Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Mkuu Waziri, hayo maneno 'fikirishi' yenye maana zaidi ya moja, mngelikuwa mnayabold.Tatizo linaanzia huku chini, hao walimu wakuu wa vyuo hawana shida
Sent using Jamii Forums mobile app
Zile diploma za zamani huwezi kulinganisha na degree za mwendokasi za sasa. Kuna mzee tulikuwa naye ofisini, amestaafu kwa sasa. Akiwa ofisini hata kama haupo wala huna wasiwasi, wakati mwingine nikiwa hata na shaka kidogo na hii Masters yangu lazima nipate opinions kutoka kwake hasa kwenye ishu za field. Hawa wahitimu wa sasa kata-K sijui tutafika wapi...hili la graduate makazini ni tatizo liangaliwe kwakweli wahitimu wa sasa wanasomea wapate vyeti na kuvaa joho wapige picha lakini field ni utumbo mtupu
Sent using Jamii Forums mobile app
Yule wa digrii ya "korosho" asiye na uwezo wa kutema ngeli alitoa rushwa ya ngono pia?Hiyo ya wahitimu ni kisingizio tu.
Hoja walioijia hapo ni rushwa ya ngono na maadili tu.
Wasidanganye watu.
Hizo barua za amombi ya Kazi wanazianfika kuomba kazi gani?
Magu anaajiri madereva na JKT tu.
Nenda website ya utumishi utakuta kazi zinazotangamwa ni madereva
Maelezo yale ni mapana na ni technical, nikiwa na muda nitaeleza vizuriHivi hili jambo huwa linasemwa, lina ukweli wowote?
Mwanamke anabaka! Anabakabakaje kwa mfano?
Ukibadili neno na kusema anashawishi ili kuhiyari tendo ama kwa vitisho, hilo lawezekana kubaka kisaikolojia, lakini siyo kubaka live kama 'baka' tunayoiongelea.
Na ndiyo maana kuanzia mashuleni wasichana kujazwa mimba,pamoja na hii sheria kandamizi ya miaka 30 jela, inayotumika sasahivi, wanawake haiwahusu.
Sent using Jamii Forums mobile app
I have nothing to commentKuna tetesi kuwa kikao cha dharura kimeitishwa mjini Dodoma kinachowakutanisha wakuu wote wa vyuo vikuu nchini.
Hatua ya kuitia kikao hicho imetokana na hali mbaya ya wahitimu wa vyuo vikuu nchini ambapo mara wanapoajiriwa katika sehemu mbalimbali wanashindwa kufanya kazi ambazo zingine ni rahisi kabisa.
Wahitimu wengine wanashindwa kuandika barua za maombi ya kazi, kushindwa kufanya majaribio mbalimbali na hata pia kushindwa kuandika taarifa kwa kwa lugha ya Kiswahili na pia kwa lugha ya kiingereza.
Waziri wa elimu profesa Ndalichako ameamua kuitisha kikao hicho kujadili kuona wapi kuna tatizo.
Pia kikao hicho kinatarajiwa kujadili hali ya utoaji wa rishwa ya ngono kwa wanafunzi wa kike vyuoni ambapo huahidiwa alama za juu ili kufaulu mitihani yao ya mwaka wa mwisho kwa masharti ya kushiriki vitendo vya ngono na wahadhiri wao.
Ni muhimu taarifa kama hizi zikawekwa kwenye umma ili kuuelimisha kuhusiana na hali halisi ya kudorora kwa kasi ya juu kwa utaji wa elimu ya juu nchini na kuachia wanafunzi khasa wa kike kutegemea kutoa miili yao ili kupata alama nzuri.
Hilo nalo neno mkuu..
Kuna tetesi kuwa kikao cha dharura kimeitishwa mjini Dodoma kinachowakutanisha wakuu wote wa vyuo vikuu nchini.