Kikatiba Rais Samia yuko sahihi kumteua Naibu Waziri Mkuu

Kikatiba Rais Samia yuko sahihi kumteua Naibu Waziri Mkuu

Kinachompa usahihi Rais ni kwa kuwa yuko juu ya sheria na hata kwenye katiba yenyewe anachokifuata ni kile kinachomnufaisha yeye mwenyewe,ndio maana hawataki kusikia kabisa neno katiba mpya.majibu yao ni mwananchi wa kijijini haitaji katiba mpya,elimu itolewe kwanza miaka 3 utafikri watanzania ndio mambumbu wa dunia nzima,mpaka hawaelewi nini maana ya katiba.
 
(2) Rais atakuwa na madaraka ya kuteua watu wa kushika nafasi za madaraka ya viongozi wanaowajibika kuweka sera za idara na taasisi za Serikali, na watendaji wakuu wanaowajibika kusimamia utekelezaji wa sera za idara na taasisi hizo katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, nafasi ambazo zimetajwa katika Katiba hii au katika sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge kwamba zitajazwa kwa uteuziunaofanywa na Rais.
Petro E. Mselewa

Hiyo nayo imekaaje? Katiba inasema "nafasi ambazo zimetajwa katika katiba hii au katika sheria mbalimbali"

Sasa nafasi ya NAIBU WAZIRI MKUU imetajwa katika ibara gani ya katiba hii? Au katika sheria gani iliyotungwa na bunge?

Hebu tujadilianeni
 
Mkuu, Ibara ya 36 (1) inahusu kuanzisha nafasi za kimadaraka ambazo si lazima zitajwe kwenye Katiba. Pia, inahusu kufuta zile nafasi zinazotajwa kwenye Katiba au ambazo zilishaanzishwa. Ibara ya 36 (2) inahusu mamlaka ya Rais juu uteuzi wa nafasi zilizotajwa kwenye Katiba.

Ndiyo kusema, Ibara ya 36 (1) inatoa mamlaka kwa Rais kuanzisha nafasi ambazo si lazima ziwe zimetajwa kwenye Katiba. Mojawapo ni ya Naibu Waziri Mkuu ambayo imeanzishwa jana.
 
Ni sawa lakini ;

Huuoni kuwa huu utata unakuja kwa sababu sisi hatuna "enumerated powers doctrine" kwenye mfumo wa Katiba yetu, kama baadhi ya nchi?

Na Je si kwamba, kama kitu kwenye Katiba hakijasemwa kwamba kiwepo maana yake kimekatazwa na hivyo hakipaswi kuwepo?
 
You have a point Mkuu!
 
Hiki cheo hakina maana yoyote ni ufujaji wa fedha za walipa kodi tu, miaka ya nyerere na mwinyi waziri mkuu alikuwa pia ni makamu wa rais, na mambo yalikuwa yanakwenda, sasa nafasi hiyo moja inashikiliwa na watu watatu ambapo zamani ilikuwa ni mtu mmoja .. huko ni kujiongezea vyeo vya anasa tu na kuwatwisha mzigo mkubwa wananchi maskini.
 
Back
Top Bottom