#COVID19 Kigoma: Wazazi wavamia shule wakidhani watoto wanachomwa chanjo ya COVID-19

Elimu jamani, elimu jamani!
Elimu muhimu jamani
Sasa hao wazazi waambie njooni shuleni kufuatilua maendeleo ya watoto, nina hakika hata mmoja hataenda
Unakuta hajawahi kukanyaga hapo shuleni hadi mtoto kafika darasa la saba ila leo gafla anatokea anasema amekuja kudhibiti watoto wasichomwe chanjo wazungu wanataka kuwauwa.
 
Sumu ya mzazi kuhusu chanjo +uoga wa mtoto kuchomwa sindano hapa somo limeeleweka, juzi nilikuwa kijijini huko mtoto wa mdogo wangu karudi mbio kumuuliza akasema wanachanjwa shuleni, ikabidi nicheke tu.
Watanzania tunapenda kulishana ujinga.
Mbona sisi enzi zetu tulikua tukiona ambulance to shuleni tulikuwa tunakimbia shule nzima,huku tukisema nyonya damu hao wamekuja shule kutunyonyaa Damu!! Utoto rahaa sana!!
 
Juzi nimekutana na kabinti kangu,kana umri wa miaka 5

Kanasema baba wazungu wanataka kutuua kwa kutuchoma sindano shuleni! Wazungu watu wa shetani, mm siendi shulen tena

Namuuliza nani kakwambia haya , anasema ni mwalimu!
 
To be honest bigup kwa jp amewafungua watz ,bila hivyo kwa ss watu wangekuwa qamepachikwa machanjo mpaka basi,hatukatai kuwa na chanjo kwa afya ya mwl ni Jambo jema,Ila hii ya corona inamaluweluwe mengi mno.
Are you sure with what you are alleging?
 
Na
View attachment 1888220
Picha: Baadhi ya Wazazi wakiwa katika Shule ya Msingi Imanga

Wazazi wa watoto wanaosoma Shule ya Msingi Imanga katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wamezuka shuleni hapo kwa madai ya kuhoji sababu za wanafunzi kupewa chanjo dhidi ya corona bila kupewa taarifa.

Hata hivyo, Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Carlos Mabula amesema leo Jumatano Agosti 11 kuwa wazazi hao waliandamana na kufika shuleni hapo huku wakiwa na hasira ya kudhani ugeni uliofika shuleni hapo ni kwa ajili ya kuchoma chanjo wanafunzi wa shule hiyo.

"Nilitembelewa na wageni ambao ni watalaamu kutoka Tari (Taasisi ya Kilimo Tanzania) waliofika shuleni kwenye shamba la michikichi ili kujionea hali halisi ya shamba hilo. Hali hiyo ilisababisha mtafaruku uliolazimisha walimu kuanza kuwatuliza wazazi na kutoa elimu ya chanjo ya virusi vya corona.” amesema Mabula.

Awali, shuleni hapo yalifika magari mawili ya watafiti kutoka Tari kuangalia maendeleo ya shamba la michikichi lenye mbegu bora aina ya Tenera iliyofanyiwa utafiti na Tari-Kihinga.

Mmoja wa wazazi hao, Fikiri Waziri amesema kwa kuwa chanjo ni hiari, walimu hawawapi nafasi ya kupata elimu itokananyo na chanjo.

Amesema kitendo cha magari kufika shuleni hapo kimewasababisha wanafunzi kukimbia kurejea nyumbani kuogopa kuchomwa chanjo.

Mwananchi
Nadhani sasa tunaanza taratibu kuongeà lugha moja. Tuliposema elimu kuhusu HV IKO haijapelekwa na watu sahihi tulibezwa sana. Selikari yetu inapeleka elimu ya UVIKO kama matangazo na kutishia hatua zitakazochukuliwa kwa atakaeyekaidi. Hii ilitakiwa kuwa hatua ya mwisho. Kuna wahubiri leo hii anaendesha kipindi siku nzima kuhubiri kupinga CHANJO kanisani, mitaani, mitandaoni na pengine popote alipo. Sasa watu wanazidi kupandikizwa elimu isiyosahihi na wanaifuata. Kundi linalosikiliza TBC linahesabika, watu kutokana na hofu ya maisha na kutekwa kiimañi wanadhani uchumi upo kanisani, wakifika kule wanakutana na upotoshaji. Watalaam wa afya sasa hawaaminiki alipopita mchungaji/ Askofu. 2atumishi wa afya nao sasa wengine wanasubiri mshahara huku wakiendeleza imani za dini zao kazini hatakusoma chanjo hizo kiundani hawataki. Sasa kuna watu wanatoka mitaani kufuata chanjo vituoni lakini watumishi wa afya hawajachanja eti wanahofu madhara yanayohusishwa na vifo na kuzaa kwa baada ya miaka kadhaa, na hii ni kulishwa elimu isiyosahihi na watu wa imani wanaowamini. Elimu yao haijawasaidia kuelewa chanjo zinafanyaje kazi.
Taifa liirudishe imani ya wataalamu wake, kwa sasa wamemezwa na siasa na dini. Na wao ndio pekee wanaweza kupindua upotoshaji mkubwa wasasa. Waingie mitaani kuelimisha chanjo zote kwa ujumla.
Turudi
 
