Kijana, Wapi uliteleza hadi kuharibikiwa kimaisha?

Kijana, Wapi uliteleza hadi kuharibikiwa kimaisha?

Wengine mnafanyaje fanyaje unapita mbezi beach africana , washkaji agemate tu wa BMW ,maduka makali yanguo na wako smart tupeane mbinu wazee
Kuna jamaa anakujal kasi.. soon katoboa na idea yake presentable. Anatoboa yuleee na ni upcoming billionaire. Vijana teknolojia Ina Fursa.


Stay turned
 
Mbona ww husemi yaliyo kukuta
Safari yetu ya utafutaji katika dunia hii imejaa misukosuko mingi sana either ya kifamilia, ndoa, kazi na kipato.

Wapo watu chungu nzima dunia hii inawasulubu na hawajui wafanye nini kila wanalofanya linakwama iwe ajira, mahusiano na kipato.

Wapo watu ambao mambo yao yamewanyokea kutokana na juhudi zao saizi wana usafiri, wanavaa safi na kusaidia familia zao kiasi kwamba wanaona wengine wazembe

Mfano mimi nimewahi pata msala katika utafutaji kama sio ndugu na washkaji zangu kunipa faraja, ushauri sidhani kama ningefika hatua moja mbele. Ilifika hatua nikamuomba MUNGU.

why Umeruhusu haya majaribu?

Shusha uzoefu wako ni msukosuko upi huwezi usahau ,na ulijikwamua vipi?

Na ambao mambo bado tafrani wafanyaje waweze kupata nafuu?
 
MWANAMKE..

Nilikuwa na mwanamke kipindi fulani nikiwa vizuri kiuchumi. Nilimsomesha pia. Baada ya kumaliza alipata kazi. Ikumbukwe nilipata nae mtoto mmoja.

Baada ya yeye kupata kazi bahati mbaya maisha yangu yaliyumba sana kwa kuwa nilisimamishwa kazi kampuni niliyokuwepo wakati ule. Nilianza upya kutafuta kazi hadi kwa kuhonga ili niingie kwenye vitengo ila haikuwa hivyo, nilifeli.

Nilijikuta akiba yote imeisha nikiwa sijapata kazi, hapo ndipo mambo yalianzia. Mwanamke alianza kujazia sehemu zenye mapungufu japo kishingo upande, zikaanza influence za kwao kuwa aondoke kwangu sababu sina mchango wowote tena.

Aliondoka na vitu siku moja nikiwa safari kufukuzia kazi. Nilipigiwa simu tu na watu wa karibu kuulizia mbona ninahama. Asikwambie mtu, from there nikaanza kuishi kama kuku, kuzurura tu. Again I started from Zero. Hakuna alienielewa, si wazazi wake wala yeye. Home wakaniambia nipotezee tu.

Ni mengi sana yalipita nikipata time nitashusha kila kitu. I thank God, nilipata kazi tena kampuni jingine and from there my life is back on track. Sina vikuuubwa ila ninaishi maisha yangu.

Dah bonge la story
 
SDsss
Forex

Mwaka 2017 ninamaliza chuo nikakutana na hilo dubwana mkuu wa kuinfluence bwana ontario...kwanza niseme ktk watu waliopata utam wa hii kitu kipnd kile tupo kwenye magroup ya wale wasouth aliewaleta ontario na mm nilikuemo niliweza kupandisha dola 100 mpaka 5000,,,kula bata club madem yaan unaish km vile muvi ukienda kwenye computer ukiclick masaa2 maokoto hayo km yote...mapcha pcha yakaaza mara soko liende tofauti mara tamaa ya kutaka utajir chap mara broker acheze na machart mara news yani balaa kipindi hiko ndugu zangu wananipgia connection za kazi mara hii mara ile wengine full kunifata adi nyumbani kwann sionyeshi ushirikiano mm wala sieleweki najiona nimepata deal kumbe mm ndio deal lenyewe mpk kufika 2019 nimeshakua km teja yani akili inawaza malambogn ferari mansion...huku nikuchoma account na kufund account uko kwenye circle ile ile mpaka nakuja kushtuka nimepoteza mda na pesa kibao na kazi kibao daah yaan acheni kabsa..2020 nikaachana kabsa na fx nikabadili mfumo wa maisha nikaanzsha biashara ndogo ile biashara ikazaa nyngne, nikakuza mtaji now nipo kkoo napambania kombe alhamdulilah bado najitafuta sjajipata vzur ila 7figure kwenye account znasoma.

