Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Wazazi wa vijana wengi wa leo wanafanya maombi na kuwaombea vijana wao sana kila lililo jema wafanikiwe katika maisha yao, hakuna mzazi alie nyuma kwenye hili kwasababu mambo yamebadilika sana sasahivi...
Lakini vijana wengi wamedinda kabisa kurudi nyumba vijijini kwao, licha yakua wameshamaliza masomo miaka mingi imepita sasa, lakini bado wamekomaa tu mijini.
Ndiyo, wanawasiliana na wazazi wao vizuri tu kwamba hawajambo wanaendelea vizuri na maisha mjini,
Ila cha kushangaza vizinga vya hapa na pale kwa vijana hawa kwa wazazi wao huko vijijini haviishi, kila mara kijana akipiga simu nyumbani kijijini kwa wazazi, basi ujue amekwama anapiga kizinga cha kuomba chochote kitu kwa mama au baba kwaajili ya kujikimu kimaisha huko mjini wanako randaranda bila uelekeo tangu wamemaliza masomo miaka zaidi 8 au 10 iliyopita lakini ajira bilabila...
Baadhi ya wazazi wamebadili hata namna ya kuwaombea watoto wao, na sasa wanawombea vijana warudi vijijini kwao kwani viwanja walivyowatengea wajenge nyumba na mashamba vipo salama na vinawasubiri ..,
Rudini nyumbani kumenoga friends ladies and gentlemen,
Au mpaka ianzishwe kampeni ya, ewe kijana mzururaji mjini, rudi nyumbani kijijini kumenoga?
Msione aibu bana eti kisa tu wadogo zako na wale rafiki zako walioishia darasa la saba wana majumba na magari ya maana kijijini na wewe mwenye shahada hata hueleweki dah 🐒
Una maoni gani kuhusu hili ndugu mdau?
Mungu Ibariki Tanzania