Kijana aliyeuawa na watu wanaojiita Sungu sungu Mburahati, Rais Samia ingilia kati

Inaonyesha wewe hujawahi kukumbana na hao vibaka au wewe una hisa nao. Kwa taarifa yako sio binaadamu kabisa wakukuta katika anga zao za ukabaji, hawana huruma wala utu, sio wa kuhurumiwa kabisa, by the way kama ni mwanao pole , ila kumbuka methali 2 za wahenga:
1.Mchelea mwana kulia, hulia yeye.
2.Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.
 
Halaf hao kibaka ni hatari watoto wakike wamebakwa sana kinguvu na wengne kulawitiwa kabsa tena kinguvu na wanamchezo hao panya road wanaweza mvutia dem mmoja baadae wanampiga mtungo kilazima.
 
USSR nionenye kifungu Cha sheria kinachosema adhabu ya kibaka kuuawa
Kwani vibaka wao kuna vifungu vya sheria vinawaruhusu kuua?

Mbona wanaua watu na hamsemi na kuuliza maswali ya hivi?

Ninadhani kikubwa hapa kama mzazi ni jukumu lako kuchunga tabia na mwenendo wa kijana wako ili aishi kimaadili katika jamii.

Hili la kutetea vibaka kwamba watendewe haki wakati wao wakipora haki za wengine ni kupigia mbuzi gitaa ili acheze.
 
Vipi kuhusu uhai wako wewe au unaweza kutafuta mwingine?

Ukipigwa kisu mpaka kufa na mmoja kati ya hao mafala utaenda kununua uhai mwingine wapi?
 
Hance nioneshe sheria inayoruhusu sungu sungu waue?

Kijana huyu aliuawa barabarani baada ya kupigiwa simu
kuna wakazi wangapi eneo hilo mpaka wampigie simu yeye tu, inaonekana kwa vyovyote anahusika na hawa si wakuhurumia wanarudisha nyuma maendeleo watupishe mitano tena kazi iendelee
 
Daa, kweli vibaka ni tatizo, lakini walau wasiwaue kikatili namna hiyo, atandikwe bakora za kutosha then apelkwe kituo cha polisi, maana kule kituoni huwa wanaachiwa tu, so watandikwe kwanza bakora, ila sio kuwaua kikatili na namna hiyo
 
Kumbe ni kibaka mzoefu na amepata halali yake sasa huyu mama anamsumbua nini rais wakati Ana mambo ya msingi ya kufanya.
Jamani, tukubali tukatae, halali ya kila mwenye kosa ni kupelekwa kwwnye vyombo vya sheria, ila kwakua vibaka wanakera na polisi huwa wanawaachia, basi wapewe kichapo tu kama bakora za kutosha kisa wapelekwe polisi, ila kukatana mikono na miguu kisha kumuua nashani si ubinadamu
 
Naunga mkono hoja yako Brazaj kwamba jeshi la polisi liko kudhibiti vya vya siasa vya upinzani
Na wewe kama ni kibaka au umezaa kibaka na anakuletea mali za wizi nyumbani basi jiandae kuuawa ni siku tu haijasoma kwenye saa. Ndipo ulalamike kabisaa kuwa unamuomba Rais aingilie kati kwa wewe kuuawa na wananchi. Endelea na huu ujinga wako.
 
Mleta mada unajua ni damu ngapi zimemwaga na hao vibaka? Unajua wangapi wamepoteza Maisha sababu za hao vibaka?
Watu wamepoteza mali kiasi gani kwa kukabwa na hao vibaka?

Vibaka si watu wa kuwatetea hata kidogo dawa yao ni kuwamalizia mbali.
Wa kuwalaumu ni wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, maana mali na fedha zinazoibwa zote huishia kwao.
 

Kuua Ni vibaya Sana
 
USSR nionenye kifungu Cha sheria kinachosema adhabu ya kibaka kuuawa
Kikubwa mama ni kuishi kwa nidhamu katika jamii inayotuzunguka ili uheshimike na kuishi kwa amani.

Unajua kwa nini raia wanajichukulia sheria mkononi?

Ni kwamba kesi za vibaka mahakamani ni nyepesi sana kuliko uzito wa matukio na madhara wanayofanya, maana kuunganisha ushahidi usiotia shaka hadi kuwatia hatiani ni mgumu jinsi ya kupata vielelezo vya kutosha kutokana na mazingira ya namna wanavyofanya uhalifu.

Pia shata shata ya mahakamani kufuatilia kitu kisichokuletea manufaa ni kupoteza wakati na watu hudharau kufuatilia.

Kwa hiyo kesi zinapuuzwa na waliodhuriwa kushindwa kupata haki zao.

Sakata aina hii wa kwanza kulaumiwa hapa ambao ni chanzo, ni sisi wazazi tunavyodili na watoto zetu majumbani kwa kutofatilia nyendo zao ama kubariki matendo yao kwa kupokea na kufurahia vitu vya wizi wanavyopora na kuvileta nyumbani.

Kwa kuwa kila mtu anaelewa uchungu wa mwana uumizavyo akiuawa, hivyo mfiwa utaendelea kupewa pole za kebehi, lakini pembeni watu wakiendelea kuunga mkono kuuawa kwa kibaka husika.

Tuwalee watoto zetu kwa kuwafundisha maadili mema.
 
Muwe mnawapa malezi bora watoto wenu, na sio kutetea vibaka kisa ni watoto wenu.
Kazi nzuri sana wanafanya hao sungu sungu.
 
Hiyo ni sheria ya jamii au kwa kifupi ni sheria ya wananchi wenye hasira kali
Kwa mujibu wa sheria kuua kibaka ni kosa ila kwa mujibu wa haki siyo kosa
*Mwizi au jambazi anavunja SHERIA dhidi ya HAKI
* Je Mtu akivunja SHERIA kwa ajili ya HAKI kafanya kosa gani?
 
Bokilo,hiyo sheria ya nchi gani ya kuua vibaka? Jibu
Kwa mujibu wa sheria kuua kibaka ni kosa ila kwa mujibu wa haki siyo kosa
*Mwizi au jambazi anavunja SHERIA dhidi ya HAKI
* Je Mtu akivunja SHERIA kwa ajili ya HAKI kafanya kosa gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…