Kiini cha Falsafa, dini za Uislamu na Ukristu ni Afrika


Waebrania 6:13
Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lake mwenyewe, maana hakuna aliye mkuu kuliko Mungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa.

Haya na wewe dadavua Allah Kuala kwa aliyeumba cha kiume na cha kike
 
Waebrania 6:13
Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lake mwenyewe, maana hakuna aliye mkuu kuliko Mungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa.

Haya na wewe dadavua Allah Kuala kwa aliyeumba cha kiume na cha kike


kwanza nashukuru umefahamu kwamba Mungu anaapa kwa ajili ya kuweka mkazo katika agano/ahadi.
Lakini pili mara nyingi huwa napata tabu na nyinyi kwenye lugha.kwa mfano unawezaje kutofautisha jina la MUNGU na sifa za MUNGU.

Kwa mfano niseme Muumba mbingu na nchi unaweza kusema MUNGU ni mwingine na Muumba mbingu na nchi ni mwingine.

Qur-an ni kitabu elekezi.kama unauelewa kama unakubali MUNGU wa biblia anaapa kwa jina lake mwenyewe vipi unashindwa kufahamu allah wa Qur-an kuapa kwa sifa zake mwenyewe.
Qur-an nzima imeanza ktk kila sura BISMI LLAHI RRAHMANI RRAHIM yaani KWAJINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREMU.jumla kuna BISMILLAHI 114 hizo zote zina maana Mungu anaapa kwa jina lake mwenyewe.

Nimedadavua kwa kirefu .
 
Ukitaka kufahamu maana ya kitu kiundani basi soma kitu chote kielewe,umesoma hiyo Quran Mungu akiiapa kwa aliyeumba kike na kiume(Quran 92-1-2)unapotaka kufahamu soma kuanzia hapo 1-7 kama kufika mwisho umeshindwa basi utajua Allah alikuwa akimaanisha....samahani mleta uzi kwa kuingiza mada nyingine
 
Hiyo sehemu uliyoisema haiishi aya ya 3 bado inaendelea soma mpaka aya ya 7 kisha hoji kutokea hapo!
 

Pole Sana, Mungu ni "generic name' kwa kila aabudiwaye na binadam katika mazingira na imani tofauti tofauti, Biblia tangu agano la kale halijapungukiwa mungu waliokuwa wanaabudiwa na mataifa na makabila mbalimbali sambamba na Mungu (YHW) muumba wa mbingu na ardhi na vyote vijazavyo,
Historia iko wazi kwamba kabla ya Muhammad Makuraish walikuwa wanamwabudu Allah aliyekuwa na wasaidizi zaidi ya 360 na sehemu yao ya matambiko na hijja kwa mungu wao ilikuwa ni hii ambayo inatumiwa na ninyi Kama sehemu takatifu na kwenda kufanya hijja huko sawa na walivyofanya makuraish.
Tukirudi kwenye kiapo cha Allah, yeye kaapa kwa hali na uumbaji sawa, lakinipia kaapa kwa Aliyeumba cha kiume na cha kike, Mungu wa Biblia amesema wazi hakuna aliyemkuu kuliko yeye hivyo anaapa kwa nafsi yake, hiyo lugha mnayosema hatujui ni ipi ?
Hizo Bismillah ni mbwembwe za kiuandishi, sawa na Mimi nikianza kila aya na Bwana asifiwe ...
Hujadadavua Lugha ya kuapa kwa aliyeumba cha kiume na cha kike imetumikaje kumaanisha anayeapa na anayeapiwa ni mmoja yule yule
 

Quran haisomwi kwa kuangalia context, kilichoandikwa ndicho inachomaanisha.
Wewe ni Muislam unao wajibu wa kutetea maandiko yako na kurekebisha pale unapoona pana kosewa, hiyo biashara ya kutaka mimi nisome hadi mpaka mahala fulan siiwezi, wewe unayetaka kunirekebisha tolea maelezo kadri ya imani na uelewa wako.
Allah kuapa kwa aliyeumba cha kiume na cha kike Ina maana anaye Mkuu zaidi yake na huyo Mkuu ndiye muumbaji wa cha kiume na cha kike.
Anyway kwa kadri ya uelewa wangu Allah hajawahi kuwa Mungu wa kweli Bali ni Mungu aliyeabudiwa na Makuraish "moon god" alikarabatiwa na Muhammad kumfanya awe mpweke bila wssaiduzi wala wana...
 

sasa kama unaelimu juu ya Qur-an na hutaki kuelekezwa naomba tuingie kwenye Tafsiri kubwa za Qur-an ili tuone aya hii imetafsiriwa vipi.

maana naona unang'ang'aniza kwamba Mwenyezi Mungu ameapa kwa alieumba kiume na kike,labda ungenisaidia nijue hio Imetafsiriwa na nani na ushahidi wa hadith ipi?

kwanza unatakiwa kufahamu TAFSIRI ZA QUR-AN ni zipi usikurupuke.
 
