Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kanumba AMEKOSEA simtetei kabsaa.Lakini lulu anastahili afungwe japo 5 years iwe funzo kwake,pia kwa wazazi wazembe kama wazazi wa lulu na wasichana wengine wanaorukaruka mabarabarani wakiwa na umri mdogo.HAKIKA endapo lulu ataachiwa watoto wakike wataaribikiwa sana mitaani
 
Kichwa cha habari kimekaa kiudaku sana,hakiendani na habari husika,kwa mara nyingine jitahidi heading yako iendane na habari husika. tunashukuru lakini kwa kutujuza.
 
Mama lulu ana makosa makubwa kwani hakuona mavazi ya mwanae. na kwann mtoto mdogo akapange chumba.
 
nyie mnamwona kanumba tu. Ray je? Ila pia kabinti ni kadogo kweli!
Alikuwa mdogo mwaka aliyopigwa hiyo picha lakini siyo sasa hivi, amekomaa viungo vyote vya uzazi na yeye mwenyewe alishasema yeye sio watoto show tena bali wakubwa show.
 
Tusilaumu sana hili kwani hata ss 2litakiwa tulikemee kama wazazi au walezi na wana jamii kwa ujumla,limetokea na liwe funzo on the way ili lisije sanuka kama hili!
 
Siku hizi nimepunguza kusoma magazeti maana magazeti ya serious yamekua kama ya udaku.mbaya zaidi hata magazeti ya michezo nayo yana headings za wizi.Utakuta mbele kuna bonge la heading,ukifunua ndani unakutana na stori nyingine kabisa alafu ya mistari miwili
 
Kichwa cha habari kimekaa kiudaku sana,hakiendani na habari husika,kwa mara nyingine jitahidi heading yako iendane na habari husika. tunashukuru lakini kwa kutujuza.

Ni kweli kabisa nakuunga mkono
 
Kanumba AMEKOSEA simtetei kabsaa.Lakini lulu anastahili afungwe japo 5 years iwe funzo kwake,pia kwa wazazi wazembe kama wazazi wa lulu na wasichana wengine wanaorukaruka mabarabarani wakiwa na umri mdogo.HAKIKA endapo lulu ataachiwa watoto wakike wataaribikiwa sana mitaani

Una mtoto wa kike wewe? Well, mimi ninao, na ninakwambia kulea watoto wa kike ni challenge kubwa, especially wanaobalehe. Lulu kufungwa miaka mitano haitatoa suluhu kwa matatizo ya kitabia kwa watoto wa kike, ila kukemea watu wazima wanaowarubuni kwa pesa na umaarufu wao inaweza kusaidia.
 
Hawa wazazi hawajui kulea. hivi kweli unaweza kuona habari kama hizi image1. image2 kuhusu mwanao 'under 18' halafu ukanyamaza??
 
Kweli fikra za mtoa hoja ni ndogo sana. Hata kama story umesikia au umesoma sehemu ulipaswa uithaminishe kwa akili yako na ujiridhishe ni significant kuianika kwa great thinkers. Ona sasa unavyoshambuliwa, ungejiuliza tu movie ya Devil Kingdom ina characters wangapi walioshiriki na wangapi wadhurika? Use your logical sense wisely before the public wisely expose your common sense.
 
Haya hayaaaa... Siiiiirii... Imefichukaaa! Eti,kwenye gazeti moja la Makorokocho!
Yule Mwigizaji wa Nigeria Ramsey Noah aliyeshiriki kwenye Filamu ya Kanumba known as Devil Kingdom anahusishwa na Kifo cha Kanumba,Kufungwa kwa Kajala na Lulu.
Ni hivi.. RAMSEY alipokuja bongo ku act movie hiyo alipata chance ya kupiga picha na Kajala..ona sasa Kajala anatumikia kifungo kwa kutakatisha fedha chafu. Lulu naye alipata nafasi ya kupiga naye picha... Ona sasa yupo rock up pia.
Kanumba kaigiza naye...ona sasa amededi. Ina maana hata hao Kajala na Lulu wangeigiza naye huenda tusingekuwa nao mpaka sasa!
Je,RAMSEY tumhusishe na kitu cha tunguli?? Kazi kwenu.

You heard!!! Unaonaaaaaa Utamuuuuuuuuuuuuuu!!!
 
Sitaki kumuhukumu huyu binti bila ushahidi kwani anaonekana kaanza harakati hizi za usanii akiwa na umri mdogo. Katika maonekano yake hapo juu, alitakiwa awe shule anasoma.

Sasa wa kulaumiwa ni nani?