Hustler migogoro junior
Kama mimi ndugu yangu, ile namaliza shule tu naingia mtaani 2009 nakutana na dada mmoja kwa huruma na mapenzi nikamchukua geto nilikaa miaka minne alitemana na mimi kama mtu ambaye hajawahi kuonana naye maishani mwake, nilipoteza vingi kwa ajili yake, hadi leo 2023 japo nina maisha mengine lakini athari za yule dada bado zipo.
Mapenzi na huruma zetu wanaume dhidi ya wanawake zimechangia sana kutuwekea kwenye daraja la umaskini kwa kiasi kikubwa.
 
Brother nakupa pongezi sana kwa kutufungua macho, unachosema ni kweli kabisa. Sisi watanzania siasa za ujamaa zimeturudisha nyuma sana. Yaani unakuta mtu anasubiri kupewa, kuna msemo "mgaa mgaa na upwa hali wali mkavu". Amini usiamini ukipambana na ukizunguka utakuja kukutana na fursa ambazo hukutegema kukutaa nazo.
Kwel mkuu, kikubwa n kuwa na uthubutu yaan
 
Kitu kingine nilichojifunza maishani ni swala la kukopesha ndugu na marafiki, I learned this the hard way, nimepoteza hela nyingi sana takribani milioni 9 kwa kusaidia ndugu ambao hawana shukrani, kuna huyo nilimpa milioni 5 hadi leo hajanilipa na hana mpango wa kunipa. Unaenda kudai hela mtu anakuchamba.
Namshukuru mungu nimewasamehe na sina kinyongo na ndugu yangu yeyote, kwa sababu naamini ndugu na rafiki ni watu muhimu sana maishani kuliko hata hela.

Kitu chingine ambacho vijana inabidi tujifunze ni kwamba, kuna kipindi flani katika maisha yetu, mungu hufungulia baraka zake, tunajikuta tunapata hela nyingi sana ambazo sometimes hajutui tuzipeleka wapi au tuzitumiaje.
Huu ni muda ambao inabidi tuwe makini sana kwasababu Lucifer(Ibilisi) hutumia nguvu sana kutuyumbisha na kutuingiza kweny mienendo isiyofaa ili tutumie hela vibaya kwa mambo ambayo siyo ya msingi kama pombe, ngono, kuzurura, mavazi expensive, na expenses zingine zisizo kuwa na umuhimu.

Hakika nakwambia ukiweza kutumia huu muda ambao kipato chako kipo stable na madili yanatiki vizur na kuepukana na zinaa, utakuja kuwa na uzee wa baraka sana, hutasumbuliwa na magonjwa, hutasumbuliwa na uchumi mbovu, utaweza kusaidia familia na ndugu zako wengine vizur, utakuwa baraka kweny ukoo wenu.
Sisemi uongo mm mwenyew ni mhanga wa kwenda viwanja, weekend hivi kama leo nisipoenda viwanja najihic kabisa mwili unauma, japokuwa situmii pombe wala kilevi chochote(kwanza siwez, siku ya kwanza kunywa pombe nilitapika sana)

Ewe kijana mwenzangu ukiona asaiv account yako inacheka basi jua muda wa kuwa makini sana.
Lucifer(Ibilisi) hataki tuwe matajiri, anajua tajiri anaweza kujiamulia maisha ya kuishi, maskini hawez, maskini hata akiambiwa sujudia sanamu nikupe millioni kumi anakubali kwasababu maskini anaamuliwa maisha ya kuishi.

Chingine jamani, tukumbuke kilimo na ufugaji, hasa tulioajiriwa, mkulima huwez kumwona anamlilia mwanasiasa amlipe mshahara, mkulima ana uhakika wa kula hata kama hana hela mfukoni, chochote unachofanya hata kama wewe ni rubani hakikisha unalima na kufuga(sio lazima uwe mkulima mkubwa hata ukiwa na bustani nzuri ya mbogamboga na kuku wa idadi flani inatosha), serikali haitabiriki tuachane na mambo ya kuwategemea wanasiasa hawa.
Mwakani mungu akinibariki naingia kweny kilimo na ufugaji rasmi.
 
Back
Top Bottom