Kigoma: Ofisa Ustawi wa Jamii jela miaka 30 kwa ubakaji

Kigoma: Ofisa Ustawi wa Jamii jela miaka 30 kwa ubakaji

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,199
Reaction score
3,307
Muhtasari:
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama ya Wilaya ya Kigoma, Eva Mushi amesema mahakamani hiyo imemtia hatiani baada ya kujiridhisha pasipo na shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Habari Kamili:
Mahakama ya Wilaya ya Kigoma imemhukumu Ofisa Ustawi wa Jamii, Frank Mabuga kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka mtoto wa umri wa miaka 13.

Akitoa hukumu hiyo leo Machi 20, 2023 Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Eva Mushi amesema mahakama hiyo imemtia hatiani baada ya kujiridhisha pasipo na shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Shauri hilo lenye namba 43/2022 lilitajwa kwa mara ya kwanza Februari 22, 2022 ambapo alikuwa akituhumiwa kumbaka mara mbili mtoto huyo kwa siku moja katika nyumba ya kulala wageni ya Ishimwe iliyopo Manispaa ya Kigoma ujiji.

“Awali kesi hiyo ilisomwa kwa mara ya kwanza Februari 22, 2022 mbele ya hakimu Venance Mwakitalu wa Wilaya ya Kigoma ambapo mshtakiwa alikana mashitaka,” amesema.

Kesi hiyo iliyosomwa katika chumba cha siri, Hakimu Mushi amesema mtuhumiwa huyo alitiwa hatiani kwa mujibu wa sheria namba 130 (1) (2) (e) na kifungu namba 131 (1) cha kanuni ya adhabu namba 16 ya mwaka 2019 kama ilivyorekebishwa mwaka 2022.

Hakimu Mushi amesema katika kesi hiyo walikuwa na vielelezo viwili Polisi fomu namba tatu (PF3), na ramani ya eneo la tukio ambapo mashahidi sita wa upande wa mashataka walitoa ushahidi wao mahakamani hapo.

Awali mshtakiwa huyo kupitia wakili wake Ignatus Rweyemamu aliiomba mahakamani hiyo kumpunguzia adhabu kutokana na kuwa na mtoto mdogo lakini mzazi mwenzake kuwa na ujauzito.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo wakili upande wa Serikali, Happiness Mayunga amesema adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa sheria kwamba mtoto akifanyiwa kitendo kama hicho anatakiwa kuhukumiwa miaka 30 jela.

“Sisi kwetu ina tafsiri kuwa haki imetendeka na kwamba mtuhumiwa alipewa dhamana na kama ofisa ustawi alikuwa na dhamana ya kulinda haki za watoto lakini alikwenda kinyume cha taratibu,” amesema wakili Mayunga.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi la Jumatatu, Machi 20.
 
Wahudumu wa guest hawakuona kuwaa huyo Ofisa yuko na binti mdogo?? Huyu binti alifikajee Guest??
Hii case ichunguzwe upyaaa, vitoto vidogo viache umalayaaa.
Vitoto vidogo VIACHE umalaya? Sio kwamba vilindwe against huu ushenzi mkuu? Duuuhh, umetumia maneno makali wakati dogo aliebakwa ni miaka 13 tuu. Labda ungesema hiyo gesti ichunguzwe na hata kuchukuliwa hatua kali.
 
Kuna kibabu Huku juzi kimepigwa miaka 30, kwanza kibabu chenyewe kilikua na ngoma.

Alafu kikawa kina mbaka mtoto wa Watu yupo Darasa Tano, kilikua kumbe kinambaka Kwa muda mrefu, Huku kikiwa kinamoa Hela yakula shule Kila siku.

Kimemuachia na ugonjwa, chenyewe kimefungwa

Mambo mengine, Hawa Watu wawe wanauliwa Moja Kwa Moja Ili liwe funzo !!.
 
Vitoto vidogo VIACHE umalaya? Sio kwamba vilindwe against huu ushenzi mkuu? Duuuhh, umetumia maneno makali wakati dogo aliebakwa ni miaka 13 tuu. Labda ungesema hiyo gesti ichunguzwe na hata kuchukuliwa hatua kali.
Hata kama ni vimalaya,kikienda kushtaki au ukakamatwa nacho hiyo inasomeka kama umebaka, hata kama alikukubalia inasomeka kuwa ulimdanganya,akili bado ni ya kitoto.....
 
Muhtasari:
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama ya Wilaya ya Kigoma, Eva Mushi amesema mahakamani hiyo imemtia hatiani baada ya kujiridhisha pasipo na shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Habari Kamili:
Mahakama ya Wilaya ya Kigoma imemhukumu Ofisa Ustawi wa Jamii, Frank Mabuga kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka mtoto wa umri wa miaka 13.