View attachment 1888220
Picha: Baadhi ya Wazazi wakiwa katika Shule ya Msingi Imanga

Wazazi wa watoto wanaosoma Shule ya Msingi Imanga katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wamezuka shuleni hapo kwa madai ya kuhoji sababu za wanafunzi kupewa chanjo dhidi ya corona bila kupewa taarifa.

Hata hivyo, Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Carlos Mabula amesema leo Jumatano Agosti 11 kuwa wazazi hao waliandamana na kufika shuleni hapo huku wakiwa na hasira ya kudhani ugeni uliofika shuleni hapo ni kwa ajili ya kuchoma chanjo wanafunzi wa shule hiyo.

"Nilitembelewa na wageni ambao ni watalaamu kutoka Tari (Taasisi ya Kilimo Tanzania) waliofika shuleni kwenye shamba la michikichi ili kujionea hali halisi ya shamba hilo. Hali hiyo ilisababisha mtafaruku uliolazimisha walimu kuanza kuwatuliza wazazi na kutoa elimu ya chanjo ya virusi vya corona.” amesema Mabula.

Awali, shuleni hapo yalifika magari mawili ya watafiti kutoka Tari kuangalia maendeleo ya shamba la michikichi lenye mbegu bora aina ya Tenera iliyofanyiwa utafiti na Tari-Kihinga.

Mmoja wa wazazi hao, Fikiri Waziri amesema kwa kuwa chanjo ni hiari, walimu hawawapi nafasi ya kupata elimu itokananyo na chanjo.

Amesema kitendo cha magari kufika shuleni hapo kimewasababisha wanafunzi kukimbia kurejea nyumbani kuogopa kuchomwa chanjo.

Mwananchi
View attachment 1888220
Picha: Baadhi ya Wazazi wakiwa katika Shule ya Msingi Imanga

Wazazi wa watoto wanaosoma Shule ya Msingi Imanga katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wamezuka shuleni hapo kwa madai ya kuhoji sababu za wanafunzi kupewa chanjo dhidi ya corona bila kupewa taarifa.

Hata hivyo, Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Carlos Mabula amesema leo Jumatano Agosti 11 kuwa wazazi hao waliandamana na kufika shuleni hapo huku wakiwa na hasira ya kudhani ugeni uliofika shuleni hapo ni kwa ajili ya kuchoma chanjo wanafunzi wa shule hiyo.

"Nilitembelewa na wageni ambao ni watalaamu kutoka Tari (Taasisi ya Kilimo Tanzania) waliofika shuleni kwenye shamba la michikichi ili kujionea hali halisi ya shamba hilo. Hali hiyo ilisababisha mtafaruku uliolazimisha walimu kuanza kuwatuliza wazazi na kutoa elimu ya chanjo ya virusi vya corona.” amesema Mabula.

Awali, shuleni hapo yalifika magari mawili ya watafiti kutoka Tari kuangalia maendeleo ya shamba la michikichi lenye mbegu bora aina ya Tenera iliyofanyiwa utafiti na Tari-Kihinga.

Mmoja wa wazazi hao, Fikiri Waziri amesema kwa kuwa chanjo ni hiari, walimu hawawapi nafasi ya kupata elimu itokananyo na chanjo.

Amesema kitendo cha magari kufika shuleni hapo kimewasababisha wanafunzi kukimbia kurejea nyumbani kuogopa kuchomwa chanjo.

Mwananchi
Hata hivyo kama mambo mengine yana wasemaji wakuu. Kwanini Afya wanajamii wote wamekuwa wasemaji? Tunaona sasa eti Dini na siasa ndiyo wanatumbana kuhusu UVIKO na wizara ya afya na wataalam wake wamewekwa pembeni. Kisayansi ushahidi wa chwnjo zinaandaliwaje upo tatizo ni nani anayeeleza utaratibu huo kwenye jamii na anaulewa wa kutosha juu ya hilo?
 
Back
Top Bottom