DOKEZO Kijiji cha Kazuramimba (Uvinza, Kigoma): Mauaji yaliyofanywa 4/10/2023 ninayekemea kwa nguvu zote, Majeruhi wako wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hii habari ya upane mmoja ila mambo kadhaa ujiulize:-
1. Mchawi kakimbilia polisi, ingelikuwa ni busara muache polisi wachukue hatua ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kama uchawi ni jinai na kama si jinai basi aachiwe na kama wananchi wa Kazuramimba hamtaki uchawi basi mkubaliane mbunge wenu aombe serikali itunge sheria ya kupiga marudfuku uchawi,

2. Je, ni sahihi kuvamia na kuvunja kituo cha polisi? Be it mhalifu yupo ndani ama si mhalifu, jibu ni HAPANA, Polisi wanajitolea maisha yao kutulinda, ni kosa kubwa sana kuvamia kituo, kosa kubwa sana.!

3. Nini kifanyike, Serikali itangaze baadhi ya mikoa kuwa huru kwa wachawi, SUMBAWANGA, SHINYANGA, KIGOMA , SIMIYU na GAMBOSHI iwe makao makuu ya wachawi.
 
Eti "Raia wakamfuata hukohuko...."[emoji15][emoji15]

Sisi Raia tuna wajibu wa kulipenda taifa letu kwa UTII WA SHERIA BILA SHURUTI...

Raia yupi MWEMA anaweza kuthubutu kukishambulia kituo cha polisi ?!!![emoji15][emoji15]

Je hao si magaidi ?!!!

Lengo lao si kupora silaha ?

Lengo lao si kutorosha WATUHUMIWA WENGINE?!!

#Wananchi Tuipende Tanzania Yetu [emoji120]
 
Ukishavamia kituo cha polisi basi hilo ni kosa

Ova
 
[emoji7][emoji7][emoji7][emoji2956]
 
Hapa mambo yasiwe mengi, huyo mchawi aendelee kuishi polisi. Akirudi mtaani wahuni wataishi nae tu. Haiwezekani utese watoto wa wenzako halafu ubakie salama.

Uchawi hauna udhibitisho ila haimaanishi kwamba haupo. Swala la kuamini upo au haupo bado inabakia kuwa hiari ya mtu binafsi.
 
Ila hali imayoendelea huko siyo haki, ule ni udhalilishaji kwakweli. Unamtambuaje mchawi kama na wewe siyo mchawi?
Km wapo ngoja wanyooshwe. Wachawi na washirikina ni adui wa maendeleo. Kumjua ni rahisi km na wao wanavyodhuru watu kirahisi. Sema hawa watu kabla hawajagusa familia yako huwezi kuamini ila viashiria vya kifo chenye utata vikiikumba familia yako hata imani yako utaiweka pembeni.
 
Raia kuvamia kituo cha polisi ni kosa kubwa sana.
Smg hapo unafungulia (blast) unaminya trigger hadi ziishe
Hao askari mnavyowatetea laiti kama wangekuwa wanawajali kiasi hicho hata CCM wangekuwa washaachia madaraka kitambo. Wao wamelinda uhai wao tu huyo raia angekuwa anafilimbwa mtaani usingeona wakisogeza hata pua
 
Kuna watu Wana ujinga mwingi sana kichwani. Yaani wanafanya nakosa ya wazi sana ambayo hata kuchomoka kwenye mkono wa sheria ni ngumu.
Hakika mkuu wangu....

Hakika [emoji106]

Tunashindwaje kudai HAKI zetu pasi na kuvunja SHERIA NA AMANI ???? [emoji45]

Inashangaza mno...
 
Siungi mkono uchawi lakini pia siungi mkono kujichukulia sheria mkononi ikiwa kuna mamlaka za usalama.

Jambo lolote unalolifanya lifanye kwa manufaa yako wewe na familia yako pasi na kuwaaangamiza au kuwaingiza katika matatizo wenzio.
 
Siungi mkono uchawi lakini pia siungi mkono kujichukulia sheria mkononi ikiwa kuna mamlaka za usalama.

Jambo lolote unalolifanya lifanye kwa manufaa yako wewe na familia yako pasi na kuwaaangamiza au kuwaingiza katika matatizo wenzio.
Sasa hukumu ya mchawi itatolewaje na mamlaka ambayo haiamini uchawi? Hio inatolewa na magwiji wa uchawi ambao wanamtambua mchawi huyo ambao ndio hao kamchape na sio kuwa wanawaua ila wanawavua vyeo tu. Sasa kama sio mchawi anaogopa vipi kuvuliwa vyeo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…