Kigwangalla: Kwanini Serikali imenunua mabehewa ya SGR yaliyotumika (used)?

Kigwangalla: Kwanini Serikali imenunua mabehewa ya SGR yaliyotumika (used)?

Hii Hoja ni Nzito Sana

Ila kwakuwa Imeletwa Na HK basi hoja Inaonekana Nyepesi kuliko Jina La HK
 
Naunga hoja ya Dr. Kigwangala.

Kuna baadhi ya watendaji walio miniwa wanataka kutumia kivuli cha Mama kufanya mambo yao! either kwa lengo la kumchafua mama au kwa tamaa zao binafsi.

lazima tuwe makini kama kweli tunataka kumsaidia Rais basi tuwe wa kweli na waadilifu.

Je haya mabehewa used yana ubora ulio takiwa au ndio used choka mbaya?!
wasiwasi wa Kigaangwla ni kwamba huenda haya mabehewa used kuna upigaji, hivyo sio vibaya kuchunguza.

kweli kulikuwa na lengo la kununua mabehewa yaliyo tumika, lakini suala la msingi hapa ni je? haya used yana viwango vilivyo kusudiwa au ndio watu/watendaji wamefanya yao?!
ili kuondoa hisia ni vyema uchunguzi ufanyike ili kujua bei halali na ubora wa mabehewa, je unlingana na thamani ya fedha?
 
kweli kulikuwa na lengo la kununua mabehewa yaliyo tumika, lakini suala la msingi hapa ni je? haya used yana viwango vilivyo kusudiwa au ndio watu/watendaji wamefanya yao?

ili kuondoa hisia ni vyema uchunguzi ufanyike ili kujua bei halali na ubora wa mabehewa, je unlingana na thamani ya fedha?
 
Mbunge wa Nzenga Vijijini Dr. Hamisi Kigwangalla kupitia mtandao wa twitter amehoji kwanini Serikali imenunua mabehewa “used”

Amesema “Hili behewa moja (tena used) limenunuliwa kwa sh ngapi? Tumeambiwa yapo haya mabehewa 54, yamenunuliwa kwa us$ 59mn. Kwa hiyo behewa moja ...
sheria si wanapitisha wao sasa anamhoji nani?Awaulize watu wa manunuzi wamwambie kama sheria inaruhusu au hairuhusu.na kuhusu bei akahoji bungeni ndo platform pekee kwake ya kupata majibu ya maswali yake vinginevyo anatubore tu.
 
Mjumbe hauwawi!
 

Attachments

  • Insta_1670309348873.mp4
    532.1 KB
Mama alitoa ufafanuzi Ila ufafanuzi wake ulikuwa wa kimama sio wa ki Raisi "kuwa yatakuja tuu yawe yametumika au vyovyote yatarekebishwa na tutayatumia" Nimeona clip ya Mama toka Clouds TV Leo asubuhi, jee sheria ya manunuzi ya serikali IPO vipi kuhusu kununua vitu vya uma...!!?? Au sheria hutumika kwenye kununua V8 pekee!!?? Nisaidieni wakuu uwezo wangu wa kufikiri umeishia hapa..
 
Nadhani sijakuelewa kwenye pragraph ya pili kuanzia sentensi ya pili, nilivyokusoma na kukuelewa ni kama umemaanisha huyo mama wa Bagaille aliyekuwa afisa elimu alimpa barua mwanae aende shule, lakini Kigwangallah akaichukua kwa kutumia jina la mwingine....
utakuwa hujui mambo ya zamani wewe,unaambiwa mwanao hajachaguliwa imeisha hiyo
 
linapofika suala la kuonyesha uzalendo ktk masuala yanoyohusu maslahi ya taifa, wanasiasa wa sisiemu sio wa kuwaamini hata kidogo
UKAWAII.jpg

Naona hujawaelewa wanasiasa, hawatofautiani tabia.Utofauti upo kwenye rangi ya vyama vyao.
 
F1EB337C-BA61-407B-93AC-5C12EC60332C.jpeg


D32E64B0-EA49-4EB8-BB3A-7B37548DA171.jpeg

Akiendelea kuzungumzia sakata la Shirika la Reli Nchini, TRC kununua mabehewa "Used" ya Mradi wa SGR, Mbunge wa Nzega, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema ni wajibu wa watumishi wa Umma kuwa Wanyenyekevu na Kujibu hoja kwa Uwazi na kina, na sio kukasirika

Amesema, "Reli iliyokamilika ni ya karibu. Kama manunuzi yangekuwa yanazingatia ukweli na uhalisia wa utekelezaji wa mradi na hatua zilizofikiwa, basi cha kwanza kufika ingekuwa ni ile treni ya EMU kwa maelezo ya TRC ya kigezo cha (masafa mafupi). Hizi Sobibor zilikuwa zije mwishoni kabisa"

Ameendelea, "Ukiwa mtumishi wa Umma ujue una wajibu wa kujibu kwa kina na kwa uwazi, na zaidi uwe mnyenyekevu na usikasirishwe na watu wanaohoji, hao wanakufanya uwe makini zaidi kazini na ujiepushe na CAG, TAKUKURU, BUNGE na hatimaye JELA na aibu kwa umma!"
 
wewe karibu tunakupa mkono wa kwaheri maana CCM ukianza kuchimba vitu wewe ndio kwaheri 👋
 
Back
Top Bottom