Kijana aliyetelekezwa na mke siku ya harusi atunukiwa tuzo ya mwanaume bora wa mwaka na Waziri Gwajima

Kataa ndoa. Ndoa ni utapeli mamboleo. Hongera sana Dkt. Gwajima D kwa kuwa upande wetu wakataa ndoa. Mungu akubariki sana.
 
Nina uhakika swala la ulevi wa huyo jamaa sio kama mwanamke alikuwa halijui,na sio kwamba hiyo siku ya sendoff ilikuwa ni mara ya kwanza kumuona akiwa kalewa,ila inaonekana ni wapambe,either ndugu,wazazi au wanafamilia wamejaza upepo ukamuingia na yeye kwa aibu kaamua kumtema jamaa,ila huko anakoenda pia asifikiri ndio anaenda mahali salama,inaweza kuwa ni ile jumping from frying pan to fire...
 
Kususwa au kuachwa kunauma jamani duh!!! Nakumbuka nakaribia kwenda kujitambulisha ukweni ndo mchumba hataki kuongea nami kila KITU ni kigumu , halafu muda mwingine Nakula blacklist, niliumia sana aseeee.unaweza ua,,, ila hiii Dunia Ina watu wapole sana
 
Kilichonichekesha alikua anacheza wimbo unaimba
"Kama kupendaaa bora nimpende mama yangu🎶
Bora niinjoy🎶
Maisha mafupi🎶🎶
Bora niinjoy
Ampende mama yake baada ya kuachwa na wanaefanya naye ngono? Huu wimbo haufai kabisa kuwa mbadala wa mwanamke. Mapenzi ya mama hayahusiani kabisa na mapenzi yanayohusisha ngono. Mama yako unampenda ukiwa au usipokuwa na mwanamke sababu upendo wake ni wa tofauti.
 
Kwahiyo huyo jamaa alikua sahihi kwenda kwenye send off huku akiwa kalewa chakari?

Tatizo hii issue,wengi mnaiangalia kwa upande mmoja tu,hata kama alikua ni mlevi,je ilikua ni busara kulewa chakari kwenye siku kama hiyo? Mbele ya familia ya mke mtarajiwa?
 
Pamoja na yote kuachana siku ya harusi sio jambo jema
 
Hujambo? Swali zuri. Sasa kuna muktadha mbalimbali wa kuangalia jambo unalotaka kwenda nalo; kwa hapa tumeangalia reaction yake mbele ya wageni wake baada ya kuona yamekuwa hayo, je alibaki mtulivu? Maana mtihani wengi wa utulivu umewashinda wengi wako jela huko na wametuachia majeruhi, Yatima na hata vifo.

Hayo ya aliendaje hapo na tabia zake zikoje, nadhani hizo pande mbili zilipaswa kuchunguzana vema kabla ya kufikia hatua hiyo na kote huko wasingefika.
 
Jamaa alifanya ujinga. Kupewa tuzo ni kupongeza ujinga alioufanya. Kisingizio kuwa kapewa tuzo sababu hajafanya ukatili ni kisingizio dhaifu. Kama waziri anaona ilikuwa sawa, siku ya kuapishwa kwake mbona hakulewa chakari? Angelewa bwii apewe tuzo. Kijana anakuja siku muhimu ya kukabidhiwa mke halafu yupo chakari kalewa ni ukatili wa hali ya juu sana kwa huyo mwanamke mbele ya wazazi wake.

NB: Natambua kazi nzuri anazozifanya waziri, maoni haya yasitoe taswira hasi ya mazuri yake.
 
Na siku idadi ya watu wapole, wavumilivu na wenye hekima ikupungua kwenye jamii, kinachofuata huwa ni vurugu.
 
Kama wakevi wana busara za kuzuia jazba kwa jambo zito kama hilo niseme tu pombe ni nzuri
 
Nimekusoma ila kama, tutafumbia macho watu wanaoepuka hasira nyakati ngumu, basi vita yetu ya kutokomeza ukatili bado pevu. Unakumbuka kule mwanza mwanaume mmoja alimpiga mke wake risasi saba kichwani kisa tu, simu iliita bila kupokelewa? Halafu naye akajiua.

Ndiyo mnapenda hivyo siyo?
 
Swali lingine kwako hili ndugu; huku kwenye ndoa tunaona watu wakiwa wanalewa huko hadi wanabebana na wake zao na waume zao. Unashaurije? Waachane?
 
Kama wakevi wana busara za kuzuia jazba kwa jambo zito kama hilo niseme tu pombe ni nzuri
Huyo alisha tambua kosa alilolifanya,ndio maana akawa mpole,hakuna cha busara hapo bali alitambua kosa lake,

Mtu mwenye akili timamu hata kama hua ni mlevi,ila hawezi kulewa chakari siku ya tukio kama hilo,hiyo ni dalili ya dharau kubwa sana kwa pande zote pamoja na wageni waalikwa,huyo mlevi alistahili kutandikwa viboko kwa kuiaibisha familia.
 
Heri nawe uchangie. Ina maana baada ya ndoa angekujwa bwi? Angeenda kuomba talaka au unachukua hatua za kutafuta ufumbuzi ajirekebishe honey wako?
 
Matukio ya ukatili yapo na ndo kazi mnayopambana nayo na kwa hilo Hongereni mno.

Lakini kumpa tuzo mlevi kwa sababu hajafanya ukatili naona haipo sawa. Ni sawa na kusema tumpe zawadi dereva mlevi kwa kuendesha gari akiwa amelewa na kulifikisha salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…