Akitoa hukumu hiyo leo Machi 20, 2023 Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Eva Mushi amesema mahakamani hiyo imemtia hatiani baada ya kujiridhisha pasipo na shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Shauri hilo lenye namba 43/2022 lilitajwa kwa mara ya kwanza Februari 22, 2022 ambapo alikuwa akituhumiwa kumbaka mara mbili mtoto huyo kwa siku moja katika nyumba ya kulala wageni ya Ishimwe iliyopo Manispaa ya Kigoma ujiji.

“Awali kesi hiyo ilisomwa kwa mara ya kwanza Februari 22, 2022 mbele ya hakimu Venance Mwakitalu wa Wilaya ya Kigoma ambapo mshtakiwa alikana mashitaka,” amesema.

Kesi hiyo iliyosomwa katika chumba cha siri, Hakimu Mushi amesema mtuhumiwa huyo alitiwa hatiani kwa mujibu wa sheria namba 130 (1) (2) (e) na kifungu namba 131 (1) cha kanuni ya adhabu namba 16 ya mwaka 2019 kama ilivyorekebishwa mwaka 2022.

Hakimu Mushi amesema katika kesi hiyo walikuwa na vielelezo viwili Polisi fomu namba tatu (PF3), na ramani ya eneo la tukio ambapo washahidi sita wa upande wa mashataka walitoa ushahidi wao mahakamani hapo.

Awali mshtakiwa huyo kupitia wakili wake Ignatus Rweyemamu aliiomba mahakamani hiyo kumpunguzia adhabu kutokana na kuwa na mtoto mdogo lakini mzazi mwezake kuwa na ujauzito.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo wakili upande wa Serikali, Happiness Mayunga amesema adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa sheria kwamba mtoto akifanyiwa kitendo kama hicho anatakiwa kuhukumiwa miaka 30 jela.

“Sisi kwetu ina tafsiri kuwa haki imetendeka na kwamba mtuhumiwa alipewa dhamana na kama ofisa ustawi alikuwa na dhamana ya kulinda haki za watoto lakini alikwenda kinyume cha taratibu,” amesema wakili Mayunga.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi la Jumatatu, Machi 30.
Jaribu mara nyingine kufanya proof reading huwezi kuandika Mahakamani hiyo bali ilitakiwa iandikwe Mahakama hiyo laikina neno washahidi lilitakiwa lisomeke mashahidi
 
Nani mlinzi wa watoto wetu, kila mahali hapako salama.

Adhabu ziwe kali zaidi ili kupunguza haya matukio.
 
Jaribu mara nyingine kufanya proof reading huwezi kuandika Mahakamani hiyo bali ilitakiwa iandikwe Mahakama hiyo laikina neno washahidi lilitakiwa lisomeke mashahidi
Asante sana kwa ushauri
 
Ila wakati mwingine kushindwa kudhibiti tamaa za mwili ndiyo kuja kupata aibu kama hizi pamoja na kuharibika kwa future zako.

Hata kama umewaka tamaa, ndiyo ubake mtoto mdogo, miaka 13?

Ameshindwa kwenda kuokota hata wa elfu 15, au huko Kigoma hakuna?

Kama alishindwa kabisa si kuna mafuta, angejilipua tu kimoja alale zake.

Mungu atupe ufahamu Wanaume 🙏
 
Daah. Jela sio mchezo. Kwa bahati mbaya au kwa makusudi, siku nitakayopokea hukumu inayozidi miezi 12 ya kukaa 'boarding' katika uso wa Dunia, ndio siku ntakayojipeleka Mbinguni mwenyewe bila kuitwa'.
Haya mambo yasikie kwa mwingine tu, ni magumu balaa.
 
Kigoma vitoto vidogo havisomi shule, ukikutana nacho utazani kimemaliza form 4 , na watu wengi tu unakuta wana mahusiano nako..

Huyu jamaa kaangukiwa na jumba bovu

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Kumaliza form 4 ndo certificate ya kuliwa? Mtoto wa miaka 13 kwamba kwa macho unaweza hisi analika? Halafu mtoto wa miaka 13 awe ameshamaliza form 4??
 
Vitoto vidogo VIACHE umalaya? Sio kwamba vilindwe against huu ushenzi mkuu? Duuuhh, umetumia maneno makali wakati dogo aliebakwa ni miaka 13 tuu. Labda ungesema hiyo gesti ichunguzwe na hata kuchukuliwa hatua kali.
Unadhani huyo kakosea !!! , Hajakosea kabisa, kigoma ujiji ndoa za utotoni nyingi mno, vitoto vinajiuza, ukute jamaa hapo alikuwa hafanyi nako ngono peke yake na kalimpanga kamemaliza form 4

Kwa akili ya kawaida, kweli mtu anaweza kwenda lodge na mtoto wa miaka 13 ? , Huyo alieetoa ushauri vitoto viache umalaya pia yupo sahihi, havitaki shule vinaolewa, Kigoma ni kama pwani kila siku harusi

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom