wanashindwa kujiuliza, Canada ambayo ipo magharibi, UIngereza, ufaransa, nchi kibao za francophone huko africa magharibi, Marekani ambayo ina maadui lukuki, wana uraia pacha. na dunia ya leo Marekani anafahamu kuwa kesho iran itarusha makombora au Urusi itapiga ukrain wakati akiwa washington anakunywa kahawa. ulimwengu tuliofikia tunahitaji watu mara chache sana kutulinda, zaidi ni mitambo ambayo africa hatuna, sisi bado tupo kwenye ujima. simu zote hatuundi hapa, computer zote, tech zote hadi internet tunategemea tech zao, wakiwa kwao wanatuchungulia hadi hawahitaji kugharimia kulipa mamluki waishi hapa, wanahitaji wachache tu, sasa tunacholinda ni nini?
halafu, hivi ukifungua milango watu wakawekeza hapa, wakajenga hapa hiyo ardhi mnayoilinda kwani wataipakiza kwenye ndege? si kila kitu kinahitaji kutungiwa sheria tu? nchi zote zenye uraia pacha zimefanya vizuri kuliko zinazolinda. na diaspora wengi wamepata uraia kule ila pesa kibao wanaletea ndugu hapahapa bongo, wanatibu ndugu ambao serikali imeshindwa kuwapa hata bima. na waliomba uraia pacha kwa ajili ya kutafuta maisha tu ila nyumbani ni nyumbani hata iweje.