Kijana mwenzangu focus na kilichokuleta mjini, mambo ya mjini waachie watu wa mjini

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2021
Posts
2,753
Reaction score
12,932
Nsikuchoshe na Usinchoshe, kwa kifupi tusichoshane!.

Kijana mwenzangu napenda kukupa ushauri wa bure kabisa.

Ushauri napenda kuwapa vijana (KIKE & ME) ambeo umetoka mkoani kuja mjini Dar es salaam kwa ajili ya kutafuta fedha,hapa mjini hatujaja kutafuta maisha,maisha hata mikoani yapo tena mazuri mno kushinda hata hapa mjini,ila hapa mjini wengi wetu tumekuja kutafuta pesa.Kama umekuja mjini kutafuta Pesa hakikisha unaitafuta kwa nguvu zako zote,kwa akili zako zote na kwa moyo wako wote.

Kumekuwa na wimbi la vijana kutoka Km za kutosha huko mkoani na kufika mjini kutafuta pesa,badala yake wamekuwa waki-adapt maisha ya mjini na wakisahau kilichowaleta.

Yaani unatokea huko Bukoba Takribani Km 1400 unakuja mjini unashindwa kutafuta pesa unaanza kulilia mwanamke?

Yaani unatoka Mkoa wa Mwanza takribani Km 1100 unakuja mjini kushinda vijiweni kushadadia Usimba na Uyanga?

Yaani Unatoka huko mkoani Mara zaidi ya Km 1200 kuja mjini Dar es salaam kutembea na wake za watu?

Yaani unatoka Arusha huko zaidi ya Km 620 unafika mjini kutwa kushinda kwenye ma-bar?

Kama umetoka Km zote hizo na ufahamu kilichokuleta mjini ni afadhali ukarudi mkoani ukaendelee na maisha kwasababu ukiendelea kukaa mjini utaendelea kusononeka kuwaona wenzio wakiishi maisha mazuri.

Wenzio kila weekend wanashinda Kitambaa cheupe kwasababu wanauhakika wa maisha,wengi wamejenga na wanausafiri wao binafsi,sasa wewe mwenzangu na mie ukipata elfu 20 kwenye hako ka-Bajaji kako au ka-bodaboda na wewe unataka ukaweke heshima Kitambaa cheupe,hivi zinakutosha kweli?

Vijana acheni tamaa pambaneni mtafute pesa,hivi vi starehe uchwara mkiviendekeza vitawapotezea muda,wakati wewe unafanya starehe uchwara mjini huku ukiwa umepanga kumbuka mkoani kuna kijana mwenzio kajenga nyumba na anaishi kwake.

Waacheni watu wa mjini na mji wao,nyie wakuja tafuteni pesa!.

Ni hayo tu.
 
Hakika mkuu umeshusha ushauri mzuri Sana,atakayeutilia maanani bila Shaka atafanikiwa.

Sema watakuja kukwambia usiwapangie maisha yao.
 
Mkuu hii ni dawa,mgonjwa akiwa serious akinywa atapona!
 
Kama amefuata wanawake wa Dar na kwenda kupaona kidimbwi je? Usipangie watu maisha yao.
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe, kwa kifupi tusichoshane!.

Kijana mwenzangu napenda kukupa ushauri wa bure kabisa.

Ushauri napenda kuwapa vijana (KIKE & ME) ambeo umetoka mkoani kuja mjini Dar es salaam kwa ajili ya kutafuta fedha,hapa mjini hatujaja kutafuta maisha,maisha hata mikoani yapo tena mazuri mno kushinda hata hapa mjini,ila hapa mjini wengi wetu tumekuja kutafuta pesa.Kama umekuja mjini kutafuta Pesa hakikisha unaitafuta kwa nguvu zako zote,kwa akili zako zote na kwa moyo wako wote.

Kumekuwa na wimbi la vijana kutoka Km za kutosha huko mkoani na kufika mjini kutafuta pesa,badala yake wamekuwa waki-adapt maisha ya mjini na wakisahau kilichowaleta.

Yaani unatokea huko Bukoba Takribani Km 1400 unakuja mjini unashindwa kutafuta pesa unaanza kulilia mwanamke?

Yaani unatoka Mkoa wa Mwanza takribani Km 1100 unakuja mjini kushinda vijiweni kushadadia Usimba na Uyanga?

Yaani Unatoka huko mkoani Mara zaidi ya Km 1200 kuja mjini Dar es salaam kutembea na wake za watu?

Yaani unatoka Arusha huko zaidi ya Km 620 unafika mjini kutwa kushinda kwenye ma-bar?

Kama umetoka Km zote hizo na ufahamu kilichokuleta mjini ni afadhali ukarudi mkoani ukaendelee na maisha kwasababu ukiendelea kukaa mjini utaendelea kusononeka kuwaona wenzio wakiishi maisha mazuri.

Wenzio kila weekend wanashinda Kitambaa cheupe kwasababu wanauhakika wa maisha,wengi wamejenga na wanausafiri wao binafsi,sasa wewe mwenzangu na mie ukipata elfu 20 kwenye hako ka-Bajaji kako au ka-bodaboda na wewe unataka ukaweke heshima Kitambaa cheupe,hivi zinakutosha kweli?

Vijana acheni tamaa pambaneni mtafute pesa,hivi vi starehe uchwara mkiviendekeza vitawapotezea muda,wakati wewe unafanya starehe uchwara mjini huku ukiwa umepanga kumbuka mkoani kuna kijana mwenzio kajenga nyumba na anaishi kwake.

Waacheni watu wa mjini na mji wao,nyie wakuja tafuteni pesa!.

Ni hayo tu.
Kuna vijana wengi tu wanakuja Dar ili wapate maeneo mazuri ya kuvinjari, unafikiri vijana wote wa mikoani ni kapuku, la hasha wengine wengi wapo Dar kutafuta starehe, fedha ipo na nyumba tayari wanazo.
 
Kama ndivyo sawa
 
Nimetoka Arusha hapa nasikia kidimbwiii nataka nishukie hapo kwanza ndio niende nyumbani, vipi hata bia moja nisipate
 
Kuna vijana wengi tu wanakuja Dar ili wapate maeneo mazuri ya kuvinjari, unafikiri vijana wote wa mikoani ni kapuku, la hasha wengine wengi wapo Dar kutafuta starehe, fedha ipo na nyumba tayari wanazo.
Kwenye mia yupo mmoja
 
Huu ushaur haina haja ya kuwaambia watumishi wa serikali haswa walim huwa wanajijua na wanaishi maisha mazur sn hata kama wametoka mkoani
 
Back
Top Bottom