Naona wafia dini tayari wameharibu mjadala mzuri na kuanza kulingishiana na kuwasifia mabwana zao jinsi walivyo wazuri,..huyu akisema bwana yake myahudi ni bora zaidi ya bwana wa mwenzake mwaarabu.

Huu ni zaidi ya ujuha..tumewaachia jukwaa la dini kule mnakotukanana bila hoja lakn bado mmekuja mpaka huku na up...uuzi.ule ele
 

Tafsiri za Quran nyingi ni kiini macho kuficha udhaifu wa Allah sawa na kiapo hicho. Makrim imebadadilishwa kwa kuwa haiyumkiniki Mungu wa kweli awe best deciever !
Sasa wewe niambie zipi ni tafsiri za wapinga uislam nisizisome...
Mengine yatafute wewe mwenyewe sina ninachotaka jifunza kipya au kinachoweza kumpa Allah daraja tofaufi na alilonalo kwangu.
 

Hivi nawe ni GT ?
 
Naona kuna Objection kutoka kwa Nyamgluu, nitajibu hoja yake post nitakayoweka hivi punde.

 
Nimeona kuna objections zimetolewa na Nyamgluu ambazo nitazijibu. Kwanza Nyamgluu ningeomba uweke kidogo bidii ya kusoma historia ya Africa, hasa historia ya Misri ya kale. I hope utasoma kwa makini majibu yangu.

Nyamgluu amesema:
Mkuu Mzee2000 nimesoma post zako lakini napata kuona ya kwamba unajaribu sana kulazimisha jambo ambalo halilazimiki.

Mzee2000 anajibu:
Mkuu silazimishi jambo, post zangu nilizoandika nimetoa na evidence angalia evidence nilizotoa halafu utoe counter-evidence . Sitaki kukutukana lakini uelewa wako wa historia bado mdogo, jitahidi kusoma vitabu vya historia, hii issue ni multidisciplinary sio rahisi kwa mtu wa kawaida, lakini bila shaka nitakayosema hapa chini yatasaidia kukuelemisha.

Nyamgluu anasema:

Kuna makabila zaidi ya 200 Afrika, sasa eti kwa sababu kati ya hayo kuna ambayo wanatahiri na hivyo basi Moses na Abraham kuiga hio tamaduni ya kutahiri basi kunaufanya Uyahudi kuwa na source ya Black Africans pamoja na Ukristo na Uislam is a very very far fetched idea.

Mzee 2000 anajibu
Mkuu, naomba usome post zangu vizuri na uzielewe, sitakufundisha kusoma, read my posts carefully lakini kama haujazielewa ngoja nikupe somo la sayansi ,historian na anthropology.Hii natoa kwa manufaa ya wote humu.

Mmmojawapo ya sababu niliyoitoa kuwa waisraeli waligeza kutahiri kutoka Afrika ni maandishi ya wanazuoni wa zamani ambao walikuwepo muda huo huo ambao biblia iliandikwa( Circa 600BC). nnimetoa mfano wa mwanahistoria wa kigiriki Herodutus ambaye wazungu wanamuita ‘father of history’ huyo katika kitabu chake cha ‘histories’ anasema kabisa kwamba watu wa asia i.e middle east walijifunza kutahiri kutoka kwa wamisri na waetheopia. Hii ni fact ambayo iliithibitisha kwa kuwauliza watu waliokuwa wanaishi muda huo ambao walimweleza hizo facts na yeye aliziona. Vilevile wanahistoria wanapoangalia vitabu vinavyoeleza kutahiri., vitabu vya kwanza/ au evidence kuhusu kutahiri viliandikwa/ vinaonekana Misri na wala sio uyahudini au middle east ndio maana wataalamu wa anthropology hawana doubt kwamba kutahiri kulianzia Africa na wayahudi waligeza hii mila kutoka kwa waafrika.