Kwanza kabisa kabla ya kuwalaumu wazazi wake, ingekuwa vizuri tujue je walikuwa na uwezo wa kumsomesha mwanao lakini wakaona bora aende kwenye sanaa katika umri ule kuliko kumpeleka shule? Kama walikuwa hawana uwezo wa kumsomesha mwanao, basi hawastahili lawama. Kama walikuwa wanao uwezo wa kumsomesha lakini wakamruhusu kuacha masomo ili aende kwenye usanii katika umri ule, basi watastahili lawama kwa kuharibikiwa kwa mwanao.
Pili Marehemu Stephen ana mchango mkubwa katika kuharibikiwa kwa huyu binti. Hili halina mjadala. Historia yake inaonyesha alikuwa ni mtu wa kuwachanganya mabinti. Tuliyaona haya kwa Wema na jinsi alivyochanganyikiwa. Bahati nzuri Mungu alimwepusha Wema na matatizo yaliyomkuta huyu binti Lulu. Bila shaka elimu na exposure alivyokuwa navyo Wema vilimsaidia kudhibiti hisia zake, ingawaje kwa taabu sana kama tulivyokuwa tunashuhudia matukio kwenye magazeti.

Lakini dunia hii ya leo, watu wenye hulka kama za Marehemu Stephen ndio wanaofanikiwa katika sanaa ya Filamu. Vijana wanapenda filamu za "kisasa" zenye tamaduni za kimagharibi kwani ndizo zinazoweza kupatikana kirahisi kwenye TV zetu na mitandao na hivyo kuwaathiri vijana wetu. Kawaida, kwenye kila kitu, mtu hufanikiwa kwenye kile kitu ambacho anachoamini. Huwezi kufanikiwa kwenye shughuli yoyote ile kama huna mapenzi nayo. Marehemu alikuwa na mapenzi na mambo ya "kisasa" na aliamini katika hilo. Filamu yake ambayo tunaambiwa ilikuwa jikoni kutoka "The Power of Love" inatabiri kifo chake. Alikuwa ana act kwenye kitu ambacho anakipenda na ndicho kilichomtokea. Haya si mambo mapya. Yaliwakuta mastaa wengi wa Magharibi kama kina Tupac.

Sasa mimi simtetei hata kidogo huyu binti Lulu kwa kitendo alichokifanya. Lakini mazingira niliyoyaeleza hapo juu yanatoa picha ya awali kwamba huyu binti ana nafasi kubwa sana ya kuwa hana hatia (innocent) kwenye sakata hili zima.

Maamuzi yeyote yatakayochukuliwa kwa binti huyu yatakuwa na mwangi (repercusion) mkubwa sana kwenye Jamii. Kwa vyovyote vile haitakuwa busara kufanya kumuhukumu bila mchanganuo yakinifu wa mazingira aliyokuwa nayo na yaliyopelekea kuchukua uamuzi mzito wa kutoa roho ya mtu.

Ni matarajio yangu kwamba vikundi vya kijamii (NGOs) zitajitokeza kufuatilia na kumsaidia huyu binti katika kesi inayomkabili ili haki itendeke badala ya kufuata hisia za watu na wanasiasa ambao mtaji wao ni watu na marehemu amedhihirisha kwamba alikuwa na watu. Sasa ni watu wa aina gani aliyokuwa nao? Bila shaka ni vijana wa kileo ambao wengi wao ndio wapiga kura. Kwa vyovyote vile wanasiasa wataona kwamba marehemu Stephen ni mtaji kwao.

Lakini vilevile tunaona hawa vijana jinsi ambavyo maadili yao yalivyomeguka. Wameonyesha jinsi walivyoathiriwa na maisha ya mastaa wa magharibi (ambapo marehemu Stephen ndio alikuwa kinara wao kwa hapa Tanzania) ambao wengi wao hawaamini mungu kwa dhati kutokana na matendo wanayofanya. Kuvunjwa kwa misalaba kwenye mazishi ya Stephen kwa sababu ya kuwahi kukimbilia kuona mazishi ni dalili moja wapo ya vijana wetu wa leo walivyomeguka kimaadili na kiimani!!!!!!!!!!!!
 
Ur 100% right, she is underage,Kanumba alikuwa anatembea na minor hivyo alikuwa MBAKAJI,najua nawaudhi wengi lkn huo ndio ukweli ambao wengi wanaukwepa kwenye tuhuma hizi

acheni kupayuka jana, juzi na siku za nyuma mlikua mnawataja hao mapedee wenye uzto kuliko kanumba na aliesababisha hayo yote ni lulu kwa ukahaba wake. Waligombana kwa ajili ya cm je alikua anaongea na baba yake akitaka kujua kama bdo yuko tution? Msilete za mkutwa na ngozi ndo mwizi. Ni wangap Tz wanafanya ivo. Huyu kindegaten hakua na shida ya hela bali ni pepo la uzinzi.
Lakucha mbe...
 
Back
Top Bottom