Kigoma: Mganga amuua Mteja aliyetaka kuzindika Fedha za Biashara Tsh milioni 9

Kigoma: Mganga amuua Mteja aliyetaka kuzindika Fedha za Biashara Tsh milioni 9

Umetafuta milioni 9 kwa nguvu zako Mungu akakubariki

unakwenda kwa mganga akazindike badala ya kuendelesa biashara yako na kumwomba Mungu kwa kutumia jitihada zilezile za milion 9

lakini pia Kutoa uhai wa mtu kwa sababu ya milioni 9 ni ushetani
 
Tamaaa mbele mauti nyuma.
kwa nini utegemee uganga na ushirikina ili utajirike?!
Mtegemee Mungu kwa kila Jambo.

Imani za kishirikina zinawatesa sana watanzania walio wengi, kila jambo wanalo lifanya lazima ushirikina uhusike!
1. Sehemu za Biashara
2 . makazini
3. maofisini
4. vyeo

n.k,
Wewe ndiye mshirikina namba moja.Ndiye wewe unayefurahia mateso ya MBOWE kisa unalipwa vipande vya fedha na CCM halafu siku ya Jumamosi kwenye kanisa la SDA unaenda kuabudu au kufanya ushirikina kanisani.Mafarisayo hawa kuwa tofauti na washirikina.Wewe ni mshirikina ,wewe ni mfarisayo
 
Ukifuatilia kwa kina utagundua chain ya damu, inaondoka na kila anaejitahd kuimiki

, jasho la mtu haliliwi bure,

tamaa mbele mauti nyuma.
 
Daah huyu sister namfaham anaitwa Lidya. Alikua anasaloon yake pale Kasulu karibu na stend ya mabus. Kipindi nikiwa nafanya kazi pande hizo za Kasulu nlikua nikipita karibu na saloon yake tunasalimiana fresh tuu ila kumbe ndo mbanga zake hizi ase daah yani siamini kabisa ase nikikumbuka jinsi alivyokua na ule muonekano wake. Ila mambo ni mengi sana nyuma ya Pazia. Rest In Peace Lidya
 
Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma linawashikilia watu wawili akiwemo dereva wa pikipiki na mganga wa kienyeji kwa tuhuma za kumuua na kisha kumfukia mwanamke aliyekuwa ameenda kuzindika fedha za biashara kiasi cha shilingi milioni 9.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo katika wilaya ya Kasulu na kukamatwa kwa mganga huyo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP James Manyama, amesema baada ya kutekeleza mauaji hayo walichimba shimo la kumfukia kisha kuchukua fedha zake ambazo katika upekuzi jeshi la polisi walizikamata nyumbani kwa mganga.


EATV
Watu bado hawataki amini! Kama mganga yuko vizuri basi hana sababu awe
Maskini, afeli darasani, barabara ziwe mbovu, apande meli boti au ndege nk nk.
Ila tulivyo vichwa ngumu bado hatujielewi wala kujitambuwa. Wacha watuuwe tu na upumbavu na ujinga wetu
 
A very good reasoning! Umepata milioni 9, Sasa unatafuta nguvu zipi badala ya kuendelea na nguvu hizo zilizokupa milioni Tisa?All in all RIP Mama milioni 9
Hujui alikuwa anatafuta nguvu ipi? Kawaulize wakinga
 
Masikini mama wa watu,,hofu ya chuma ulete imemponza.

Chuma ulete ipo ndg zng tuchukuwe hatua.
 
Back
Top Bottom