Kijana aliyetelekezwa na mke siku ya harusi atunukiwa tuzo ya mwanaume bora wa mwaka na Waziri Gwajima

Hilo tukio limenipa funzo moja hasa kwenye haya mambo ya michango ya harushi, yaani ni bora tujenge utamaduni wa kuchangishana na watu wachache unaofahamiana na ndugu wa karibu ili yanayotokea haya mnakaa sehemu mnapiga sherehe yenu inakuwa kama "get together party" flani hivi kwa kuwa mnafahamiana in person.

Sio utaratibu huu wa sasa unakuta robo tatu ya ukumbi hawana ukaribu na bwana na bibi harushi hata kufanya maamuzi ya michango Yao inakuwa ngumu
 
Hakuna mzazi atavumilia hiyo dharau. Unamkabidhi binti kwa mlevi? Serious? Kalewa chakari? Hata kuheshimu tu hiyo siku moja muhimu imeshindikana? Kama ni wazazi wameshinikiza Walikuwa sahihi kabisa. Kama wanapendana sana wakafunge ndoa bila hizi taratibu za sendoff.
 
Kulewa siku ya sendoff haikuwa jambo zuri,lakini huyo mwanamke hakupaswa kufanya alichokifanya.Huo ni mtihani tu katika mahusiano,kuna mengi zaidi na mabaya yatakuja kutokea mtakapokuwa tayari kwenye ndoa na yanahitaji kusamehe na kusuluhishana,sio kila likitokea baya unaamua kuvunja uhusiano...
 
Tumpe ushuhuda ana hali gani huyo
 
Pombe imesajiliwa na inalipiwa kodi toa ulokole hapa🤣
 
Kila kitu kina matokeo yake. Hata wewe ukilewa siku ya interview unaweka rehani ajira yako. Huyo kijana alipaswa kuwaheshimu wazazi wa binti. Hakuwaheshimu, wakaamua hivyo na binti yao akawasapoti. Ukumbuke Sherehe huwa ni za wazazi.
 
Swali lingine kwako hili ndugu; huku kwenye ndoa tunaona watu wakiwa wanalewa huko hadi wanabebana na wake zao na waume zao. Unashaurije? Waachane?
Hili swali nikiliongelea kwa misingi ya imani ya dini yangu,

Mke anaruhusiwa kuomba talaka kwa mume mlevi ambae ameshindwa kuacha ulevi,

Uamuzi wa familia ya mke mtarajiwa kumnyima mke huyo mume mlevi,ulikua ni uamuzi wa busara sana,huwezi kwenda kwenye tukio muhimu kama hilo ukiwa umelewa chakari,

Huyo mlevi alitakiwa apewe elimu kwa kosa alilofanya kwenye siku muhimu kama hiyo,ila bila shaka huyo mlevi alitambua kosa alilolifanya na ndio sababu kuu iliyomfanya awe mpole,angekua na busara asingelewa chakari siku muhimu kama hiyo,

Huu ni mtazamo wangu,Mimi kama Mimi.
 
Pombe imesajiliwa na inalipiwa kodi toa ulokole hapa🤣
Mm natumia Pombe. Nakunywa Camino dry au Absolute. Ila siku namkabidhi binti yangu halafu aniletee kijana kalewa eti nimkabidhi watafanya sherehe ya ndoa kwenye ofisi za serikali za mitaa ili wapewe na tuzo kabisa huko huko.
 
Yes. Nakubaliana na wewe kabisa Mh Waziri. Haya ni mambo mawili tofauti ambayo hayapaswi kuchanganywa.

Nina uhakika mchumba wake alifahamu fika kuwa mume wake mtarajiwa ni mnywaji. Na utamu wa pombe lazima mtu ulewe. Hili ndilo lengo hasa la pombe. Wanaosema kuwa hakupaswa kulewa huenda hawafahamu malengo ya uwepo wa pombe hapa duniani.

Kama mtu hajui maana na umuhimu wa pombe hapa nchini, aje nimuelimishe.
 
Swali lingine kwako hili ndugu; huku kwenye ndoa tunaona watu wakiwa wanalewa huko hadi wanabebana na wake zao na waume zao. Unashaurije? Waachane?
Juzi tu mke wangu kanifata nikiwa chakari nimeshindwa kuendesha gari ikabidi nimpigie aje nilipo. Hoja hapa si matumizi ya pombe, hoja ni Tuzo baada ya matumizi ya pombe sehemu isiyo sahihi.

Nikuulize, hapo wizarani kijana aje kwenye mkutano maalumu na mh Raisi wa Jamhuri ya muungano akiwa amelewa raisi akamfukuza kazi utampa tuzo sababu hakuchana mafile wakati anaondoka?
 
Good question
 
Huu mfano wa swali lako mbona umetoka nnje ya mada mkuu..
Usichanganye kazi na mapenzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…