blog ya issa michuzi kama kuna mtu anajua kuweka link saidia


[h=3]BREAKING NYUZZZZZ........Elizabeth Michael a.k.a Lulu apandishwa kizimbani leo kusomewa mashtaka yake kufuatia kuhusika na kifo cha Kanumba[/h] Muigizaji wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba,Bi Elizabeth Michael a.k.a Lulu amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana na kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.



Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko sinza vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.



Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.



Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.



Muigizaji huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.
 
Upendo huwa wakati wa raha tu...palikobakia kila mtu anachunga mzigo wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…