Vilevile diversity ya kitu ndio kawaida huwa mwanzo wa hicho kitu, hii ndio sheria moja kuu ya anthropology. Kwa mfano tukitaka kuhjua lugha za ki anglo-saxon zilianzia wapi tutaangalia diversity kubwa ya hizo lugha iko wapi. Tunajua lugha za ki anglo saxon zilianzia ulaya ya kaskazini kwa sababu huko ndio kwenye lugha nyingi tofauti( au diversity) zilizoko kwenye kundi hilo. Mfano lugha za kiingereza, kidachi na kijerumani zinaongelewa ulaya ya kaskazini kwahiyo huko ndio chanzo cha hizo lugha za anglo saxon. Hivyo hivyo tamaduni za kutahiri ziko kwa wingi Afrika kuliko sehemu yoyote duniani, kwa hiyi ndio maana wataalamu wanasema Afrika ndio Mwanzo wa kutahiri na wengine waligeza. Nimetoa uthibitisho wa diversity pamoja evidence ya maandishi ya wanahoistoria walioishi muda huo.

Naomba utoe countervidence yenye uzito kuliko ya kwangu .


Nyamgluu anasema

Ni sawa na mtu aje aseme chimbuko la kingereza ni kiswahili sababu kwenye kingereza kuna neno "safari".

Mzee 2000 anajibu:

Huoni uhusiano kwa sababu haujui wala haujasoma historia ya wamisri/ waafrika wa kale ndio maana huoni chochote.Vilevile unapongalia kitu usiangalie kijuu juu tu, angalia kiundani. Waisraeli walichukua misingi ya tamaduni na dini za waaafrika lakini waliongeza au kutoa mambo mengi kiasi cha kwamba ukiangalia sasa hivi unaona kama hamna uhusiano, sikulaumu.

Nyamgluu anasema:

Sijui ni kwanini unataka kufanya kuwa hizi dini kuu zina originate kutoka black africans wakati vitabu vyao wenyewe havisemi hivyo na hakuna imani hata moja ya kiafrika yenye kufanana na Abrahamic religion yeyote ukiachilia mbali swala la kutahiri ambalo katika makundi hayo linabeba maana tofauti kabisa kama wewe mwenyewe ulivosema.

Mzee 2000 anajibu:

Inaelekea hujui tofauti kati history na mythology. Wayahudi kujustfy dini yao ilitoka kwa Mungu wasingeweza kuwataja Wamisri directly kwa sababu hii isinge saidia argument ya Moses kwamba alikuwa nabii wa Mungu katika macho ya waisraeli. Hata hivyo Moses kusemwa kwenye biblia kwamba alikulia Misri na alikuwa ‘Padri’ wa dini za wamisri ni uthibitisho tosha kwamba kimila na kimtazamo alikuwa mwafrika. Nimetoa proof kwenye mfanano wa amri za wamisri na amri kumi za Mungu za waisraeli pamoja na kutahiri.

Nyamgluu anasema

Kwa WaAfrika ni initiation process ya kuashiria mtoto kuwa mwanaume na kwa waYahudi waliambiwa ni ishara ya kuwatofautisha wao na gentiles.

Mzee 2000 anajibu;
Waisrael walichukua concept hiyo hiyo ya waafrika na kuifit kwenye worldview yao.Na hilo wazo la kutahiri la wamisri/ waafrika linaendana na wayahudi, ingawa wayahudi walibadilisha kimtazamo. Natumaini this is simple enough for you to see.

Nyamgluu anasema:

Ni kweli historia kama ilivyoandikwa na watu wengine imekandamiza sehemu ya mwafrika lakini hii imefanya baadhi ya waAfrika kudai vitu ambavyo kwa kweli ni a stretch of the imagination sana.

Mzee 2000 anajibu:

Sio kudai vitu visivyo vyao , tatizo ni waafrika kama wewe, ambaye unabisha facts wakati unaonekana hujui lolote kuhusu historia ya Afrika. Ni wajibu wa Waafrika kufanya research na kugundua facts nyingi ambazo wazungu walificha na kutumia ujinga wetu na kutulaghai.

