Kijana usiwe kataa ndoa ni hatari inafupisha maisha

Kijana usiwe kataa ndoa ni hatari inafupisha maisha

Wanawake wakizungu wenyewe wameshashtuka tukiwa single tunakula maisha zaidi😅
Screenshot_2026-07-05_064104.jpg
 
Mimi pia ni kataa ndoa na wengi humu wanajua hili ila ukweli nitausema.

Ishu ya kataa ndoa ilianzia mitandaoni ila ishafika mitaani na vijana wameanza kuhubiriana na ninaiona hatar kubwa.Huu ukiwa utamaduni maisha ya wanaume wengi yataharibika na single maza wataongezeka sbb kataa ndoa wanataka watoto ila hawataki ndoa.Hivyo kataa ndoa ni laana Itakayoharibu maisha ya mwanaume,mwanamke(kuwa singo maza) na ya mtoto (kukosa malezi ya wazazi wote wawili ni hatari)

Kwenye bandiko nililoeleza kuwa mimi ni kataa ndoa nilisema ni kwa sababu nahofia nikiolewa kisheria italeta shida kwenye masuala ya tumali twangu iwapo nitatalikiwa ila kwenye hilo bandiko nilisema naamini ndoa ni kitu kizuri wawili wafananao wakapendana na kuishi pamoja.

Mimi kwa sasa ni 'mke' wa mtu ila sina cheti cha ndoa ila natimiza wajibu wote wa mke mwema kwa 'mume' wangu kipenzi❤️ na siioni tofauti yeyote kati yangu na wale wake wenye vyeti vyao kabatini na nina 'a very happy marriage life '. na niseme tu maisha haya yamenibadilisha kwa namna nyingi nzuri.Maisha ya wawili ni matamu asikudanganye mtu.

Kwa hiyo utaona kwamba mimi ni kataa ndoa nisieishi maisha ya upweke.Maisha ya nyeto na maisha ya kufia mwenyewe chumbani.Hii ndio aina ya kataa ndoa ninayowaonya nayo vijana.

Kijana ,ukitaka kuwa kataa ndoa kuwa kama mimi.Naelewa dhulma ya Mali itokanayo na ndoa ila usiishi mwenyewe.Binadamu ni mnyama wa kuishi kimakundi.Tafuta mwenza mnaeendana na kupendana then ishini sogea tukae style.

Studies zinaonesha watu wenye ndoa huishi maisha marefu kuliko wale wanaoishi wenyewe.Unajua ni kwa nini?Ni kwa sababu sio wapweke.

Upweke ni ugonjwa.Upweke huleta stress then depression.Unhealthy mind husababisha unhealthy body.Upweke huleta hadi magonjwa ya moyo na stroke.

Kijana,leo hii sio rahisi kuuhisi upweke sbb una kampani ya marafiki wa kwenda kula nao bia na good times ila kuna umri utafika rafiki zako wote wataoa na kila utakayempigia mkale bata hatatokea sbb ya dharura ilotokea kwenye familia yake.

Licha ya hivyo,hata wewe kuna umri utafika zile bata zilikua zinakufurahisha utaziona ni mateso tu.Utatamani uchill zako home na hapo ndo upweke utaanza process za kufupisha maisha yako.Wakati wenzako wakiwa wana cuddle na wenza wao wewe utashinda mitandaon kujifariji.Wateja wengi wa mitandao ni watu wapweke na wenye stress za upweke.Yaani unhappy people.Utakutana na post zao wameziandika usiku mzito.Mida ambayo wanandoa hubebishana jambo ambalo hufanya miili yao kitengeneza hormones nzuri zenye kuchochea furaha na furaha ni kinga ya stress na magonjwa.

Juzi kati kuna kataa ndoa kama sio fundi wake kwenda nyumbani kwake kuchukua vifaa vyake alivyovisahau angekufa.Kakutwa hoi hawezi hata kushika simu.Huyu kataa ndoa ana pesa chafu ila anaishi mwenyewe kwenye bonge ya jumba.


Thank you for your attention to this matter🙏
Kwani ndoa ni nini tuanzie hapo.Tafsiri iwe ya kisheria ili tuanze kuchangia mada yako.
 
Kama ni mwanamke, wewe ni kiraka tu. Mchepuko. Kama ni mwanaume, wewe ni buzi tu. Coward. Huna sababu ya kuigiza maisha wanayoishi wanandoa halali. Badala ya kuwaza future na umoja na familia wewe unawaza ubinafsi na mali
 
Kwasababu sio haki kugawa mali ambayo haujashiriki kuitafuta. Mchakato wa kupata mali unaweza kuhusisha watu wengi wengine ila mali zikawa kwa jina lako Denoo. Mali kama hii itaguswaje during divorce?

