Kigwangalla: Kwanini Serikali imenunua mabehewa ya SGR yaliyotumika (used)?

kwrnye suala la mabehewa mmetuumiza Sana mradi wetu ni mkubwa Sana wa trillions of money hatukutakiwa kufanya vitu vya mzaha ety kuanza na mitumba hafu mnatuletea mabehewa ya hovyo kiasi hiki mradi utakaodumu miaka 100 ijayo kama ujenzi umegharimu 16 trillion mnashindwa kweli kuongeza trillion 2 zaidi na sisi tukawa na kautalii ketu kwa nn mnatutesa wananchi sisi ni wa vitu vibaya tu kweli?
 
Weeee

Ishia hukohukoo

Na hizo kodi tunazolipa haziwatoshii.

Wewe inaonyesha sio mlipa kodi.

Ni mtegemezi kwenye familia ya mtuu
 
Jamaa wameshavuta chao
 
Symbion amelipwa mabilioni bila kufuata utaratibu, kwa hiyo fedha zipo
 
Nijuavyo mimi, usafiri wa reli unapaswa kuwa wa raha mustarehe, nafasi ya kutosha bila msongamano...

Hivyo ndivyo ilivyo huko majuu na naamini ndio lilikuwa lengo la kujenga reli mpya ya kisasa sambamba na ile ya zamani.

Mabehewa yaliyoletwa hayafanani na reli na vituo tulivyojenga, treni na mabehewa ni lazima viendane. Lengo ni kusafirisha abiria na mizigo kwa raha zaidi, kwa nafasi na haraka zaidi.

Kutuletea mabehewa ambayo yanafanana na yale yaliyowahi kuletwa kutoka India miaka ya themanini, ni dharau kwa wananchi ambao wametozwa kodi ili reli ijengwe. Nendeni China au Japan mkanunue mabehewa na treni za kisasa muache janja janja.

Sisi ndio wapandaji wa hiyo treni na mabehewa yake tofauti na nyie wenye ma VX mapya kabisa ya shilling million 400...... Tunastahili vitu vizuri na bora kwa kodi tunayolipa. 😡
 
Huyo ni mwizi na mnafiki. Kwanza Baba yake siyo Kigwangala bali ni Bagalile. Aliiba jina la Hamus Kigwangalaaliyekuwaamechaguliwa kwenda kysoma Kigoma...
Hapo sasa!!, ukifanya uchunguzi kwenye majina ya watu, hasa wasomi wa miaka kati ya sabini na themanini, unaweza kutengeneza ile kitu wanaita "Bongo movie". 😀 😀 😀 😀
 
Kigwa unajitekenya na kucheka mwenyeweee[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huyo ni mwizi na mnafiki. Kwanza Baba yake siyo Kigwangala bali ni Bagalile. Aliiba jina la Hamus Kigwangalaaliyekuwaamechaguliwa kwenda kysoma Kigoma....
Kama alilitumia jina la mtu basi atakuwa amelitendee haki sana
 
Kila kinachoendelea hapa nchini ambacho Hayati JPM alikisimamia vyema sasa kina mauzauza na harufu za upigaji.

Kwa nini kununua mabehewa used? Kuna haraka gani ili hali mradi unasuasua kumalizika?

Mradi wa JNHP ndiyo una mauza uza kabisa na kuna dalili na ushahidi wa kimazingira kuwa kuna mikakati usimalizike kwa wakati ili mgao wa umeme uwanufaishe wahuni wa CCM.

Tanzania inanunua used? Why? Mitumba?
Your browser is not able to display this video.
 
Mbunge wa Nzenga Vijijini Dr. Hamisi Kigwangalla kupitia mtandao wa twitter amehoji kwanini Serikali imenunua mabehewa “used”...
Inawezekana kukawa na cha kuhoji maana serikali zetu always bila ya uongo hatuendi. Lakini, kuna haja gani ya kusema mama hahusiki?

Kwani Kigwa kaulizwa kama mama kahusika au la? Yeye aichane serikali, wenyewe watajipanga. Kama mama hahusiki na vinamkera si yeye kashika mpini, atumie kisu sasa.
 
Behewa moja jipya bei yake ni TSh 200 million au Rs 2.5 million au TSh 200,000,000. Kama ni kweli tumeuziwa behewa moja kwa TSh 2.57 billion basi tutakuwa tumepigwa mara 10. Yaani tujamaa tumeongeza sufuri moja kwenye 200,000,000. Simple as that. Hii ni ngumu kuamini ikawa kweli. Yaani kila behewa wapige TSh 1.8 billion. Kwa behewa 54 watakuwa wameweka kibindoni TSh 100 billion. Hilihaliwezi kuwa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…