Kuna jamaa mtaani kwetu,alioa na kujaaliwa kupata mtoto mmoja, kwa mujibu wa maelezo yake alisema kabla ya kutoweka "mimi na mkewangu baada ya kupata mtoto,mke wangu alinambia,kutokana na ugumu wa maisha naomba mume wangu tuwe tunatumia condom ili kuepukana na mimba nyingine,inatakiwa huyu mtoto tuliyempata akue angalau afikishe miaka 5", kweli jamaa akakubali,pilika zikaendelea,wanatumia condom wakati wa tendo,lakini cha kusikitisha na cha kushangaza,jamaa alishtukia tu mke wake ana ujauzito,si ugomvi ukaibuka,mpaka mwanamke akasema aliyempa ujauzito,kuwa ni mwalimu wa kwaya kanisani kwao, na ameshaondoka, kiukweli jamaa aliumia sana moyoni jambo lililopelekea jamaa kuuza kitegauchumi chake alichokuwa anamiliki na kuondoka,amemuacha mwanamke walipokuwa wamepanga,yamkini kodi ikiisha atarudi kwa babake. Hii comment naifungulia uzi.