Mfano mzuri mimi nimesaidiwa kujenga nyumba na mama yangu… Kwenye mali yangu kuna jasho la mzazi wangu ambaye si mzazi wa Mume wangu. Practically inaweza kumuhusu tukiwa tumeoana mfano tunapokea kodi, ila haiwezi muhusu tukiachana.

Simple.

Sheria zina maana nyuma yake.
Ndoa kwangu naichukulia kama jambo la kiroho zaidi, najua wenzangu mna mitazamo yenu tofauti ndio maana mnaichukulia ndoa kama issue flani tu!.

Sioni sababu kwanini uogope kutoa mali kwa familia ambayo tayari una damu yako [watoto] hata kama mali hiyo ulipewa na mama yako mzazi bila kuwepo mumeo.

▪ Hakuna mama anayeweza kasirika akiambiwa na binti yake ile nyumba uliyonipa nimeitoa kwa wajukuu zako, hayupo!.

Kwenye ndoa tunazungumzia muunganiko wa wawili kuwa mwili mmoja, sasa kwanini kanisani mjiite "mwili mmoja" wakati vichwani mwenu mali zenu hamtaki ziwe za familia? Utapeli.

Hapa kuna tatizo kwenye mindset, na nakubaliana na prida 100% watoto wa kike wengi mnazitaka ndoa kama maonesho, muitwe wake za watu, mheshimiwe na jamii iliyowazunguka, lakini kiuhalisia hamjitoi 100% kwa ajili ya hizo ndoa zenu.

Kwa hii mentality yenu, basi nina hakika wale kataa ndoa wataendelea kusimamia misimamo yao, nyie mnaingia kwenye ndoa na mindset ya kitapeli, ya kibinafsi kuficha mali zenu.

Bora muolewe na hizo mali zenu wallah ndoa zenu zitadumu, na mtazitumikia kwa 100%
 
Unfortunately comprehension is rocket science for you. Huwa una manage vipi kumlisha mtu maneno ambayo hajayasema. Rudi kwenye comment yangu ya kwanza nimesema inaweza kumhusu katika circumstance ipi (nimetaja labda tunapokea kodi) na inaweza isimuhusu katika circumstance ipi (divorce)

Sizingumzii hisia nazungumzia sheria.

Ukitwist maneno yangu tena sitajibu……
Sasa nimetwist maneno wapi?
Kwani divorce sio kuachana?
Nime kuuliza kama sisi wanaume tungekuwa tu nakuja na hii mentality yako ingekuaje?
 
Ndoa kwangu naichukulia kama jambo la kiroho zaidi, najua wenzangu mna mitazamo yenu tofauti ndio maana mnaichukulia ndoa kama issue flani tu!.

Sioni sababu kwanini uogope kutoa mali kwa familia ambayo tayari una damu yako [watoto] hata kama mali hiyo ulipewa na mama yako mzazi bila kuwepo mumeo.

▪ Hakuna mama anayeweza kasirika akiambiwa na binti yake ile nyumba uliyonipa nimeitoa kwa wajukuu zako, hayupo!.

Kwenye ndoa tunazungumzia muunganiko wa wawili kuwa mwili mmoja, sasa kwanini kanisani mjiite "mwili mmoja" wakati vichwani mwenu mali zenu hamtaki ziwe za familia? Utapeli.

Hapa kuna tatizo kwenye mindset, na nakubaliana na prida 100% watoto wa kike wengi mnazitaka ndoa kama maonesho, muitwe wake za watu, mheshimiwe na jamii iliyowazunguka, lakini kiuhalisia hamjitoi 100% kwa ajili ya hizo ndoa zenu.

Kwa hii mentality yenu, basi nina hakika wale kataa ndoa wataendelea kusimamia misimamo yao, nyie mnaingia kwenye ndoa na mindset ya kitapeli, ya kibinafsi kuficha mali zenu.

Bora muolewe na hizo mali zenu wallah ndoa zenu zitadumu, na mtazitumikia kwa 100%
Sawasawa.

Mengine tuyaache sikuwa huko.

Mkioana mali ni zenu, mkizeeka pamoja mali zitakuwa urithi wa watoto, mkiachana mali mlizochuma before ndoa huwa hazigawanywi.

Kwaheri Denoo, leo hautanikausha maji 😂
 
Sasa nimetwist maneno wapi?
Kwani divorce sio kuachana?
Nime kuuliza kama sisi wanaume tungekuwa tu nakuja na hii mentality yako ingekuaje?
Gunner unajua unachokitetea hapa kikitekelezwa kisheria kitawaramba wanaume kuliko wanawake? unadhani wanawake wangapi wana mali ukilinganisha na wanaume?

Unless haujajua unachotetea na haujajua unachonipinga.

