Miaka ya nyuma nilikuwa naishi huko 'waja leo waondoka leo', sasa kulikuwa na wezi hawa wa kudokolea watu wanasumbua kweli...
Siku moja akatiwa nguvuni na wananchi wenye hasira kali. Watu wakapiga yowe, "tumchomee, lete petrol, lete kiberiti, sijui lete tairiiii"...
Kuna Mpemba mmoja alikuwa mvuvi na mtengeneza yale majahazi ya uvuvi, Tanga wayaita madau...
Akawaambia watu "yakhhee niachieni huyo", jamaa akaingia ndani akatoka na msumari mmoja (waitwa msumari wa dau, ni kama ule aligongwa nao Yesu) na nyundo...
Basi, alipigwa msumari wa utosi hadi ukazama wote, halafu wakamuacha aende zake...
Huyo kibaka naye kwa sasa yupo kuzimu akiendelea na harakati za kupora vinyamkera huko...