Kijana baada ya kumaliza masomo yako mjini ni wakati wa kurudi nyumbani kijijini, wazazi wako wanakungoja

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Wazazi wa vijana wengi wa leo wanafanya maombi na kuwaombea vijana wao sana kila lililo jema wafanikiwe katika maisha yao, hakuna mzazi alie nyuma kwenye hili kwasababu mambo yamebadilika sana sasahivi...

Lakini vijana wengi wamedinda kabisa kurudi nyumba vijijini kwao, licha yakua wameshamaliza masomo miaka mingi imepita sasa, lakini bado wamekomaa tu mijini.

Ndiyo, wanawasiliana na wazazi wao vizuri tu kwamba hawajambo wanaendelea vizuri na maisha mjini,

Ila cha kushangaza vizinga vya hapa na pale kwa vijana hawa kwa wazazi wao huko vijijini haviishi, kila mara kijana akipiga simu nyumbani kijijini kwa wazazi, basi ujue amekwama anapiga kizinga cha kuomba chochote kitu kwa mama au baba kwaajili ya kujikimu kimaisha huko mjini wanako randaranda bila uelekeo tangu wamemaliza masomo miaka zaidi 8 au 10 iliyopita lakini ajira bilabila...

Baadhi ya wazazi wamebadili hata namna ya kuwaombea watoto wao, na sasa wanawombea vijana warudi vijijini kwao kwani viwanja walivyowatengea wajenge nyumba na mashamba vipo salama na vinawasubiri ..,

Rudini nyumbani kumenoga friends ladies and gentlemen,

Au mpaka ianzishwe kampeni ya, ewe kijana mzururaji mjini, rudi nyumbani kijijini kumenoga?

Msione aibu bana eti kisa tu wadogo zako na wale rafiki zako walioishia darasa la saba wana majumba na magari ya maana kijijini na wewe mwenye shahada hata hueleweki dah 🐒

Una maoni gani kuhusu hili ndugu mdau?

Mungu Ibariki Tanzania
 
Tatizo ujuaji mwingi. Vijiji vya sasa hv vina kila huduma ya jamii barabara nzuri umeme wa wakika,Maji safi kila eneo maeneo ya ibada yapo hakuna foleni za magari hali safi ya hewa maeneo ya kulima ya kutosha fursa za kuanza biashara ndogo ata ya milioni mbili zimejaa vijijini. Matokeo yake mtu anakaa mjini miaka 30 haeleweki anafanya nn chumba kimoja cha kupanga nacho nikama store. Hapana kwakweli. Alafu sasa wakija kwenye siku kuu wanataka kama ni ndugu zako wafikie kwako wewe uliyejiwai mapema ukawekeza kwenu maana hawana sehemu ata yakuweka mbavu zao mashamba yao yamekandiana.
 
Mimi nadhani ni vzr kwa kijana baada ya kumaliza masomo yake arudi nyumban walau wiki kadhaa kupata baraka za wazazi kabla hajazamia mjini kupambana na maisha.
Wazazi wengne wanaumia wanapoona mtt wao tangu amalize chuo hajawahi kanyaga nyumban tena.
Yawezekana mtu hafanikiwi kwakuwa mzazi ananung'unika kila siku kuwa hajamuona kijana wake miaka mingi.

#anywaymaishahayanafomula#
 
Vijiji vingi ni choka mbaya.
Mzunguko wa hela mdogo.
Hakuna taasisi wala mashirika.
Sasa wazazi gani hao wanamngoja mtu aliyehitimu chuo arudi kijijini..

Ili afanye nini huko kijijini badala ya kujitatuta mijini kwenye fursa zaidi.

Kijijini ni kupumzika tu, once in a while, kusalimia ndugu na jamaa na kutambika kwa wenye imani hii njema.
 
Wazazi wa vijana wengi wa leo wanafanya maombi na kuwaombea vijana wao sana kila lililo jema wafanikiwe katika maisha yao, hakuna mzazi alie nyuma kwenye hili kwasababu mambo yamebadilika sana sasahivi...

Lakini vijana wengi wamedinda kabisa kurudi nyumba vijijini kwao, licha yakua wameshamaliza masomo miaka mingi imepita sasa, lakini bado wamekomaa tu mijini.

Ndiyo, wanawasiliana na wazazi wao vizuri tu kwamba hawajambo wanaendelea vizuri na maisha mjini,

Ila cha kushangaza vizinga vya hapa na pale kwa vijana hawa kwa wazazi wao huko vijijini haviishi, kila mara kijana akipiga simu nyumbani kijijini kwa wazazi, basi ujue amekwama anapiga kizinga cha kuomba chochote kitu kwa mama au baba kwaajili ya kujikimu kimaisha huko mjini wanako randaranda bila uelekeo tangu wamemaliza masomo miaka zaidi 8 au 10 iliyopita lakini ajira bilabila...