Nyamgluu anasema:
Kama hili nalo ni a strech of the imagination to the limits of elasticity. Sisi waAfrika imani zetu sio monothiest, sio za kuamini Mungu mmoja bali imani zetu ni za kuamini miungu wengi kama wahindi, wachina na hata hao ma Pharaoh.
Sasa inashangaza kuwa imani ambazo msingi wake ni miungu wengi ndio ziwe chimbuko la imani za Mungu mmoja.

Mzee 2000 anajibu:

Ni kweli Mafarao waliamini miungu mingi kama waafrika wengine ingawa kama waafrika wengine huwa kuna Mungu mkuu. Sasa siwezi kuendelea kukufundisha historia ya Misri, lakini naomba utype google jina la Farao Akhenaten. Huyu ni binadamu wa kwanza kurikodiwa katika historia ya dunia kusema kwamba Mungu ni mmoja. Ni wakati huo huo ambao Moses alisemwa alikuwa anaishi Misri na ndio maana wataalamu wanasema inawezekana Moses alitoa hiyo idea ya Mungu mmoja kutoka kwa Akhenaten. Wamisri hawakupenda ideas za Akhenaten , alipokufa waliendelea kuabudu Miungu mingi. Again, Soma soma soma soma vitabu vya historia, siwezi kukufundisha kila kitu.

Nyamgluu anasema:

Halafu hoja yako unaanza kuijenga kwenye fallacy. Yani msingi wa hoja yako yenyewe ni wa mashaka sana. Maana ili ikubalike kuwa chimbuka la Abrahamic religion ni black African religions inabidi kwanza tukubali kuwa ma Pharaoh na ancient Egyptians were black people.

Mzee 2000 anajibu:

Hivi ni vithibitisho kwamba Pharaos na ancient Egyptians walikuwa black.

1. Kwanza nimetoa uthibitisho kwenye kufanana kwa lugha ya wamisri wa kale na lugha za waafrika wengine kama Hausa wa wanigeria lakini inaelejea hukusoma, kwa hiyo sitarudia tena.
2. Mwanahistoria Heredotus alisema hivi kuhusu wamisri wa kale wakati alipoandika kitabu chake ‘Histories’ takriban 500BC

'There can be no doubt that the Colchians are an Egyptian race. Before I heard any mention of the fact from others, I had remarked it myself. After the thought had struck me, I made inquiries on the subject both in Colchis and in Egypt, and I found that the Colchians had a more distinct recollection of the Egyptians, than the Egyptians had of them. Still the Egyptians said that they believed the Colchians to be descended from the army of Sesostris. My own conjectures were founded, first, on the fact that they are black-skinned and have woolly hair'.

Hapa heredotus anasema kwamba watu wa colchis lazima walitoka Misri kwa sababu kama wamisri, watu wa colchis wana ngozi nyeusi na nywele zilizosimama (kama za kiafrika).

2.Uthibitisho wa pili kwamba wamisri walikuwa waafrika weusi ni sayansi ya kisasa ya mifupa hii paper iliyoandikwa na Dr sonia ni mojawapo ya papers nyingi zilizoandikwa na wanasayansi ambao wamefukua miili ya wamisri wa kale na kuthibitisha kuwa wamisri walikuwa waafrika. Hii ni kutokana na body plan yao, ambayo inafanana na waafrika wanaotoka kwenye tropics (super negroid i.e subsharan Africa ) ingawa Misri haipo kwenye tropics. Paper inatoka conclusion hii;

Variation in Ancient Egyptian Stature and BodyProportions
Sonia R. Zakrzewski*
Department of Archaeology, University of Southampton, Southampton SO17 1BF, UK

'The nature of the body plan was also investigated by comparing the intermembral, brachial, and crural indices for these samples with values obtained from the literature. No significant differences were found in either index through time for either sex. The raw values in Table 6 suggest that Egyptians had the “super Negroid” body plan described by Robins (1983). The values for the brachial and crural indices show that the distal segments of each limb are longer relative to the proximal segments than in many “African” populations (data from Aiello and Dean, 1990). '


3. Uthibitisho wa DNA
DNA za mafarao wa zamani waliokufa zilipimwa na kuthibitishwa kwamba asili yao ni sub sahara Afrika. Paper nzima ambayo conclusion yake nimeiweka hapa chini unaweza kuisoma hapa:
http://www.dnatribes.com/dnatribes-digest-2012-01-01.pdf
Na inasema hivi:

‘Results indicated the autosomal STR profiles of the Amarna period mummies were most frequent in modern populations in several parts of Africa. These results are based on the 8 STR markers for which these pharaonic mummies have been tested, which allow a preliminary geographical analysis for these individuals who lived in Egypt during the Amarna period of the 14th century BCE.’

