Sio mara moja au mbili alikuwa anaambiwa abadilishe sheria ili kusiwe na mkanganyiko, na sehemu kubwa ilitakiwa iwe ni kwenye katiba haswa rasimu ya Warioba. Ila Magufuli alikuwa hataki mambo ya katiba, maana yeye hakuwa muumini wa sheria wala katiba, bali msaka sifa binafsi. Alikuwa anajua katiba itaondoa sifa ya one man show, na kupeleka nguvu kwenye taasisi, jambo ambalo lingepunguza kupenda kwake sifa. Nasema hivi, Magufuli alikuwa rais mchapakazi, lakini hakuwa rais mzuri wala bora, bali msaka sifa binafsi.