masdinero masproblemas
JF-Expert Member
- Mar 19, 2022
- 224
- 177
Mimi naona ni suala la uimara wa saikolojia.Hivi nyie mnao umizwa na hii kitu mapenzi, hua mnaumia wapi??
Yaani nikikuuliza unaweza ukanionyesha panapo una kwasababu ya mapenzi??
Kuna mtu kaniambia eti anaumia kwasababu ya mapenzi, sasa nimemuuliza anionyeshe mahali panapo muuma
Kama ni mtu wa kufikiri kwa mpangilio huwezi kutumia muda mwingi kuwaza sana mapenzi.
Jamii ilivyo inafundisha watu kulalamikia mapenzi na hizi porojo za kudai moyo umefanya hiki na kile. Tumia akili. Hisia zisikuendeshe.
Binadamu kwa jinsia zetu zilivyo tumezaliwa ili tuzae. Miili yetu imejaa vimelea kibao. Ndio uhai.
Hivi vina lengo moja tu. Kutawala dunia kwa kujitandaza kila sehemu. Vimelea vyetu vikikomaa vinakuwa na mikakati mingi ya kujilinda kufa na kuendeleza uzalishaji wake.
Katika harakati hizo hawawezi kutegemea mwili mmoja. Lazima watafute koloni lingine ikitokea umekufa ghafla au utapozeeka. Basi vitahangaika hadi uzae mtoto.
Hapo vitafurahi. Lakini kwa vile havioni wala kuelewa kinachoendelea nje vitaendelea kutaka kujisambaza tu. Utazaa tena na tena kama mjinga. Hivi ndio vinaendesba miili yetu.
Ukiona unavutiwa na mtu sio wewe kichocheo cha kwanza ni vimelea vyako mwilini. Vinakusukuma ukafanye kazi yao wasambae. Sasa hapo ndio muda wa kuhamishia ufahamu wote kichwani. Peleka damu kichwani. Fikiria. Bila hivyo utajikuta uko na jitu la ajabu tu.
Mahusiano yakifika mwisho ulalame moyo wakati kumbe ni wewe kushindwa kutumia akili. Hata ukilia umetendwa inasaidia nn kama sio udhaifu?
Kuna watu "wanatendwa" na mapenzi toka wadogo sana. Mtu analia kabisa chozi konki. Utasema anaigiza na kucheka. Moyo unauma eti. Hamna kitu.
Ni ishu ya kisaikolojia ila jamii imeamua kulifanya jambo la moyo. Moyo hauna hatia yoyote. Kazi yake ni moja tu toka mimba inatungwa.
Siku ukisimama jumla ndio mwisho. Hauna kazi ingine zaidi ya kuupa uhai mwili.