Kifuani nina mzigo wa hasira na kisasi, mgoni wangu kuwa makini

Mama amekupigania sana mpaka hapo ulipofika. Amatokwa na jasho, akamwaga chozi na damu kwa ajili yako halafu uje ujitoe uhai kiboya tu kisa mwanamke asiejielewa?
Sijawaza kujiua hata Mara moja zaidi yakupambana nanhali ya kujiumiza kwa stress
 
Kuna jela mkuu
Utaacha watoto na wewe
 
Amen this is only I can reply
 
Acheni kumbeza mtoa Mada. Anahitaji ushauri mzuri Na kutiwa Moyo. .

Mtoa Mada hauko peke yako. Kati ya wanaume Kumi wenye wake zako Tisa wanapigiwa na mmoja ambae hapigiwi ndoa yake haijafikisha miezi mitatu...
 
Nipe dawa yaku kubali defeat
 
Kinachonisumbua Ni hi Hali ya uchungu moyoni mi natafuta hata dawa ninywe niwe na amani naambiwa hamna sijui Nani wakinisaidia
Dawa pekee ni MUDA tuu jipe muda jipe mudaa maumivu lazima tupitie na hakuna maumivu yana dumu milele.Jipoge kifuani sema hili nalo litapita ila litachukua tu muda.
Mwakani tu muda kama huu hutakua na huo uchungu.Zaidi utakua unakumbuka na kujicheka kwanini hata uliumia kiasi hicho.
 
Mi niko tofaut na washaur wengi hapo.

Kwanza vipi hicho kisasi chako ulichopanga kina madhara yoyote kwako?? Kama hakuna basi go on mkuu, iridhishe nafsi yako upunguze maumivu.

Ila kama kinahusu kwenda jela na watoto kuteseka basi achana nacho mkuu tafuta namna nyingine tu ya kuachana na mkeo uendelee na maisha yako bila kumfatilia.
 
Kisasi chochote unashauriwa kuchimba makaburi mawili.
Lako na la unayempangia kisasj hicho.
 
Tuliza hasira usije ukaishia jera kwa kulipiza kisasi.watoto bado wanakutegemea hawana hatia yeyote.Hebu jaribu kusamehe na kusahau Kama ni mke utampata mwingine aliye mwema kwako ambaye atakuwa tayari kuyafuta machozi yako.Watafute watumishi wa Mungu waaminifu wanaomwabudu Mungu kwa roho na kweli wakuombee na kukushauri.Maana kengere ya hatari imeshalia ndani ya moyo wako.Jifunze kuhendo presha maisha yamejaa presha na misuguano Kuna baadhi ya wanadamu wapo kwa ajili ya kuwavuruga wengine.
NUKUU "wa Kwanza kuomba msamaha siku zote ni mwerevu,wa Kwanza kusamehe ni mwenye nguvu,na wa Kwanza kusahau ni mwenye furaha.Ebu wapuuzie tu,Akili zako za kutoa maamuzi zinapofika mwisho Muombe Mungu akupe hekima itokaye kwake.maana ni ngumu kukubali unaona kisasi ndio solution,lakini utakapofanya kisasi utawaumiza wasio na hatia kumbuka nyuma yako Kuna familia,ndugu,jamaa na marafiki bado wanakutegemea.[emoji3578][emoji848][emoji1241]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…