Kigwangalla: Kwanini Serikali imenunua mabehewa ya SGR yaliyotumika (used)?

Hivi raisi yeye haoni wala kuwaza mpaka tuwe tunamuondoa kwenye lawama!? Kale kadaraja pale pwani kwa B7 tumepigwa, haya mabehewa pia tumepigwa. Haya mataifa ya Africa bila rushwa tungefika mbali sana
 
Nadhani sijakuelewa kwenye pragraph ya pili kuanzia sentensi ya pili, nilivyokusoma na kukuelewa ni kama umemaanisha huyo mama wa Bagaille aliyekuwa afisa elimu alimpa barua mwanae aende shule, lakini Kigwangallah akaichukua kwa kutumia jina la mwingine..

Hebu tuambie, hiyo barua ilimfikia vipi Kigwangallah? na huyo mama wa mtoto aliyetakiwa kwenda shule, baada ya kuona mwanae hajaenda amekwenda mwingine, alichukua hatua gani? au kama aliamua kukaa kimya huoni inawezekana palikuwepo na makubaliano kati ya mama wa mtoto na Kigwangallah?

Kwa mtazamo wangu, kama palikuwepo na makubaliano kati yao, basi sioni kwa vipi Kigwangallah anastahili kuitwa mwizi, kwani mwizi ni mtu anayechukua kitu cha mwingine bila ruhusa, jambo ambalo Kigwangallah inawezekana hakulifanya.
 
Najua mama yuko na sisi, tunachofanya ni kumsaidia kazi ya kuwawajibisha watu wajanja wajanja! Peke yake hawezi kufanya yote haya!"
Hii ni dharau kwa Mwenyekiti wa Chama na kiongozi wetu wa Nchi. Yaani, anasema Mama hawezi? Machineries zote alizonazo Mama, Hamisi anasema Mama hawezi, kweli? Kwamba Hamisi ndiye mwenye uwezo wa kuziba mapungufu ya Mama ! Mapungufu ambayo mimi siyaoni. Hamisi awajibishwe kwa dharau hizi!!!
 
Wanajifanya wanamtanguliza Kigwa ila kiuhalisia wanatupanga na vile wanajua kucheza na akili zetu
 
Anachokifanya ni kitu kizuri sema akipata uteuzi atakuwa bubu
 
hapo kwenye kumsifia mama, ndipo ameonyesha nia yake. Akiteuliwa wizara inayohusika na TRC hatazungumza tena.....ukiona mwanasiasa tanzania analalamika ujue njaa inamsumbua
 
Yani awamu hii tumekosa mtu kama Dr slaa au kafukulila, au zitto kabwe pale bungeni pangewaka moto yani pangechimbikanl zaidi ya richmond inaonekana Kuna mambo mengi sana nyuma ya pazia yani Kuna upigaji mwingi sana sema tumekosa mtu wakutupa data upinzani wa Sasa umepoa hakuna vijana wakufukunyua fukunyua data na kuja nazo, wandishi nao hivyo hivyo udadisi mdogo

JF nao mtu akija na nondo zake hapa mod watafuta
 
Hivi hiki kivuko chakavu ingawa kilinunuliwa kwa mabilioni, hivi leo hoja yoyote ya kujua kilipo ni marufuku hadi humu JF. Kwa kweli CCM ni dampo halafu unakuta watu wenye akili timamu wanashangaa nzi kupiga kambi kwenye dampo...CCM oyee!

Masikini Watanzania, kuna viumbe vinatafuna kodi zetu hadi kuvimbiwa huku sisi tunapiga makofi na vigelegele na tukivitafutia sifa za kuwapa. Wakati vinavimbiwa, wapo wananchi wenzetu hata mlo moja kwa siku ni kwa kubahatisha...kazi iendelee!
 
linapofika suala la kuonyesha uzalendo ktk masuala yanoyohusu maslahi ya taifa, wanasiasa wa sisiemu sio wa kuwaamini hata kidogo.

leo atatoa msimamo kuonyesha yupo pamoja na wananchi. keshokutwa akilambishwa asali kidogo ataibuka na msimamo tofauti na ule wa awali.

kigwangalla ni wa aina hiyo. ni suala la muda tu ataibuka na ngonjera za kusifia hayo mabehewa. mtakuja kuniambia, nimekaa paleeeee.
 
Akipewa uteuzi ataanza kusiifia.

CCM hawana uchungu na hii nchi na watu wake.

Ufisadi ni jadi ya CCM na wanalindana kwelikweli.

Mama anaweza kukaa kimya kama hajui kinachoendelea.

Usikute watu wameshaanza kutafuta fedha za uchaguzi ujao.
ajibiwe kwa hoja japo na yeye ni wale wale
 
Hivi raisi yeye haoni wala kuwaza mpaka tuwe tunamuondoa kwenye lawama!? Kale kadaraja pale pwani kwa B7 tumepigwa, haya mabehewa pia tumepigwa. Haya mataifa ya Africa bila rushwa tungefika mbali sana
ongezea na bwawa la mwalimu nyenyere plus kukatika kwa umeme japo mvua zinanyesha na kina cha maji kwenye mabwawa kimeongezeka
 
Ni Nani basi msafi na mkweli ndani ya CCM??
 
Si akawaulize huko huko walipo

Ova
 
Kigwa aliona kapuyanga kurukukia alichosema bashiru na mama kukazia wasimsifie basi ameamua kuja kwenye kiki hii! Basi uwe unaongea vitu nya maana Kama hivi
 
Hii nchi mtu akisema ukweli anadhambuliwa,kama kasema uongo njooni na ukweli.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…