Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

pia wote kabla ya kuzimia vitu kama simu,miwani,chain,hereni na vitu vingine vya thaman mtu alikua anavikusanya na kumkabidhi shosti yake halafu ndio anajifanya anazimia...kumbe full maigizo
 
Taarifa za kintelegensia zinasema ni wassira

Khaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Kama ni huyu sasa SK alikasirika nini????
Si atasinzia kifuani tu hawezi kufanya lolote!!!!!!!!!!!!!!!!
 
hyo nimeipenda wanakomaa na 18 birth certificate yke inaonesha 17,ilibidi adanganye make alikuwa akienda club anajatazwa kuingia,in short mnamponda lulu ila baadh ya watoa hukum wachafu kuliko lulu mh
 
hivi ile filamu ya 'the lost twins' aliyocheza na msichana Lucky Peter (ambaye character wake alipokuwa mdogo alichezwa na LULU) pia ilikuwa ya SK au alishirikishwa tu?

nikikumbuka hiyo movie ya lost twins,lulu alikuwa katoto sana na kanumba alionekana mkaka,ama mbaba,naona kama alikuwa anambaka
 
yeye ramsey kasema hajaamin na hakupenda kuja kuona mwl wa rafik wke kpz acheni fitina.wabongo wanaish kwa hicia km cjui nn,nyie mnaopenda kuzusha mkikaa bila uzushi mnaugua unyakanyo
 
15.jpg


Bw. Michael Edward Kimemeta - Baba Lulu


Baba mzazi wa Muigizaji wa kike wa filami nchini maarufu kama Lulu, ambaye anahusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba, ameibuka na kueleza kushtushwa sana na taarifa za kifo hicho pamoja na habari kuwa bintiye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo nguli na kuwa anahusika na kifo chake.

Baba Lulu, ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimemeta(49) mzaliwa wa Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro, ame mwambia mpekuzi wetu leo huko Moshi kuwa alimtambua Steven Kanumba kama mwalimu wa mtoto wake Lulu,lakini hakuamini masikio yake baada ya kupata taarifa za kifo hicho, huku bintiye, anayedaiwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu, anahusika.


Lulu alifikishwa mahakamani jana April 11, 2012 akikabiriwa na mashtaka ya mauaji ya Marehemu
Steven Kanumba, ikiwa ni siku nne baada ya kifo cha msanii huyo.

Alisema kuwa Elizabeth ama Lulu alizaliwa tarehe April 17,1995 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, na kwamba alimaliza elimu ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Midway mwaka jana na kamba hivi sasa ana umri wa miaka 17.

Bw Kimemeta alisema kuwa ni vyema polisi kuwa makini katika uchunguzi wao kwa kuzingatia kuwa tukio hilo limejenga chuki na uhasama baina ya Lulu na ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wa marehemu Steven Kanumba.

Alisema kuwa kilichomshtusha zaidi ni taarifa za polisi kusema kuwa kulitokea ugomvi kati ya Marehemu Steve Kanumba na Lulu,huku ikitajwa kuwa walikuwa wapenzi.



"Hatukutegemea kama Marehemu Kanumba angeweza kuwa na mahusiano y kimapenzi na binti yetu; kwanza ndiye tuliyekuwa tukimtegemea kwa kiasi kikubwa
katika kuendeleza na kukikuza kipaji alichokuwa nacho Elizabeth", alisema baba mtu.

"Ninaomba Wanasheria na wanaharakati wa haki za kibinadamu kuingilia suala hili na kusaidia katika kupatikana kwa haki dhidi ya shtaka la mauaji linalomkabili binti yangu Elizabeth na pia naomba swala hili lisichukuliwe kishabiki ama kwa hisia bali haki ichukue mkondo wake"alisema.

Alisisitiza kuwa jamii inatakiwa kutambua mazingira ya tukio hilo,ambapo chanzo kinasemekana ni ugomvi uliopelekea tafrani kwa Lulu kutuhumiwa kumsukuma Marehemu Kanumba kwa kile kinachodaiwa kuwa ulikuwa wivu wa kimapepenzi na haiyumkini hakukusidua kumuua hivyo yeye anashangaa bintiye kuhusishwa moja kwa moja na mauaji.

"Ushiriki wa mwanangu kuhusu mambo ya sanaa nilikwishapata wasiwasi na mama yake mzazi alikuwa akiwasiliana na Marehemu Kanumba enzi za uihai wake ambaye alikuwa anamhakikishia usalama wa Lulu na kusema kuwa ataendele kubaki kama mwalimu…..lakini leo nasikia alikuwa ni mpenzi - nilishtushwa" alisema Kimemeta.

Baba Lulu pia ameelezea kusikitishwa kwake kwa kushindwa kuhudhuria mazishi marehemu Steven Kanumba kuhofia usalama wake, na kusema mazingira yatakaporuhusu hata sita kufika nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba na kutoa pole.