Baadhi ya wazazi wamebadili hata namna ya kuwaombea watoto wao, na sasa wanawombea vijana warudi vijijini kwao kwani viwanja walivyowatengea wajenge nyumba na mashamba vipo salama na vinawasubiri ..,

Rudini nyumbani kumenoga friends ladies and gentlemen,

Au mpaka ianzishwe kampeni ya, ewe kijana mzururaji mjini, rudi nyumbani kijijini kumenoga?

Msione aibu bana eti kisa tu wadogo zako na wale rafiki zako walioishia darasa la saba wana majumba na magari ya maana kijijini na wewe mwenye shahada hata hueleweki dah 🐒

Una maoni gani kuhusu hili ndugu mdau?

Mungu Ibariki Tanzania
sept 23 maandamano ya amani yapo palepale kulaani mauaji na utekaji tanzania, wacha vijana waishi popote wameshakuwa watu wazima,wakiwa nyumbani munawaita mizigo
 
Vijiji vingi ni choka mbaya.
Mzunguko wa hela mdogo.
Hakuna taasisi wala mashirika.
Sasa wazazi gani hao wanamngoja mtu aliyehitimu chuo arudi kijijini..

Ili afanye nini huko kijijini badala ya kujitatuta mijini kwenye fursa zaidi.

Kijijini ni kupumzika tu, once in a while, kusalimia ndugu na jamaa na kutambika kwa wenye imani hii njema.
unajua tatizo tangu umehitimu chuo 2015, gentleman hakuna sehemu ni kijijini tena kama ulivyoondoka miaka ya 2000 gentleman 🐒
 
Majumba na magari ya maana vijijini? Vijiji hivi hivi vya Tanzania 😀😀
mmeng'ang'ana town ndugu akikupigia simu na kukujulisha yupo po mjini leo, anataka aje akutembelee, unamruka utadhani anakudai dah 🤣

visingizio kibao,
mara ooh nimesafiri kidogo, ntakupigia baadae, mara ooh niko bize ntakucheki subiri kidogo

kumbe geto lako la mjini ni vichekesho na aibu na tayari una 20yrs uko town,

wakati anaekupigia ni bwanamdogo tu ulimuacha shule ya msingi na aliishia hapo hapo, anakwambia kaja kufunga mzigo kwajili ya duka lake 🤣
 
sept 23 maandamano ya amani yapo palepale kulaani mauaji na utekaji tanzania, wacha vijana waishi popote wameshakuwa watu wazima,wakiwa nyumbani munawaita mizigo
maandamano ya waliogoma kurudi vijijini sio?
dah ila aibu sana aise geto la jamaa msomi wa miaka 35-40 town linatia huruma sana aise, na kazi hana anatamani kila aina ya maandamano 🤣

stress ni kitu mbaya sana aise
 
Turudi nyumbani tukaangaliane na wazazi...tuache kwanza tupige uwinga tutaendaga tu
wazazi wengi vijijini wamewandalia vijana wao waliowatuma masomoni mijini viwanja vya kujenga miji yao lakini na mashamba makubwa kwajili ya kilimo...

halafu sasa hivi,
wazizi wengi wanaskia uchungu sana kwamba kijana kaenda kusoma mjini miaka10 iliyopita, hana kazi, hana plot, hana mjukuu ni vizinga tu, wakati watoto wa majirani zao ambao hawakusoma wanakula maisha balaa wanamiliki majumba hadi mijini pia dah,

huruma sana aise,
unaulizia rafiki zako uliosoma nao shule ya msingi unaambiwa, aah jamaa alinunua nyumba wilayani huku anakujaga shamba tu,

wakati wewe unatakiwa kulipa kodi na mwenye nyumba kaishakupigia mara 4 na sms kibao, aise!🐒
 
Ni wazazi wachache sana wameandalia future vijana wao....wengi wetu tunasubiriwa na wazazi tuwatumie hela ya sukari
 
aise,
muwe mnatuma kweli basi hiyo sukari, sio tena nyie ndio mnawapiga vizinga wazazi dah!

nikiwa mjini siku zingine hapo nyuma,
nimemsika dada moja muhitimu wa chuo kikuu hapo mjini, amehitimu miaka 4 iliyopita yuko nyumbani hana cha kufanya ,

siku hiyo,
akawa anabishana na mamake mzazi kwa uchungu sana,
na akamwambia mamake kwamba amechoka kua housegirl wa nyumbani kwao dah! ilinishangaza sana kwakweli...

nikajiuliza hivi kama familia hii ingekua na mashamba pangekua na mabishano ya aina hii kweli ?
huenda angeambiwa kabishane na shamba maana sasa mama atafanyaje?🐒
 
Back
Top Bottom