Kijana wa miaka 28 anywa sumu baada ya kuambiwa mtoto aliyekuwa akimlea si wake

Kijana wa miaka 28 anywa sumu baada ya kuambiwa mtoto aliyekuwa akimlea si wake

mara nyingi genetics hua haingopi ukiona mtoto hafanan na baba au mama 90% umepigwa


nenda kafanye DNA test haraka
Na mtoto hawezi fanana na wewe 90% kama hauna sura ya hivi.
1736080655195.jpg
 
kwann walikuwa hawasemi mapema

Lakini naye mbaga alikuwa haoni sura siyake kwa mtoto huyo

badala ya kusema warudishe Hela waombwe warudishe uhai wa marehemu
Ukiona mke wako kila saa anasema yani ka junior kamefanana na baba yake mara yani "huyu ni baba yake mtupu" jua kuna kaharufu ka kupigwa Braza .
 
marehemu nae mpumbavu tu
asa kuambiwa mtoto sio wako ndo ujiue

ye angetulia na kupambana juu chimi azae na ndugu wa iyo familia

uyo mama mkwe anarahisisha tu kurejesha gharama,hajui mtu kajitoa kiasi gani
 
Wazazi ndo wàlitumia busara baada ya binti yao kukiri mimba alipewa na mwanaume mwingine wakaamua kutafuta suluhu. Binti angewaambia wakati wa mimba nadhani pia wangemtaarifu huyu marehemu.
Mabinti acheni tamaa.
wazazi hawana busara hao ilitakiwa wamwambie jamaa akapime d.n.a kujithibitishia

vp huyo jamaa mwingine akikataa, ukiona hivyo wazaz wameona kwa jamaa mpya kuna unafuu kuliko huku kwa marehemu
 
Mtoto hana shida, shida ipo kwa mama, alafu shida kubwa ilikua kwa mwanaume.
Unajiuaje kwa jambo dogo kama hili?
Sio dogo linaumiza umelea mimba umejitoa sadaka kwa mambo mangapi ili mtoto na mama wawe na afya mkuu inaumiza kuna muda mwanaume unaamua kuyavaa madeni ili kuweka mazingira ya familia safe kazini unapambana ukijua nyumbani nimea acha watu wawili wana niangalia mimi nikizembea tu nawaangusha
 
JUSTINE AMEFARIKI BAADA KUAMBIWA MTOTO SI WAKE

Mwili wa kijana Justine Mbaga mwenye umri wa miaka 28 ambaye amefariki dunia jana Februari 11,2025 ikidaiwa ni kwa kunywa sumu baada ya kupewa taarifa kuwa mtoto aliyekuwa anamhudumia si wake, umezikwa leo katika makaburi ya Magegele yaliyopo Halmashauri ya mji Makambako.

Taarifa zinaeleza kuwa siku ya jumapili Februari 9,2025 familia ya binti ya aliyekuwa naye kwenye mahusiano walimwita Justine Mbaga, na familia yake na kumweleza kuwa mtoto ambaye alikuwa anamlea si wake, jambo ambalo lilipelekea kuathirika kisaikolojia na kuchukua uamuzi huo.

Baadhi ya majirani wa Justine Mbaga wamesema kifo cha mpendwa wao kimewaacha na majozi mazito kwani alikuwa ni kijana mwenye maadili mema.

Ratifa kibiki ni, mama mzazi wa binti mwenye mtoto huyo anayedhaniwa ni mtoto wa Justine Mbaga akizungumza na El olama fm amesema waliamua kumuita Justine Mbaga na Familia yake na kuwaeleza kuwa mtoto huyo si wao kwani aliona si busara Justine aendelee kulea mtoto ambaye si wake.

Aidha Mama huyo amesema binti yake alikuwa tayari kurejesha gharama za matunzo ambazo Justine Mbaga alizitumia kumlea mtoto huyo ambazo ni 850,000/=.

Diwani wa kata ya kitisi Nevy Sanga na mtendaji wa mtaa wa Kisingire,wameiasa jamii iache tabia ya kuchukua sheria mkononi hasa inapojitokeza changamoto yoyote kwenye maisha.

🎥
✍️

View attachment 3234433
hata tusimlaumu, roho ya mauti ikikuambata yeyote anaweza kufanya lolote, hata kama hangejinyonga ila as long as roho ya mauti ilikuwa inamwandama, angekufa kwa kingine hata ajali tu. Uzuri uliopo ni kwamba, Yesu Kristo alikufa, akazikwa, siku ya tatu akafufuka kwa kuishinda mauti, uwapo uchungu wako ewe mauti, Yesu Kristo ana nguvu kuliko mauti yeyote ile, Yesu KRisto anao uwezo kureverse mauti yeyote, Yesu Kristo, ukisoma Isaya 53 inasema alipigwa na kuuawa badala yetu, chochote alichofanyiwa, ilikuwa kwa niaba yetu kwa ajili ya kutukomboa sisi toka kwenye hiyo hali.

Ushauri kwenu, kama hauna Yesu Kristo moyoni, okoka haraka, ili Yesu akuponye na mauti, akuepushe na mauti, au la, wewe binafsi utapambana na mauti na hautashinda, na elewa kwamba, kwa uwezo wako hautaishinda mauti, anahitajika yeye aliyeishinda mauti, ndiye Yesu Kristo mnayemkataa. Mungu awasaidie.
 
Sio dogo linaumiza umelea mimba umejitoa sadaka kwa mambo mangapi ili mtoto na mama wawe na afya mkuu inaumiza kuna muda mwanaume unaamua kuyavaa madeni ili kuweka mazingira ya familia safe kazini unapambana ukijua nyumbani nimea acha watu wawili wana niangalia mimi nikizembea tu nawaangusha
Kwanini ajiue sasa? Kama wanaume hili tulikatae kwenye vikao vyetu
 
Kuna kipindi nilitaka kujiua kisa nimeachwa na mpenzi wangu,nilikaa na msongo wa mawazo takribani 7days akili ilipokaa sawa,nikajiona ni mpumbavu haiwezekan nife kwa ajiri ya nyapu! Na kukaa na mpenzi mmoja inawafanya vijana wengi wajiue linapokuja suala kuwa wameachwa. Hao wazazi wa binti wampeleke huyo mtoto kwa babake na sheria ichukue mkondo wake. APUMZIKE KWA AMANI ila amefanya maamuzi ya kipuuzi mno
 
Back
Top Bottom