Bw Kimemeta amesema kuwa anaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia ya Marehemu Steven Kanumba na kutoa mkono wa pole kwa msiba huo mkubwa ambao haukutarajiwa.


Kasema kuwa Kanumba alikuwa bado ni kijana mdogo aliyeonyesha umahiri
kwenye sanaa na kwamba amecha pengo kwa familia yake na Tanzania kwa ujumla.
 
Ni mapya? Mwalimu kutembea na mwanafunzi ni jambola kawaida. Lakini baba Lulu mbona hajasema kitu juu ya hao wengine ambao binti yake anadaiwa kutemeba nao siku zote hizi?:yell:
 
wakuombee kwanza wewe uliemtamani kabla ya kuleta hii habari
wewe kama mtu mzima unaangaliaje picha za uchi za mtoto mdogo kama lulu kama huna matatizo tena unaelezea kabisa akiwa uchi unapenda kuangalia uchi za wengine??nimesoma kote sijaona watu wakiongelea uchi wa lulu sasa huku ni kutamaniana na pepo hilolishindwe Kwa jinala YESU HATA KABLA AJASHINDA KESI UWE HURU IN JESUS NAME

.
Yesu amekuwa kichaka cha kujificha wahalifu wengi siku hizi. Tatizo halipo kwa hao wahalifu, hapana. Tatizo lipo kwa viongozi wa dini waliosahau kwa makusudi kufunga mlango wa zizi la kondoo. Mbuzi wakatinga ndani kwa wingi na kuligeuza kanisa kuwa pango la biashara za wanyanganyi. Injili iliyoagizwa itolewe bure sasa inauzwa bei mbaya, na wasanii wote waliokuwa katika biashara zao wahehamishia usanii wao kanisani. Wanauza huduma kwa kwenda mbele bila pesa kutinga kwenye account zao hawatii timu kunisani kutumbuiza. Zamani watakatifu walikuwa wanamwimbia Mungu mpaka milango ya magereza inafunguka sasa hivi wasanii wanatumbuiza hadi mnywa kangara na mbege anaburudika aishushapo huku akisikilizia.
.
 
Story yake ina walakini. Kama Kanumba alikuwa akimharibia mtoto wake anakwenda kwa akina Kanumba kufanya nini? Naona kama mhuni fulani.
 
Ni mapya? Mwalimu kutembea na mwanafunzi ni jambola kawaida. Lakini baba Lulu mbona hajasema kitu juu ya hao wengine ambao binti yake anadaiwa kutemeba nao siku zote hizi?:yell:
awakupata bahati ya kufia kifuani mwa lulu huyu aliefia kwake atatusaidia iweje mwalimu kutembea na mwanafunzi wake anashatkiwa nani???
 
Hahaa Ndugu Mwambie huyo anayejifanya anajua kutoa hukumu Mimacho imemtoka Kaa Watch Men wa kwenye Minara. Ndgu we uliangalia hizo Picha za nini kama sio Ufuska huo. Koma kuhukumu wenzio . Hukumu ya haki anatoa Mungu Peke yake..........!
 
Ukinijibu hili utanisaidia

1..kanisa gani linaruhusu kuangalia picha za uchi
2..ukiwa kama pastor unawezaje kutuhakikishia kwamba lulu ana mbegu mbaya na mbegu nzuri ni ipi..nijuavyo mimi mwenye kutoa mbegu ni baba sasa unisaidie lulu amekuwaje na mbegu na anaziifadhi wapi kama mwanamke
3..ni vibaya na mapema kumuita ana mbaya labda ulikuwa unamaanisha hivi kama pastor ombea hakai itendeke else endelea kukata castle light zako kile chumba cha kuhesabia sadaka kama mama yangu rwakatare anavyosema wakati wa kutangaza harusi mwenye neno juu ya ndoaa hii aseme kama hana akae kimya mpaka yesu wa nazareti atakaapokuja nimesema hivi maana naona kila mtu anamtumia yesu wake ..
 
sijui kuhusu kina jeniffer wa uncle jj wako salama!!!
 
naskia Uwoya ndio alishinda,alizimia mara sita..yani alizimia akazinduka akazimia tena akazinduka,akazimia tena akazinduka akazimia tena akazinduka,waliokuwa wanampepea wakachoka nae akapumzika kidogo... baada ya kuona Wema anamkalibia kumfunika akaendelea kuzimia mfululizo..

aisee ipo siku utashtakiwa kwa kosa la mauaji maana nimecheka hadi nikazimia kisha nikawauliza washkaji kwani nimekaribia kufa? wakasema hapana ndo nikaamka. usirudie tena kuweka comment kama hii
 
Back
Top Bottom