Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Hii habari ya upane mmoja ila mambo kadhaa ujiulize:-Wakuu, hii Nchi ya Ovyo sana, Kuna wajinga wanapopewa nafasi Huwa wanageuka kua Miungu watu.
Jana tarehe 4/10/2023 Kijiji Cha Kazuramimba, Wilayani Uvinza kulitokea vurugu baina ya Polisi na Raia, zilizopelekea Polisi kutumia Silaha za moto, hali hii ilipelekea Raia Kadhaa kufa na wengine kujeruhiwa .
RC, RPC na DC, wakaamua kuzitembelea Hosp zilizopokea majeruhi kimyakimya na kuwaonya kutotoa Taarifa.
Chanzo cha Ugonvi...
Kuna waganga walipelekwa Kijiji huko Kwa Imani za kijadi kwamba wanatafuta wachawi, Kuna mji Mmoja mwenye mji huo akagundulika na Mchawi, Akakimbilia Polisi kishtaki.
Polisi wakamficha hapo na Raia wakamfata hukohuko.
Kukosekana Kwa Busara baina ya Polisi na Raia,. Fuji zikatokea na kituo Cha Polisi hiko kikavunjwa.
Polisi wakaanza kutumia Silaha za moto yaan Bunduki kushambulia Raia.
Raia wengi sana wamejuruhiwa, Vijana, Wanawake na watoto na wazee wameumizwa sana.
Polisi wamewakamata watu Kadhaa na majeruhi Kadhaa na kuwapeleka kusikojulikana, mpaka Sasa Ndugu wanafuta Ndugu zao .
Ni majeruhi wachache tu Tena waloamua kujipeleka Hosp ndio ambao wamejulikana mpaka Sasa ,huku wengine wakiwa hawajulikani.
Polisi wa Kigoma, wanaongoza kuwa na matukio ya "Majeruhi alinyakua Bunduki ya Polisi nakuanza kurushiana risasi ".
Ndugu zangu nawaomba sana Mnisaidie Kupaza sauti,. Ndugu yangu Yuko huko Kikazi, amesombewa humohumo , mpaka Sasa hatuma Taarifa ya uhai au lolote kumhusu yeye.
1. Mchawi kakimbilia polisi, ingelikuwa ni busara muache polisi wachukue hatua ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kama uchawi ni jinai na kama si jinai basi aachiwe na kama wananchi wa Kazuramimba hamtaki uchawi basi mkubaliane mbunge wenu aombe serikali itunge sheria ya kupiga marudfuku uchawi,
2. Je, ni sahihi kuvamia na kuvunja kituo cha polisi? Be it mhalifu yupo ndani ama si mhalifu, jibu ni HAPANA, Polisi wanajitolea maisha yao kutulinda, ni kosa kubwa sana kuvamia kituo, kosa kubwa sana.!
3. Nini kifanyike, Serikali itangaze baadhi ya mikoa kuwa huru kwa wachawi, SUMBAWANGA, SHINYANGA, KIGOMA , SIMIYU na GAMBOSHI iwe makao makuu ya wachawi.