Jumbe Brown
JF-Expert Member
- Jun 23, 2020
- 12,077
- 12,786
Ndugu RBC ni kweli wewe una fedha nyingi.....Njaa mbaya sana ! kila kapuku wa ccm kaagizwa kuleta uzi huu jf , hivi ni kweli mnalipwa tsh elfu 7 kwa wiki ?
Kwanini mnatumikishwa kibwege sana ! uzi mmoja watu 100 kweli !Ndugu RBC ni kweli wewe una fedha nyingi.....
Biashara ulizonazo ndani na nje ya nchi si kigezo cha sisi wengine kutokuwa na fedha "kiduchu" ambayo ni halali ya kututimizia mahitaji yetu muhimu ya kila siku.....
Kweli sina utajiri ulionao wewe na familia yako na hwenda nisiufikie ukwasi wako mpaka naingia kaburini ila si sababu ya kila UCHAO kututukana raia wenzako kuwa ni MAKAPUKU.......
Niishie hapa bibie tajiri!
#KaziIendelee
#SiempreCCM
#TujitokezeniKuchanjwa
#NchiKwanza
Mkuu RBC...Kwanini mnatumikishwa kibwege sana ! uzi mmoja watu 100 kweli !
Hata Polepole enzi za Jiwe aliamini hivyo , wacha atafunwe tuHoja niliyoiona hapa dhidi ya Mr Slow ni kwamba mwenyekiti hatakiwi kupingwa. Hii ni hatari na nusu.
Nyuzi za wachumia tumbo wenzako kuhusiana na hili umeziona ?Mkuu RBC...
Kwa hiyo kila anayeandika uzi humu ndani anatumikishwa?
Una ushahidi ama unaongea kihisia tu kwa sababu ya kiburi cha fedha ulizonazo?!
Tofauti tu ni kwamba Mr Slow alikuwa anamtetea Rais mzalendo; huyu anaitetea korona.Hata Polepole enzi za Jiwe aliamini hivyo , wacha atafunwe tu
Lini mlimpinga mh.mwenyekiti Mbowe?!!Hata Polepole enzi za Jiwe aliamini hivyo , wacha atafunwe tu
CCM inasemewa na Stephen Nyerere.!? Maskini Tanzania ndio tulipofikia hapa. Uhiari wa chanjo unafungwa na Rais kuchanja? Kwa nini waliochanja wawe na haki ya kuhimiza wasio chanja kuchanja. Wasio chanja wasiwe na haki ya kuhimiza watu waikatae chanjo yenye walakini mwingi.
Kwa nini Mh Polepole na sio Mh Askofu Gwajima? Ubunge wa Polepole alipewa na JPM hili nalo UV-CCM hawalijui? Heshima hailazimishiwi itakuja yenyewe kutokana na matendo yako kwa jamii.
kwa lipi ?Lini mlimpinga mh.mwenyekiti Mbowe?!!
Nikumbushe lini ?!!
Tajiri RBC....Nyuzi za wachumia tumbo wenzako kuhusiana na hili umeziona ?
Umenithibitishia kuwa huwa hamumpingi mwenyekiti wenu....kwa lipi ?
Asingekuwa mzalendo asingepitishwa kuwa AMIRI JESHI wa nchi hii.....Tofauti tu ni kwamba Mr Slow alikuwa anamtetea Rais mzalendo; huyu anaitetea korona.
Mkuu, fafanua kidogo basi tukuelewe juu ya hiyo ☝Ndugu RBC ni kweli wewe una fedha nyingi.....
Umeandika kihunihuni ila nimekuelewa.Katibu Mkuu wa UVCCM ,Camarada El Comandante mtunduizi mh.Kenani Kihongosi amemtaka mh.mbunge kamarada Humphrey Polepole atambue kuwa CCM si chama Cha kiharakati (vilivyo vya upinzani) bali chama kilichoaminiwa vyema na watanzania kusimamia maslahi yao kuntu.
Ameendelea kumkumbusha kaka yetu ndugu H.Polepole kuwa CCM imesimikwa juu ya nidhamu kuu kwa mwenyekiti wetu na viongozi wengine.
Hii ni ada na kawaida ya CCM inayosisitiziwa sana katika MADARASA YA ITIKADI.
Kamarada Kenani Kihongosi amemkumbusha ndg.Kamarada Polepole ya kwamba AENDELEE KUIHESHIMU SERIKALI NA VIONGOZI WAKE KAMA ALIVYOFANYA NA KUONEKANA AKIENENDA VYEMA WAKATI WA UTAWALA WA AWAMU YA 5.
Ndg.Polepole anakumbushwa kuwa CHANJO NI HIYARI NA SI LAZIMA....ila kuipinga kwa hoja kinzani ni kumpinga mwenyekiti wake wa CCM mh.Rais SSH na SERIKALI YAKE.
SIEMPRE CCM
HASTA LA VICTORIA CCM
#SiempreSSH
#TujitokezeniKuchanjwa
#KaziIendelee
Vipi hajamuonya gwajiboy Mzee wa verse moja?Sehemu ya Nukuu za Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndugu. Kenani Kihongosi Akimjibu Mbunge wa Kuteuliwa na Rais Ndugu Humphrey Polepole.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi - UVCCM, Ndugu. Kenani Kihongosi amesema, wanasikitishwa na matendo yanayofanywa na mbunge Humphrey Polepole kuhusu suala la chanjo ya corona, kwani Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshasema kwamba chanjo ni hiyari na maamuzi yake lazima yaheshimiwe.
"Tunapenda kumwambia mbunge Humphrey Polepole kwamba awe na nidhamu na adabu kama aliyokuwa nayo wakati wa Utawala wa Awamu ya Tano. Nidhamu ile ile aiendeleze pia katika utawala huu wa awamu ya Sita Inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan " Kenani Kihongosi, Katibu Mkuu wa UVCCM.
"Mijadala yake (Humphrey Polepole) kuhusu chanjo ni bora akakaa kimya kama hahitaji kuchanja lakini sio kujificha katika kivuli cha chanjo kuipinga serikali." Kenani Kihongosi, Katibu Mkuu wa UVCCM.
"Tunamuonya na tunamtaka Humphrey Polepole aache mara moja mijadala yake kuhusu chanjo kwani hatutakubali kiongozi yoyote avunje heshima ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan au kupinga yale aliyoyaelekeza" Ndugu Kenani Kihongosi, Katibu Mkuu wa UVCCM.
"Hatutovumilia utovu wowote wa nidhamu kwa Rais. Humphrey Polepole kuendelea kutengeneza maneno ya kejeli, dhihaka na mengine ya aina hiyo yanabeba mazingira yanayotia shaka dhamira yake aliyonayo kwa Mwenyekiti wetu na Rais wetu, hivyo tunamtaka aache mara moja" Kenani Kihongosi.
"Chama cha Mapinduzi (CCM) siyo chama cha harakati bali ni chama kilichojijenga katika misingi ya kutii na kuheshimu viongozi, hivyo jambo lolote la kupingana au kuendeleza mijadala ambayo Mwenyekiti wa CCM Taifa ameshalitolea maelekezo ni utovu wa nidhamu" Ndugu Kenani Kihongosi.
Ndugu. Kenani Kihongosi
Katibu Mkuu wa UVCCM.
View attachment 1885779
View attachment 1885780
Wanamgambo wanaruka na kukanyagana.Fisi wanaparuana.