Nashukuru haujachezesha hii comment 😅😅
 
Sawasawa.

Mengine tuyaache sikuwa huko.

Mkioana mali ni zenu, mkizeeka pamoja mali zitakuwa urithi wa watoto, mkiachana mali mlizochuma before ndoa huwa hazigawanywi.

Kwaheri Denoo, leo hautanikausha maji 😂
Naona bora wawili hasa huku mijini waishi kisela tu, kama hivyo mleta mada alivyosema hapendi upweke.

Kuliko kufunga ndoa za maigizo huku kila mmoja akiwa na mawazo yako tofauti.

Au kama issue ni uzee, basi mngesubiri mzeeke ndio muolewe ili mtoe mali zenu kwa watoto!.

Kuwa na amani mdada!.
 
Gunner unajua unachokitetea hapa kikitekelezwa kisheria kitawaramba wanaume kuliko wanawake? unadhani wanawake wangapi wana mali ukilinganisha na wanaume?

Unless haujajua unachotetea na haujajua unachonipinga.

Nashukuru haujachezesha hii comment 😅😅
Wewe bado ego inakusumbua.😅
Unajua fika nyie ndo mtaumia.
Najua hata nikueleweshe vipi hautaelewa
 
Huwa nasoma hili humu mara nyingi naelewa kuwa watu wengi hawajawahi kuwa kwenye kesi za divorce. Kuna mtazamo wa jumla jumla ati ya kuwa kila mali hugawanywa ni upotoshaji.

Hata mali za ndoa pia hazigawanywi kibabe na mahakama, ni mpaka wanandoa /wanaovunja ndoa wakubaliane, ndio maana wasipokubaliana kesi inaenda miaka na miaka.

Mahakama si mgawa mali bali mhakikisha mali zinagawanywa kwa haki. Kama kuna divorce lawyer humu aje atupe muongozo zaidi.

Tuko nje ya mada ya Prida tho.
Mali za kabla ya ndoa hazigawanywi lakini kuna kitu wengi hawakijui. Hili mali hizo zisiletwe kwenye mgao zinatakiwa kuwa vile vile kama ambavyo zilikua wakati mnafunga ndoa. Mfano nimejenga nyumba kabla ya kumalizia kupiga rangi nikafunga ndoa. Masuala mengine kama rangi, tiles, ukuta nikamalizia nikiwa ndoani. Hapo kwenye divorce settlement hiyo nyumba italetwa kwenye mgao kwa sababu imeongezeka thamani nikiwa ndoani.

Niwe na duka, kampuni, kiwanda n.k mali husika inatakiwa ibaki vile vile ili isiletwe kwenye mgao. Ukiiongezea thamani mtu kiwanda ukaongeza ukubwa wa uzalishaji au kampuni ukafungua matawi mengine. Mali inaletwa kwenye mgao.

McKenzie Scott akiolewa na Bezos wakati ambao Amazon tayari ishaanzishwa na walibyotalakiana McKenzie akapata mgao wake kwa sababu Amazon ilikua kubwa tofouti na wakati wanafunga ndoa
 
Hata hujatoka nje sana.
Hebu shusheni nondo tujifunze ukute nashindwa kutimiza ndoto yangu ya kuvaa shela kwa kutokua na elimu sahihi.

Kataa ndoa wengi wanakufa vibudu kwa upweke kwa kuhofia tumali twao.
KIlio kikubwa cha kataa ndoa ni kutapelewa mali na wanawake.Wanasema ni scam.
Ni utapeli.
Ni laana.
Ni biashara ya wanawake.

Pia elimu yakutosha itasaidia wanawake wanaoolewa kuvizia mali wajue kuna uwezekano wa kuingia na mawigi na kutoka na mawigi hivyo wakiingia waingie kwa mapenzi na sio kwa nia nyingine ovu.
Tunakataa ndoa sio kwa sababu ya mgao wa mali tu, tunakataa ndoa kwa sababu mfumo wa mzima ukiufanyia tathmini na maisha ya sasa unaona hakuna faida iliyobaki kwa ajiri ya mwanaume uko kwenye ndoa.

Modern marriage demand traditional sacrifices from men, while removing nearly every traditiinal benefit that once came with it

-mwanaume anatakiwa kuprovide lakini asiwe na mamlaka juu ya mwanamke(mnaita uswa aa kijinsia)

-ndoa za kisasa ni presha na stress kwa mwanaume, sio amani

-risk to reward ratio haiingii akilini. Nitumie maisha yangu yote kutafuta hela, kujenga himaya yangu na future yangu only to lose half of it through one emotional decision. Tottaly bullshit.

-mwanaume anatakiwa kujitoa wakati wanawake wanaambiwa wajipe kipaumbele wenyewe.

Zaidi ya mgao wa mali zipo sababu nyingi sana za wanaume kuachana na suala ndoa.
 
