Kigamboni: Eneo lenye watu Wapole, Wavumilivu na Wanaonewa zaidi na Serikali yao

Pale Kuna usafiri wa kivuko Cha MV KAZI chini ya TEMESA, ambao ni 200 kwa safari moja,

Huku kukiwa na mzabuni kwa huduma ya premium ambaye ni Azam marine akitoa huduma ya kusafirisha abiria kati ya kivukoni na Kigamboni kwa Tzs 500 per safari...
 
Babu kumbe upo kigambn hii hii, ?
 
Ila kuishi kigas inahitaji utayari, au laa uwe middle class income, vinginevyo ni mateso.
Kunae mate alikua anaishi kule, nlikua napata wakati mgumu kumtembelea, zile heka heka za ferry, mara ndani ya panton usumbufu, nlikua nachoka hatarii.

Maji sasa, chumvi tupu, iwe kisima au bomba, yaan shida kabisaa. Aaah nkamshauri ahame, na kweli akahama, now yuko kimara, full kula life.
 
Kimara napo si shida maji, usafiri,kama una gari foleni,wakat wa mvua njiaaa tope +mashimo au

Ova
 
Huko si anakaa mwandishi wa vitabu vya ujasusi vipi ameshindwa kuwasaidia amjirani?
 
Poleni sana
 
Wakati nasoma hayo maeneo kuna siku mwizi aliiba simu ya mtu watu walivyoanza kumkimbiza akakimbia kuingia baharini. Watu wakawa wanamsubiri huku upande wa Posta.

Raia walivyoona hana dalili ya kutoka wakaanza kurusha mawe, jamaa akasogea mbali zaidi.

Raia wakakodi mtumbwi wakaanza kumfuata. Yule mwana alikua anaelea huku kanyanyua mkono mmoja simu isilowe ila alivyoona wanamfuata na mtumbwi akaachia simu.

Ile siku watu walikua wamevurugwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…