Nyamgluu anasema:

Hivyo basi mimi binafsi mpaka hapo ulipofikia sijaweza kushawishika ya kwamba kiini cha Uislam na Ukristo ni Black Africans (Bantus) kama tuwajuavyo leo! Ancient Egyptians, Ethiopians wana undugu zaidi kivyao kuliko watu weusi wa west africa, central africa na south. Hatuna chetu humo, una force. Unajua kila race ina physical features zake, sasa ukiangalia physical features za wale ma Pharaoh waliokua mummified hawana typical Bantu African features. Nafikiri ni 1 tu kama nakumbuka vizuri nae ni utata. Na wanao support hii view ya ancient egyptians walikua blacks wanatoa hoja ingine kua ile pua ya sphinx iliomeguka ilivunjwa makusudi sababu ilikua pana na kuonyesha kuwa alikua black african!

Mzee 2000 anajibu:

Samahani lakini inaelekea hujui hata maana ya neno Bantu.bantu ni language group haiendani na mwonekano wa mtu. Kwani waafrika wote afrika wanaongea kibantu? Kibantu ni language group ambayo inongelewa na watu wenye sura na maumbile tofauti. Kuna watusi, wazulu n.k..Wamasai au wasudan au wajaluo wengi ni weusi tii lakini hawaongei lugha ya ‘kibantu’ .Wengine wana pua pana na wengine pua nyembamba. Tanzania kuna makabila mengi ambayo hayaongei lugha za kibantu.Kwa maana hiyo huwezi kusema mwafrika ni mbantu tu.

Halafu umepata wapi hilo wazo laku kuwa waethiopia wanauusiano zaidi na wa Persia? Vipimo vyote vya DNA vinaonyesha kuwa waithiopia ni 100% African. Vipimo vya DNA vinaonyesha kuwa waethiopia ni Haplotype E kama walivyo wabantu na asilimia kubwa ya waafrika.

Hiyo link ya DNA ya mafarao inaonyesha kuwa mafarao walikuwa na DNA ya watu wa Afrika kusini mwa jangwa la sahara. Wamisri wanaoishi sasa hivi misri walivamia kutoka Uarabuni, Greece,Uturuki nk na uvamizi huo unajulikana( umeandikwa kwenye vitabu). Wamisri enzi za mafarao walikuwa waafrika weusi kama nilivyoonyesha kupitia lugha walioiongea, ngozi yao, structure ya miili yao pamoja na vipimo vya DNA na utamaduni wao.
 
Mzee2000 asante kwa kutumia mda wako ili kujaribu kunieleza hili swala. Usijali, kuambiwa sijui sio tusi kwangu sababu hakuna anayejua kila kitu na kujifanya najua kile ambacho sio speciality yangu sio tabia yangu.

Maelezo yako hapo juu yana matundu kadhaa, kwa mfano tafsiri yako ya hio passage ya Heredotus sio sahihi.
Nakubali pia kutumia neno bantu hapo ni makosa.

Napenda pia unavyojitahidi kutoa vithibitisho vya point zako.
Unajua kwa hio reasoning yako basi kila kitu duniani origin yake lazima ije kuwa Afrika sababu DNA and other evidence zinaonyesha kuwa early man originated from Afrika. Sasa with that argument ni kwamba KILA WATU NA TABIA ZAO DUNIANI zitakua na chimbuko Afrika na hivyo mtu mweusi.

Sasa nikipata mda nitapitia mada yako hapo juu niinyambulue point by point, kwa sasa naomba unedelee na maelezo yako ya kwamba kiini cha falsafa za Abrahamic religion in Black Africans kwa kuleta mifano mengine zaidi ya huo wa kutahiriwa.
Nina uhakika utakua na mengine na imani yako sio based kwenye kutahiriwa tu.
 
Last edited by a moderator:

Mwanzoni nilikua sielewi unachokielezea hasa ni kizu gani, na kina umuhimu gani, bt now nimeanza kukuelewa.
 
haya mambo yanachanganya sana,

 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…