1. Kufanya partnership na mtoto 2a kishua.
Baada ya kufunga ndoa nilikuwa sina ajira nikachukua zile hela za zawaditunazope2a na kamati. Baadhi nikanunua bodaboda enzi zile chombo ilikuwa fekon 150. Nyingine nikafungua duka la uzushi la chakula na kufanya mishe zingine.
Sasa kutokana na kuwa na njaa ya mafanikio pale kwenye fremu nilizokuwa nimepanga alikuwa Mzee mmoja wa kishua ameritire alikuwa na vijana wake rika sawa na wote tulikuwa tumemaliza degree za kwanza. Walikiwa na Yale mafriza makubwaa sijui futi sita walikuwa wameliweka ndani.
Huku shop ikiwa inaendelea kuchanganya kwa kuwadaka kama ntilie wanakopa jioni maharage, unga wa ngano, mafuta na Michele kesho yake wanafanya biashara jioni tena wanarudisha, wakawa wanafuata samaki mbagara. Nikaona hii fursa. Nikawashawishi wale vijana kuwa hii fursa tujipange mimi nakodi fremu kwa Mzee na nyie mtoe friza kwa mshua mimi nitatoa mtaji wa kuuza samaki tuuze tugawane faida itakayopatikana. WIFE ALINIONYA AKASEMA BORA TUKOPE FRIZA JAPO KWA KUANZIA DOGO,
Tukaandika proposal kupeleka kwa mshua wao akasema very good. Mimi nawapa fremu Bure na akaweka order ya samaki tasi kwa wiki kilo 4.
Enzi box la samaki yalikuwa kati ya kilo 10 Hadi 20 pale mbagara. So unatakiwa udamke asubuhi unaingia pale mbagara kwa nyuma unachukua mzigo kilo zako 30 za samaki aina tofauti tofauti huku wameganda wakifika utawadumbikiza kwa friza.
Mtaji ulikuwa kama 300k niliotenga.
Biashara tulikuwa tunafanya vyema japo mwanzoni ilikuwa na ugumu fulani maana wateja wapo scarted, faida ilikuwa ukinunua mzigo wa 60 unapata 30 au 40 kabisa. Maana kilo unanunua 6000 jumla unauza 10 au 9.
.tukafikia Hadi kilo 100 kwa wiki..
Sasa kutokana na kuoenda kazi mimi nikawa natafuta soko kwa mama ntilie, wadosi wa kanisani, mtaani, kwenye kuuza nikawa nawachia majamaa.
Sasa kwa sababu fremu ipo karibu na nyumbani, wanakaa wanaangalia tv na maseries mteja anaita wee mwishowe wanaondoka. Muda mwingine wanaitwa na wife wanamuuliza anataka kilo ngapi alisema kilo au nusu wanasema anatusumbua. Au unaweza ukawa umepigiwa simu na mama ntilie.naomba niletee samaki kilo 2 wanakujibu poa then hawapeleki wapo busy na tv. Generally walikiwa ni wavivu sana. Ila faida wanapenda
Siku moja nikawaonyesha msg toka kwa mdosi analalamika jamaa walivyomjibu mke wake shits.. nikamwomba msamaha.
Mzigo ulipokuwa mkubwa kubeba hizo kilo mia Mzee wao alitupa kirukuu tubebe samaki badala ya kukodi Bajaj,
Machangamoto yakaanza.
1. Wakienda wao mzigo wanachukia wa Bei rahisi kumbe umeanza kuchili then wakiwa box hawapokei serious na kazi wanakaa kwenye gari wanapakia mzigo mbovu. Kwa hiyo kama tasi wamechukua 20 kg maana watauza mbili au 3 then 17 inatupa au unauzia nusu Bei ila uwe umekwangua mifupa pembeni ndo wanakubali kununua huo mzigo.mbovu.
Ukiwaambia wanakujibu utakuwa tajiri kwa 5m au 2m wewe tafuta hela uagize mzigo mwanza. Kwanza faida hakuna kwa sababu vitu vingi tumepewa buree kwa tukiweka real investment hakuna faida hapa. Then wanajadili bifu la kalapina na chid benzi sijui diamond na mtu gani.
2. Hawaheshimu hela ndogo ndogo anajiunga bundle na hela ya mauzi dukani then anasema faida yake kaitumia. Au akiwa na ratiba ya kugonga Malaya anachukua 50 hapo then anasepa.
3. Show off zikawa nyingi. Anakuja na mademu zao anawaonyesha hapo ndo nipo now days anashinda hapo hafanyi kazi ataingia mchana akula demu wake wakati wa kuondoka anakuja anakuomba nauli then anamsindikizq demu wake. Sasa Ukiwaambia ukweli wanakuona mdwanzi. Wakati wewe ukipata kifaida unaweza upanue biashara, ufanye maendeleo kidogo..
Sasa niliwahi kuitwa kwenye kazi ya muda wa miezi 6 hivi yankusafiri ilikuwa inalipa maana kwa siku walikuwa wanatoa kama 75 hivi.
Nimeeenda nimekaa miezi miwili nikaambiwa biashara imekufa...
Yani kama ningekomaa mwenyewe ningekuwa mbali...
Usifanye biashara wa watoto wa kishua