#COVID19 Kigoma: Wazazi wavamia shule wakidhani watoto wanachomwa chanjo ya COVID-19

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1628677959670.png

Picha: Baadhi ya Wazazi wakiwa katika Shule ya Msingi Imanga

Wazazi wa watoto wanaosoma Shule ya Msingi Imanga katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wamezuka shuleni hapo kwa madai ya kuhoji sababu za wanafunzi kupewa chanjo dhidi ya corona bila kupewa taarifa.

Hata hivyo, Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Carlos Mabula amesema leo Jumatano Agosti 11 kuwa wazazi hao waliandamana na kufika shuleni hapo huku wakiwa na hasira ya kudhani ugeni uliofika shuleni hapo ni kwa ajili ya kuchoma chanjo wanafunzi wa shule hiyo.

"Nilitembelewa na wageni ambao ni watalaamu kutoka Tari (Taasisi ya Kilimo Tanzania) waliofika shuleni kwenye shamba la michikichi ili kujionea hali halisi ya shamba hilo. Hali hiyo ilisababisha mtafaruku uliolazimisha walimu kuanza kuwatuliza wazazi na kutoa elimu ya chanjo ya virusi vya corona.” amesema Mabula.

Awali, shuleni hapo yalifika magari mawili ya watafiti kutoka Tari kuangalia maendeleo ya shamba la michikichi lenye mbegu bora aina ya Tenera iliyofanyiwa utafiti na Tari-Kihinga.

Mmoja wa wazazi hao, Fikiri Waziri amesema kwa kuwa chanjo ni hiari, walimu hawawapi nafasi ya kupata elimu itokananyo na chanjo.

Amesema kitendo cha magari kufika shuleni hapo kimewasababisha wanafunzi kukimbia kurejea nyumbani kuogopa kuchomwa chanjo.

Mwananchi
 
Nasisitiza nyie watu wa taasisi mnaoenda vijijini mnaanza kujivinzari bila kutoa taarifa kamili kwa uongozi mtachomwa moto sana,kuna taharuki ya mambo mengi sana huko vijijini ikiwemo hili la Covid, ugomvi wa ardhi nk
 
Yooh! Pamoja na jitihada zote hizi zinavyofanywa chanjo ikubalike bado tu hao wananchi hawaelewi? Kama lipo fungu la fedha kutosha kuhamasisha chanjo hiyo ikubaliwe na wananchi kwa wingi litolewe tu kampeni ianza mara moja ili wananchi waache kuogopa hiyo chanjo
 
Itabidi wahamasishaji waambatane na kikosi cha polisi ili kutoa ulinzi la sivyo........ohooo! mi simo.
 
View attachment 1888220
Picha: Baadhi ya Wazazi wakiwa katika Shule ya Msingi Imanga

Wazazi wa watoto wanaosoma Shule ya Msingi Imanga katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wamezuka shuleni hapo kwa madai ya kuhoji sababu za wanafunzi kupewa chanjo dhidi ya corona bila kupewa taarifa.

Hata hivyo, Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Carlos Mabula amesema leo Jumatano Agosti 11 kuwa wazazi hao waliandamana na kufika shuleni hapo huku wakiwa na hasira ya kudhani ugeni uliofika shuleni hapo ni kwa ajili ya kuchoma chanjo wanafunzi wa shule hiyo.

"Nilitembelewa na wageni ambao ni watalaamu kutoka Tari (Taasisi ya Kilimo Tanzania) waliofika shuleni kwenye shamba la michikichi ili kujionea hali halisi ya shamba hilo. Hali hiyo ilisababisha mtafaruku uliolazimisha walimu kuanza kuwatuliza wazazi na kutoa elimu ya chanjo ya virusi vya corona.” amesema Mabula.

Awali, shuleni hapo yalifika magari mawili ya watafiti kutoka Tari kuangalia maendeleo ya shamba la michikichi lenye mbegu bora aina ya Tenera iliyofanyiwa utafiti na Tari-Kihinga.

Mmoja wa wazazi hao, Fikiri Waziri amesema kwa kuwa chanjo ni hiari, walimu hawawapi nafasi ya kupata elimu itokananyo na chanjo.

Amesema kitendo cha magari kufika shuleni hapo kimewasababisha wanafunzi kukimbia kurejea nyumbani kuogopa kuchomwa chanjo.

Mwananchi
Hii situation ndio ilinikuta last week hadi nikaandika ile thread. Yaani kule wako so ignorant. Mshana Jr
 
kama fikira za mwendazake zilipenya sana masikioni na akilini mwa watu, kwa nini alitumia polisi, tiss na walimu kumteua urais, wabunge na madiwani?

je, tiss walikuwa wanampa matangopoli ya kumtia hofu?
 
Back
Top Bottom