TheCrocodile
JF-Expert Member
- May 31, 2021
- 1,199
- 3,307
Muhtasari:
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama ya Wilaya ya Kigoma, Eva Mushi amesema mahakamani hiyo imemtia hatiani baada ya kujiridhisha pasipo na shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.
Habari Kamili:
Mahakama ya Wilaya ya Kigoma imemhukumu Ofisa Ustawi wa Jamii, Frank Mabuga kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka mtoto wa umri wa miaka 13.
Akitoa hukumu hiyo leo Machi 20, 2023 Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Eva Mushi amesema mahakama hiyo imemtia hatiani baada ya kujiridhisha pasipo na shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.
Shauri hilo lenye namba 43/2022 lilitajwa kwa mara ya kwanza Februari 22, 2022 ambapo alikuwa akituhumiwa kumbaka mara mbili mtoto huyo kwa siku moja katika nyumba ya kulala wageni ya Ishimwe iliyopo Manispaa ya Kigoma ujiji.
“Awali kesi hiyo ilisomwa kwa mara ya kwanza Februari 22, 2022 mbele ya hakimu Venance Mwakitalu wa Wilaya ya Kigoma ambapo mshtakiwa alikana mashitaka,” amesema.
Kesi hiyo iliyosomwa katika chumba cha siri, Hakimu Mushi amesema mtuhumiwa huyo alitiwa hatiani kwa mujibu wa sheria namba 130 (1) (2) (e) na kifungu namba 131 (1) cha kanuni ya adhabu namba 16 ya mwaka 2019 kama ilivyorekebishwa mwaka 2022.
Hakimu Mushi amesema katika kesi hiyo walikuwa na vielelezo viwili Polisi fomu namba tatu (PF3), na ramani ya eneo la tukio ambapo mashahidi sita wa upande wa mashataka walitoa ushahidi wao mahakamani hapo.
Awali mshtakiwa huyo kupitia wakili wake Ignatus Rweyemamu aliiomba mahakamani hiyo kumpunguzia adhabu kutokana na kuwa na mtoto mdogo lakini mzazi mwenzake kuwa na ujauzito.
Akizungumza baada ya hukumu hiyo wakili upande wa Serikali, Happiness Mayunga amesema adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa sheria kwamba mtoto akifanyiwa kitendo kama hicho anatakiwa kuhukumiwa miaka 30 jela.
“Sisi kwetu ina tafsiri kuwa haki imetendeka na kwamba mtuhumiwa alipewa dhamana na kama ofisa ustawi alikuwa na dhamana ya kulinda haki za watoto lakini alikwenda kinyume cha taratibu,” amesema wakili Mayunga.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi la Jumatatu, Machi 20.