Kigoma mjini kuna fursa za maisha kweli? Naiona Kasulu ikiipita kigoma mjini

Kigoma mjini kuna fursa za maisha kweli? Naiona Kasulu ikiipita kigoma mjini

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1,842
Reaction score
6,087
Hivi inakuaje mkoa uliozungukwa na Congo na Burundi kuwa chini vile? Singida wasemaje?

Nilipata fursa ya kutembelea mji wa Kigoma wiki iliyopita nikaanza na Nyakanazi, Kibondo, Kasulu, Manyovu na Kigoma mjini.

Kuanzia kibondo mpaka kasulu ni vumbi la kutosha na kuna Kilometer Nyingi saana, nilivyofika kasulu nikapata muda wa kutulia kidogo, aisee hapa pamechangamka saana ninatabiri miaka 10 inayokuja, kasulu patachangia pato kubwa kulio Kigoma mjini, itakua sawa sawa na kahama vs shinyanga mjini au katoro vs geita mjini.

Nikashuka Kigoma mjini, aisee huu mkoa ni mgumu sana vitu bei ziko juu, kisingizio ni umbali kutoka wanapochukulia unajiuliza kwanini kasulu vitu ni bei nzuri?..

Kulikua kuna soko wanalitegemeaa linaitwa Mwanga wamevunja wafanyabiashara wegawanyika wengine wapo stand na wengine wapo barabarani Kama unaelekea hospital ya mkoa,

Nikakaa sehemu moja kufanya utafiti, aisee mtu anaweza Kukaa siku nzima bila kuuza biashara yaaani siku nzima amepigwa doro tu.

Ninaona miaka ijayo hata kibondo panaweza kuja vizuri kuliko mjini.

Niwaulize wakazi wa huko kigoma ukiachana na sabuni za mawese, vitenge kuna fursa kwa mkoa wa Kigoma?
 
Kigoma ni mji mzuri sana uliotulia ingawa ukuaji wake sio wa kasi sana.. ila ni moja kati ya miji yenye hali nzuri sana ya hewa.

Kasulu inakimbia kibishara nadhani kwakuwa na uwepo wa kambi za wakimbizi kama nyarugusu ambapo mashirika mengi sana ya kimataifa yapo huko..hii imefanya kasulu kukua kibiashara.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hakika Mkuu, Kila Mwezi lazima niwe mkoa wa Kigoma ila naanzia Kasulu 2 week halafu naenda Kigoma mjini 2day naondoka zangu.

Kwa uzoefu wangu huo ni kweli kabisa mkuu Kasulu ina mzunguko wa kibiashara sana tofauti na Kigoma mjini.

Ila Kuna Frusa nyingi sana ndani ya mkoa wa Kigoma kwa ujumla.
 
Kigoma ni kwa makamu.

Naye naona ana vinasaba vya Mwalimu Nyerere, kwamba Tanzania ni ndugu.

Aangalie asije kutuachia udongo mwekundu barabarani badala ya lami.

Asipambane kuruka hewani tu, historia itamhukumu kesho kama ben.

Achukue mifano ya akina pesambili ambao walipambania mikoa yao.

Nategemea kutembelea Kigoma 🤣🤣
 
Kigoma ni mji mzuri sana uliotulia ingawa ukuaji wake sio wa kasi sana..ila ni moja kati ya miji yenye hali nzuri sana ya hewa.

Kasulu inakimbia kibishara nadhani kwakuwa na uwepo wa kambi za wakimbizi kama nyarugusu ambapo mashirika mengi sana ya kimataifa yapo huko..hii imefanya kasulu kukua kibiashara.

#MaendeleoHayanaChama
Umeongea ukweli kabisa hapo nimeelewa, kambi za wakimbizi zimechochea ukuaji wa kasi wa kasulu
 
Hakika Mkuu, Kila Mwezi lazima niwe mkoa wa Kigoma ila naanzia Kasulu 2week alafu naenda Kigoma mjini 2day naondoka zangu.

Kwa uzoefu wangu uwo ni kweli kabisa mkuu Kasulu ina mzunguko wa kibiashara sana tofauti na Kigoma mjini.

Ila Kuna Frusa nyingi sana ndani ya mkoa wa Kigoma kwa ujumla.
Ndio nilitaka nizijue Mkuu, maana nimezunguka sijaona kabisa Kama kuna pesa
 
Kigoma ni kwa makamu.

Naye naona ana vinasaba vya Mwalimu Nyerere, kwamba Tanzania ni ndugu.

Aangalie asije kutuachia udongo mwekundu barabarani badala ya lami.

Asipambane kuruka hewani tu, historia itamhukumu kesho kama ben.

Achukue mifano ya akina pesambili ambao walipambania mikoa yao.

Nategemea kutembelea Kigoma 🤣🤣
Miaka zaidi ya 60 ya uhuru lakini hakuna lami kibondo to Kasulu na ni parefu haswaa, unaanza kupachukia Kigoma hata kabla ya kufika.
 
Hakika Mkuu, Kila Mwezi lazima niwe mkoa wa Kigoma ila naanzia Kasulu 2week alafu naenda Kigoma mjini 2day naondoka zangu.

Kwa uzoefu wangu uwo ni kweli kabisa mkuu Kasulu ina mzunguko wa kibiashara sana tofauti na Kigoma mjini.

Ila Kuna Frusa nyingi sana ndani ya mkoa wa Kigoma kwa ujumla.
Hebu tushirikishane hizo fursa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kigoma ni kwa makamu.

Naye naona ana vinasaba vya Mwalimu Nyerere, kwamba Tanzania ni ndugu.

Aangalie asije kutuachia udongo mwekundu barabarani badala ya lami.

Asipambane kuruka hewani tu, historia itamhukumu kesho kama ben.

Achukue mifano ya akina pesambili ambao walipambania mikoa yao.

Nategemea kutembelea Kigoma 🤣🤣
Karibu uje ukule Migebuka na mawese!
 
Back
Top Bottom