Kijana mkoani Kilimanjaro auawa kwa panga kwa madai ya kutaka kushiriki tendo la ndoa na mke wa mtu

Mkazi wa kijiji cha Kibaoni wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro, Juvenal Claudi (20) ameuawa kwa kukatwa katwa na mapanga baada ya kufumaniwa akitaka kufanya mapenzi na na mke wa mtu.

Taarifa zinadai kuwa kijana huyo aliyeuawa alikuwa akichati na mke wa mtu ambapo baadaye mume wa mwanamke huyo, Riziki Shirima (22) alidaka simu ya mkewe na kukuta meseji za mapenzi.

Baada ya kukuta meseji hizo, mwanaume huyo aliweka mtego kwa kuendelea kumtumia meseji kijana huyo aliyeuawa, akijifanya yeye ndio mwanamke huku akimtaka kuja nyumbani jambo ambalo alifanya hivyo.

Baada ya kijana huyo kufika nyumbani alianza kushambuliwa kwa kukatwa mapanga na baadaye kufariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoani wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio ambapo amesema tukio lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 4 na kusema baada ya mwanaume huyo kufanya mauaji alijisalimisha mwenyewe polisi.

"Ni kweli hili tukio limetokea katika kijiji cha Kibaoni wilaya ya Rombo ambapo mwanaume alimfumania mkewe nyumbani kwake akiwa na huyu kijana aliyeuawa wakitaka kufanya mapenzi," amesema Kamanda Maigwa

Kamanda Maigwa amesema jeshi la polisi linaendelea kumshikilia muuaji baada ya kujisalimisha mwenyewe polisi.

Chanzo cha Habari ni Mwananchi online
hivi wchaga nao mapenzi wameanza lini aisee.
 
Unaenda jela, mke wako anabaki akiliwa kwa uhuru.

Busara inaepusha mengi sana.
mi niliuliza swali hapo lini wachaga nao wameanza mapenzi? manake hiyo hata sio carrier yao. rip dogo.

though tukiacha utani, shetani ni mbaya sana, ni kama mvuvi wa samaki, anaweka chambo kwenye ndoana ili akikuvua akumalize kabisa usitubu ili ukateketee motoni pamoja naye. kijana alipelekwa chambo cha mwanamke bila kujua kama shetani anataka kuchukua maisha yake, na amefariki bila hata kumrudia Mungu. tujifunze kujua kuwa uzinzi ni wa shetani na wazinzi wote hawataurithi ufalme wa Mungu.
 
Mkazi wa kijiji cha Kibaoni wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro, Juvenal Claudi (20) ameuawa kwa kukatwa katwa na mapanga baada ya kufumaniwa akitaka kufanya mapenzi na na mke wa mtu.

Taarifa zinadai kuwa kijana huyo aliyeuawa alikuwa akichati na mke wa mtu ambapo baadaye mume wa mwanamke huyo, Riziki Shirima (22) alidaka simu ya mkewe na kukuta meseji za mapenzi.

Baada ya kukuta meseji hizo, mwanaume huyo aliweka mtego kwa kuendelea kumtumia meseji kijana huyo aliyeuawa, akijifanya yeye ndio mwanamke huku akimtaka kuja nyumbani jambo ambalo alifanya hivyo.

Baada ya kijana huyo kufika nyumbani alianza kushambuliwa kwa kukatwa mapanga na baadaye kufariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoani wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio ambapo amesema tukio lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 4 na kusema baada ya mwanaume huyo kufanya mauaji alijisalimisha mwenyewe polisi.

"Ni kweli hili tukio limetokea katika kijiji cha Kibaoni wilaya ya Rombo ambapo mwanaume alimfumania mkewe nyumbani kwake akiwa na huyu kijana aliyeuawa wakitaka kufanya mapenzi," amesema Kamanda Maigwa

Kamanda Maigwa amesema jeshi la polisi linaendelea kumshikilia muuaji baada ya kujisalimisha mwenyewe polisi.

Chanzo cha Habari ni Mwananchi online
Kama mwanaume ndiye aliyekuwa anamtumia meseji akijifanya ndiye mwanamke, imekuwaje tena awafumanie wakitaka kufanya mapenzi? Si kwamba alikuwa akimsubiri yeye mwenyewe?
 
hahahahaha Aisee inasikitisha mbususu yenyewe usikute hakukuta hata sio bikra na utashangaa jamaa aliyeuwawa Ndio alitangulia kuichakata na hapo alikua anapasha kiporo tu sema Ndio bahati mbaya Haina mwenyewe kaisha!

Utachukuwaje mke wa mtu!!! Huo ni upumbafu haswaaaaa. Na huyo alieuwa ajiandae washkaji hawatamkalia kimya 🤣
 
Huyo dogo aliye uwawa na muuaji wote ni mafala wakutupwa. Mmoja kafa na mwingine anakwenda kuozea lupango. huku walimwengu wakiendelea kujitwalia kisababishi
 
Back
Top Bottom