Mali za kabla ya ndoa hazigawanywi lakini kuna kitu wengi hawakijui. Hili mali hizo zisiletwe kwenye mgao zinatakiwa kuwa vile vile kama ambavyo zilikua wakati mnafunga ndoa. Mfano nimejenga nyumba kabla ya kumalizia kupiga rangi nikafunga ndoa. Masuala mengine kama rangi, tiles, ukuta nikamalizia nikiwa ndoani. Hapo kwenye divorce settlement hiyo nyumba italetwa kwenye mgao kwa sababu imeongezeka thamani nikiwa ndoani.

Niwe na duka, kampuni, kiwanda n.k mali husika inatakiwa ibaki vile vile ili isiletwe kwenye mgao. Ukiiongezea thamani mtu kiwanda ukaongeza ukubwa wa uzalishaji au kampuni ukafungua matawi mengine. Mali inaletwa kwenye mgao.

McKenzie Scott akiolewa na Bezos wakati ambao Amazon tayari ishaanzishwa na walibyotalakiana McKenzie akapata mgao wake kwa sababu Amazon ilikua kubwa tofouti na wakati wanafunga ndoa


Asante kwa kutuongezea hilo sikuwa nalifahamu (kwa reference niliyokuwa nimejifunzia hii kitu) Tuko pale pale mali kabla ya ndoa hazigawanywi, unless under circumstance kama hizo ulizozitaja.

Mfano wako; I hope haikuwa 50/50 tho ndio maana Amazon hadi sasa bado ipo. Mimi mtu yoyote kupata mgawo ni valid kwangu, tuki validate kwa kutumia muda na eneji (moral &material)
 
Huwa nasoma hili humu mara nyingi naelewa kuwa watu wengi hawajawahi kuwa kwenye kesi za divorce. Kuna mtazamo wa jumla jumla ati ya kuwa kila mali hugawanywa ni upotoshaji.

Hata mali za ndoa pia hazigawanywi kibabe na mahakama, ni mpaka wanandoa /wanaovunja ndoa wakubaliane, ndio maana wasipokubaliana kesi inaenda miaka na miaka.

Mahakama si mgawa mali bali mhakikisha mali zinagawanywa kwa haki. Kama kuna divorce lawyer humu aje atupe muongozo zaidi.

Tuko nje ya mada ya Prida tho.
swadakta,mimi kuna kesi niliisimamia mwanamke alihonga mara kadhaa mwisho akaangukia pua hata mia mbofu,na alimkuta jamaa na kila kitu akasoma walishiriki kujenga alikuwa anatuma hela na alikuwa rombo ndani hukoo
 
Unaona sasa ndio maana nakwambia wewe ni mamluki.Kataa ndoa ni chama cha kipekee sana kipo decentralized wanachama ni selfcentered hawana njaa hiki chama hakijawahi kuchangisha hata thumni.

Humu kuna matajiri akina Jeff Benzo,Cr 7,Elon mask,Bill gate kajiugha juzi.Matajiri huku ni wengi na hakuna ombaomba.


Chama kina matawi dunia nzima na hakuna shobo za rejareja mikutano yetu tunafanya zoom.

Hizo hela uliwachangisha akina nani,acha utapeli wewe chama kina misingi imara na hakuna kima wakuibadilisha.

Wewe huna itikadi ni bendera fata upepo ukiwa na nyege unakimbilia kwa boyfriend( ambaye unamuita mume) ukiwa na makasiriko unajiita kataa ndoa.

Huku watu wapo na EMOTIONAL INTELIGENCE YA HALI YA JUU MNO.Mambo ya upweke unapataje wakati unashughuli za kufanya na ratiba tight.Na ukitaka kimasihara unalipia chapu unafanya yako unaendelea na mambo ya msingi.

Kataa ndoa hawana nyege mshindo,wanajimudi kipesa so kwao mapenzi sio ajira wala hisani ni starehe kama starehe nyingine.

📌KATAA NDOA HATUKUTAMBUI, WEWE TAFUTA PAKUFIA!!!
Iam the boss😃
 
me nina experience direct na watu wazima ambao hawakuoa kabisa kwenye ujana wao. They regret nothing. They are living their best life currently. Upweke ni wewe mwenyewe unavyou-define.
Hapana upweke sio vile unavyou define.
Ni hali inakuja automatic kutokana na sbb kadha wa kadha
 
Hapana upweke sio vile unavyou define.
Ni hali inakuja automatic kutokana na sbb kadha wa kadha
Jamaa kajua kukukamata yaani sogea tukae lakini unaamani na furaha hivyo siku mkifunga ndoa sijui itakuwaje inaonekana ulikuwa mpweke sana.
 
Back
Top Bottom